Naungana na mleta mada.
Binafsi sijawahi kulitumue hilo neno iwe positively au negatively. Watumiaji wa neno hili wanasema haliashirii kabila bali itikadi. Lakini hata kama linaashiria itikadi, uwepo wa neno linalotaja kabila, tayari umeleta hisia za ukabila.
Makosa au wema wa mtu usihusishwe na kabila la mtu, labda kama tendo lililofanywa na mhusika ni sehemu ya mila, tamaduni na desturi za kabila lake. Kama mtu hafai, basi atajwe yeye kwa sifa zake mbaya kuwa hafai.
Siku za huko nyuma, nilipokuwa nafanya masomo yangu ya shahada ya kwanza pale UD, kulikuwa na kawaida watu wa mkoa fulani au wilaya fulani kuwa na aina fulani ya umoja. Baadaye wengine walienda mbali zaidi na kufanya umoja huo kuashiria ukabila. Mathalani, tunajua wakazi wengi wa wilaya ya Kibosho ni wakibosho, Mwanga ni wapare, Bariadi ni wasukuma wanaojiita wanyantuzu, sasa wakatokea baadhi ya wanachuo, kwa mfano badala ya kuwa na umoja wa watu watokao Kibosho, wakataka kuwepo umoja wa wakibosho, au badala ya umoja wa wanachuo watokao Bariadi, wangetaka uwepo umoja wa wanyantuzu, n.k. Chuo kilipiga marufuku. Kwa sababu moja tu kwamba hata kama wakazi wengi wa Kibosho ni wakibosho, ni ubaguzi kuwa na umoja wa Wakibosho kwa sababu itaashiria kwamba kama kuna wanyamwezi wanaoishi Kibosho hawatakuwa na sifa ya kuwemo kwenye umoja huo, sawa na kama ukiwa unatoka Bariadi lakini wewe siyo mnyantuzu, utakuwa huna sifa ya kuwepo kwenye umoja wa wanyantuzu.
Tujiepushena fikra zinazoibua hisia za ubaguzi wa kilabila. Makabila yetu yabakie kwenye utani wetu wa asili lakini siyo kututenga kwa lolote.
Kama mtu ana viashiria vya ubaguzi wa aina yoyote hafai kuwa kiongozi.