Je, tukemee udini, ukanda na ukabila au? Je, neno Sukuma Gang si neno la kibaguzi? Mnaonaje tukiungana kukemea ubaguzi wowote kwa jina lolote?

Je, tukemee udini, ukanda na ukabila au? Je, neno Sukuma Gang si neno la kibaguzi? Mnaonaje tukiungana kukemea ubaguzi wowote kwa jina lolote?

Mosi Magufuli hakuwa msukuma alijibanza katika usukuma labda uniambie kama Burundi kuna wasukuma siku hizi.

Pili ,kuhusu ukanda ,ukabila ,undungu katika serikali yake ulishamiri mfano mdogo tu ni je mpwa wake alistahili kushika nafasi ile pale hazina na hakukuwepo na watu senior zaidi yake ?

Tatu je Magufuli alipokuwa anasema wakichagua watu wasio wa CCM hatoleta hata maji rejea walichoambiwa watu wa Tunduma .

Nne , je Magufuli alipokuwa akiita raia wa kigeni na waliokuwa wakipingana na mambo yake majina kama "mabeberu " na "vibaraka wa mabeberu" bila ushahidi usiotia shaka mbona hamkuonekana kuumizwa.?

Tano, Magufuli alisema wafungwa wafanyishwe kazi usiku na mchana wanaonyesha kuchoka wapigwe mateke na wafanyishwe kwa lazima je hii haiko kinyume na haki za binadamu na watu waliishia kupiga makofi ya pongezi .

Mkizungumza chuki na mgawanyiko mkubwa ulioletwa na awamu yake basi msisahau kufanya rejea ya matendo na kauli zake zilizoleta migawanyiko.

Wasukuma kama Wasukuma ni watu wema sana.

Wasukuma kama Wasukuma ni watu wachapakazi sana.Ni wakulima wazuri,ni wafugaji wazuri.

Wasukuma ni kabila ambalo wanawake wao wanaheshima sana.Wanawake wa kisukuma ni rahisi kuishi na kuolewa na makabila mengine.

Nijuavyo mimi Magufuli hakuwa msukuma alijinasibisha na usukuma ili kutimiza ajenda zake mbaya.

Nadhani itakuwa ni makosa makubwa iwapo siku za usoni msukuma atanyimwa nafasi ya uongozi wa juu kwakutumia kigezo cha uovu wa Magufuli.

Ni kweli tena pasipo shaka kwamba katika Utawala wa Magufuli Wasukuma walipendelewa sana.

Kabila la Wasukuma ni kubwa labda wapo 15 Million lakini waliopata upendeleo hawazidi 200.Sasa kwanini tuwahukumu watu 15 Million kwa hoja ya upendeleo wa watu 200.

Katiba mpya na bora ndio mwarubaini wa kuondoa ukabila & ukanda.
 
Aisee kwa hapa nilipoku quote umenishangaza sana,hivi kwa akili yako unaamini kila mtu anafahamu kiswahili? Kuna ubaya gani kwa huyo Mama kuongea Kisukuma? Bibi na Babu yangu wote hawafahamu Kiswahili,ingetokea wamekutana na JPM na wanafahamu ni Msukuma wangeongea nae kwa lugha ipi? So unawahukumu Wasukuma kuwa ni watu wabaguzi kwakuwa tu yule Mama aliongea na Rais kwa kisukuma?

Kwamba matendo ya JPM ni pamoja na kuongea na yule Mama kwa kisukuma kwako wewe ilikukera sana? Mnajaribu kujificha kwa kuzunguka zunguka lakini deep down mna chuki na ubaguzi mkubwa na Wasukuma.
1. Kuna maswali nimeuliza wewe umekwenda moja kwa moja kunishutumu kuwa nina chuki.

Nimeuliza kama mhusika alikuwa hajui Kiswahili. Pia nimeuliza kama mhusika alihisi njia bora ya "kumuingia" Jpm ilikuwa kumuongelesha Kilugha.

2. Kwa muonekano wake hakuwa Mama mtu mzima. Hivyo inapunguza uwezekano kuwa hajui Kiswahili.

3. Tukio hilo lilitanguliwa na matukio ya Raisi kuzungumza Kilugha mara kwa mara. Hivyo inaongeza uwezekano wa wananchi kuhisi lugha ya Raisi imerasimishwa.

4. Tukio hilo lilitokea nje ya kanda pendwa ya Raisi Magufuli hivyo lilistaajabisha.

5. Sina kumbukumbu ya Maraisi au Mawaziri Wakuu waliomtangulia Magufuli kuzungumza kwa lugha za makabila yao ktk ziara au shughuli za KISERIKALI.
 
Watu wa pwani akina nani? Yaani mnakemea ubaguzi halafu unaletaubaguzi, mimi mnyamwezi lakini nawachukia sukumagang kwa maana ya wanufaika wa itikadi na matendo ya Magufuli
wigo wa kunufaika kivipi , acheni uhuni sukuma gang ni ushenzi usiokubalika,
 
1. Kuna maswali nimeuliza wewe umekwenda moja kwa moja kunishutumu kuwa nina chuki.

Nimeuliza kama mhusika alikuwa hajui Kiswahili. Pia nimeuliza kama mhusika alihisi njia bora ya "kumuingia" Jpm ilikuwa kumuongelesha Kilugha.

2. Kwa muonekano wake hakuwa Mama mtu mzima. Hivyo inapunguza uwezekano kuwa hajui Kiswahili.

3. Tukio hilo lilitanguliwa na matukio ya Raisi kuzungumza Kilugha mara kwa mara. Hivyo inaongeza uwezekano wa wananchi kuhisi lugha ya Raisi imerasimishwa.

4. Tukio hilo lilitokea nje ya kanda pendwa ya Raisi Magufuli hivyo lilistaajabisha.

5. Sina kumbukumbu ya Maraisi au Mawaziri Wakuu waliomtangulia Magufuli kuzungumza kwa lugha za makabila yao ktk ziara au shughuli za KISERIKALI.

Bado unajichanganya tu Mkuu,kwa hiyo umri wa mtu ndiyo una determine kama anajua kiswahili au la? Njoo vijijini huko utakuta hata watoto wapo shuleni na bado hawawezi kuongea Kiswahili na hii siyo kwa Wasukuma tu hata makabila mengine pia.

Hao Marais wengine kama hawakupendelea kuongea lugha zao wanapokuwa maeneo waliyotoka ni wao na haimfanyi JPM aliyependelea kuongea Kisukuma akiwa Mwanza kuwa ni mbaguzi.Njoo na hoja nyingine lakini siyo hii ya Magufuli kuongea Kisukuma na watu wa Mwanza.
 
Certified MBWIGA.
 
Hilo neno sukuma hapo halipo kwa bahati mbaya, haingii akilini et wafuasi wa Magufuli ufikirie kuwaita sukuma halafu useme haihusiani na kabila la wasukuma. Yani mie niwaite mashoga wote kuwa ni wapemba gang halafu niseme haihusiani na wapemba nitaeleweka?
BANYAMULENGE tuliza mshono

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Wasukuma kama Wasukuma ni watu wema sana.

Wasukuma kama Wasukuma ni watu wachapakazi sana.Ni wakulima wazuri,ni wafugaji wazuri.

Wasukuma ni kabila ambalo wanawake wao wanaheshima sana.Wanawake wa kisukuma ni rahisi kuishi na kuolewa na makabila mengine.

Nijuavyo mimi Magufuli hakuwa msukuma alijinasibisha na usukuma ili kutimiza ajenda zake mbaya.

Nadhani itakuwa ni makosa makubwa iwapo siku za usoni msukuma atanyimwa nafasi ya uongozi wa juu kwakutumia kigezo cha uovu wa Magufuli.

Ni kweli tena pasipo shaka kwamba katika Utawala wa Magufuli Wasukuma walipendelewa sana.

Kabila la Wasukuma ni kubwa labda wapo 15 Million lakini waliopata upendeleo hawazidi 200.Sasa kwanini tuwahukumu watu 15 Million kwa hoja ya upendeleo wa watu 200.

Katiba mpya na bora ndio mwarubaini wa kuondoa ukabila & ukanda.
Magufuli alilichafua sana kabila letu pendwa la Wasukuma, aendelee kuteseka tu huko aliko

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Bado unajichanganya tu Mkuu,kwa hiyo umri wa mtu ndiyo una determine kama anajua kiswahili au la? Njoo vijijini huko utakuta hata watoto wapo shuleni na bado hawawezi kuongea Kiswahili na hii siyo kwa Wasukuma tu hata makabila mengine pia.

Hao Marais wengine kama hawakupendelea kuongea lugha zao wanapokuwa maeneo waliyotoka ni wao na haimfanyi JPM aliyependelea kuongea Kisukuma akiwa Mwanza kuwa ni mbaguzi.Njoo na hoja nyingine lakini siyo hii ya Magufuli kuongea Kisukuma na watu wa Mwanza.

..Ni nadra kwa Mtanzania wa umri wa kati kutokujua lugha yetu ya taifa Kiswahili.

..Watanzania wa umri wa kati wana uwezekano mkubwa kuwa waliandikishwa shule na kufundishwa Kiswahili.

..Tukio ninalolizungumzia mimi lilitokea nje ya kanda pendwa, mjini, ambapo mwananchi wa kawaida alizungumza na Mh Rais kwa KILUGHA.

..Kiongozi wa serikali / taifa kuzungumza kilugha ktk shughuli za kiserikali ni jambo lisilokubalika. Sheria zetu zimeelekeza kwamba lugha ya taifa ni KISWAHILI.

..Kuna viashiria vingi ambavyo ukiviangalia kwa ujumla wake utaona Magufuli alikuwa kiongozi aliyepungukiwa uwezo wa kuwaunganisha Watanzania. Wengine wanasema alikuwa kiongozi mbaguzi.

NB:

..Vipi kuhusu kauli ya Rais Magufuli kwamba watu wa kabila fulani hawapaswi kupewa dhamana ya kushika pesa. Je, hiyo haikuwa kauli ya kibaguzi?
 
Samahani mkuu waweza kunitajia Full Ministries achana na Manaibu wa5 tu ambao walikuwa wasukuma kipindi cha JPM ili tulipe uhalali bandiko lako mkuu
1. Leonard Chamuliho Ujenzi
2. Dotto Biteko Madini
3. Medard Kaliman Nishati
4. Elias Kwandikwa Ulinzi
5. Mashimba Ndaki aamaifugo
6. Innocent Bashungwa Habari

Niendelee au umetosheka.
 
Jiulize kwanza kwa nini ni sawa Mtu mweusi kumuita majina ya Kibaguzi Mzungu lkn Mzungu akifanya the same kwa mtu mweusi anaweza hata kufunguliwa mashitaka kwa Ubaguzi? Jibu ni power, mtu mweusi ni weak na Mzungu ni strong ndo maana pia inakubalika kuita Sukuma gang na kukejeli Sukuma jinsi utakavyo lkn Msukuma haruhusiwi kufanya the same kwa wengine bila ya consequences.

Hivyo kwangu Wasukuma ni powerful na wengine ni weak ndiyo maana weak wako sensitive.

Fikiria tu kwa mfano kilema cha macho alichoumbwa nacho Mbowe labda angeumbiwa nacho Magufuli hali ingekuwaje, unafikiri wangemsitiri kama Mbowe anavyositiriwa? Hata watu wanaomchukia Mbowe bado wanamsitiri sijawahi kusikia mtu akikejeli macho ya Mbowe lkn ule upande mwingine wasingejali hivyo ni swala kukosa power, maturity na pia lack of boundaries, Wasukuma wanajua wanajitambua na wanajua power yao na wanaowakejeli ni weak na cowards!
'Macho ya Mbowe' umeyaongelea makusudi kama aina ya kejeli, brain game ulichofanya ni kujulisha/kukumbusha kwa makusudi yaani umetukana/umekashifu.
Wapo wengi humu humuita makengeza mara DJ hivyo kutokuwa Msukuma hakujawa kinga, wengine wanamuita Lissu kilema japo ulemavu umesababishwa na utawala wa awamu ya Magu.
Makabila yanayoongoza kupigwa vita/kushambuliwa kwa maneno ni Wachaga na Wahaya, hayo makabila wapambane sana kwani nchi nzima(Wasukuma included) wanayahofia yasishike nafasi za juu za uongozi.
Pamoja na arguments zangu mimi ni muumini wa freedom of speech, watu waseme chochote pasina kutukana, kushawishi jamii fulani ishambuliwe/ifanyiwe fujo yaani kusiwepo na uchochezi wa uvunjifu wa amani au uvunjivu wa sheria.
Wasukuma pamoja na wingi wao ushawishi wao ni mdogo ukiwalinganisha na Wachaga, Wahaya na Wanyakyusa ambao kila nyanja wapo katika nafasi za juu mpaka wanapigiwa kelele.
 
Nyerere aliona mbali sana makabila makubwa ni sumu kwenye uongozi wa Nchi,Wasukuma,Wachaga,Wanyakusya na Wahaya maana watajazana kwenye nafasi zote.

Kikwete alifanya vibaya sana kwenda against mtazamo wa Nyerere na matokeo yake ndio hayo tuliyoyapata.
Haya ni mawazo ya kizamani na enzi zile Nyerere alikuwa anajenga nchi,kusema mtu aliyetoka kabila kubwa hafai kuwa Rais nikwasababu hatuna taasisi imara na mifumo inayoeleweka.Yaani Katiba iwe strong,mtu alete upuuzi?
 
Wanabodi,

Kama kawaida yangu kila nipatapo fursa, huja na makala hizi za "Kwa Maslahi ya Taifa" ambazo hizileta kwa mfumo wa swali fikirishi na mimi kutoa tuu maoni yangu lakini kukupa wewe msomaji fursa ya kufikiri, kushauri na kutoa majibu unayoona yanafaa.

Swali la leo ni kuhusu kuibuka na kuchopuka kwa viji sentiments vya viashiria vya ubaguzi wa udini, ukanda na ukabila, sasa jee ni tuunganishe nguvu kukemea au roache tuu ukiisha ota na kukomaa ndipo tuukate?. Ubaguzi Ubaguzi huu wa kisasa unafanywa kwa viji neno neno vya kibaguzi, je neno Sukuma Gang, sio neno la kibaguzi?. ni neno tuu la kawaida tuliache au ni neno la kibaguzi linalostahili kukemewa?. Je mnaonaje kama Watanzania tukiungana kukemea vijineno neno vyenye viashiria vya Ubaguzi wa aina yowote kwa jina lolote?

Nimeileta hoja hii kufuatia as days goes by, hizi issues za hii kitu inayoitwa Sukuma Gang is escalating to the point of unbecoming!. Sukuma gang ni itikadi siyo kabila

The Mkuu Sexless , kwanza nikupongeze kuileta hoja hii, pili japo ni kweli neno Sukuma Gang ni itikadi tuu, lakini si kweli kuwa iliasisiwa na Magufuli!. Tumwacheni Magufuli apumzike kwa amani!. Voices From Within: Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani

Neno Sukuma Gang ni a fictitious Group that doesn't exist in reality lililobiniwa na yule Kigogo wa Twitter na watu wajinga wajinga wenye akili fupi wakaamini hili kundi ni kweli lipo!. Kiukweli kabisa Sukuma Gang sio kundi la kweli, halipo popote and don't exist anywhere in reality except ndani ya vichwa vya watu waliofilisika kisiasa!

Pia sii kweli! bali baada ya Kigogo wa Twitter kuliasisi kundi hili fictitious, akatumia nguvu kubwa kulifanyia indoctrination kuwa hili kundi does real exist, hivyo wale watu wa Magufuli na watu wote wanaomsupport Magufuli wakawa pointed kuwa ni members wa Sukuma Gang, hata mimi ni Msukuma, na namsupport Magufuli na sio Sukuma Gang!

Hakuna kitu kama hiki, ila kwa vile indoctrination ya existence ya uwepo wa kundi hili imefanyika na watu wenye akili fupi waliofilisika kisiasa wakaamini', kama na wewe unaamini kuwa kundi la Sukuma Gang kweli lipo and does exist in reality, ujijue ni akili fupi and muflis kisiasa kama wale muflis wengine wote wanaoamini ujinga huu!

Hapa nakuunga mkono!

Kumchukia mtu yoyote kwasababu yoyote sio jambo jema! Dini zinatufunza hata adui mpende!. Hivyo it's not right kumchukia mtu yoyote!

Japo hii shana ya the existence of the Sukuma Gang ni dhana tuu, na the Sukuma Gang ni just a fictitious Group that doesn't exist in reality, lakini kufuatia indoctrination iliyofanywa na yule Kigogo wa Twitter, watu wenye akili ndogo, akili fupi na waliofilisika ki fikra, wakaamini, hivyo chuki dhidi ya Wasukuma is real!. Hili sio jambo jema!.

Kufuatia kabila la Wasukuma kuwa ndilo kabila kubwa Tanzania kuliko makabila yote, zikitokea nafasi zozote za uongozi, na watu wote wako huru kugombea, obviously Wasukuma pia lazima watakuwepo.

Kulitokea nafasi fulani za uongozi ndani chama fulani, wakajitokeza wagombea 186 kugombea nafasi 8 aa uongozi. Miongoni mwa waliojitokeza walikuwepo Wasukuma wengi tuu ila mimi nawajua kulikuwa na Wasukuma wawili ambao kama wangepitishwa wangetupatia wawakilishi wazuri the best of the best.

Ikasemekana kuwa mmoja kati ya hao Wasukuma wawili ni member wa the Sukuma Gang!. Then kwenye mchujo ikaelezwa kuwa wamepewa maelekezo hatua ya kwanza kabisa ni kuwakata Wasukuma wote waliojitokeza!. Na kweli Wasukuma woote tukakatwa eti ni Sukuma Gang! This is not fair at all! Taifa linakosa uwakilishi wa watu wazuri kwa ubaguzi wa kijinga kabisa!

Na katika hili naomba na mimi nijiunge kwenye kukemea hii sumu ya ubaguzi mbaya kabisa ya kuwabagua Wasukuma kwa kisingizio cha Sukuma Gang, na naomba kutamka kama kuna Msukuma yoyote popote ameadhibiwa au kubaguliwa kwa kisingizio ni member wa the Sukuma Gang, then dhambi hiyo ya ubaguzi, itawatafuna wabaguzi hao kupitia kitu kinachoitwa karma! Karma haina mswalie Mtume wala haijali nani ni nani!

Paskali

Umeandika kwa jazba sana na kujaza nadharia zako.
 
Wasukuma 95% ni washamba uwe umesoma au hujasoma, by the way mmeturudisha nyuma sana kama Nchi.
Washamba kivipi kwanza?
Kuna makabila mengi yaliyo na ushamba kuliko hata wa wasukuma.
Ebu imagine mtu unakula mbwa, panya funza wale wkubwa wanaopatikana kwenye magogo ya miti iliyooza,
Makabila yanayokula vitu hivi yapo mengi huko mikoa ya kati na kusini ya Tanzania ila sisi wasukuma hatulagi au huwa hatuli madudu yenu hayo.
Sasa mpaka hapo mshamba ni nani.
Mnaowashambulia wasukuma kwamba ni washamba ebu jitokezeni na nyinyi mjitaje makabila yenu tuwajue, la sivuo nyinyi ndo wala panya , mbwa , funza nk.
 
Wapi
Kwa sababu huna akili hebu kwanza tupe uthibitisho kuwa asilimia kubwa ya mashoga Tanzania ni wapemba?

Pili hii yako siyo ubaguzi ila inakukera tu sukumagang? Sukumagang ni kundi wanufaika wa matendo ya dikteta Magufuli aliyeamua kuwajaza wasukuma wenzake kwenye nafasi za uongozi serikalini.

Mwisho kwa matendo ya Magufuli na kundi lake maarufu sukumagang bila shaka ni watu wabaya. Hakuna walioumizwa na utawala wake na wateule wake kama akina Sabaya?
Wapi nimesema asilimia kubwa ya mashoga Tanzania ni wapemba? Mimi nasema nyie wapemba mnalawitiana toka udogoni huko na mnachificha kesi hizo kwa kuogopa aibu mnaishia kuzimaliza nyumbani mwisho wa siku mnatengeneza mashoga na mnajulikana wapemba kwa kupenda michezo ya kuingiliana kinyume cha maumbile kwa kifupi wazanzibari ni washenzi na ni wabaguzi.
 
Back
Top Bottom