Je tumefikishwa hapa na dhambi ya Ubaguzi ya JK Nyerere?

Je tumefikishwa hapa na dhambi ya Ubaguzi ya JK Nyerere?

Kilichotufikisha hapa ni nongwa ya wakatoliki kwa Bandari ya Dar. Mengine yote chenga tu. Huyo mama hana Shida yoyote. Amefanya kila kitu kwa bidii kubwa sana katika kuijenga nchi yenu. Ila eleweni, mnaenda kuitengeneza Congo nyingine kwa tamaa zenu.

..Mama angetekeleza 4R tusingeishia kwenye mauaji na machafuko.
 
Kilichotufikisha hapa ni nongwa ya wakatoliki kwa Bandari ya Dar.
Kobazi? Wakatoliki ndiyo wanateka na kuua watu? Wakatoliki ndiyo wanafanya maisha yawe magumu kwa Watanzania walio wengi huku mafisadi wakila kwa urefu wa kamba zao kama wapo peponi? Wakatoliki ndiyo wanatangaza Matokeo feki na kumwapisha rais feki? Una hata fununu ni kwa nini vijana wanaandamana?🚮🚮🚮
Huyo mama hana Shida yoyote.
Hata sheikh majini atakupinga huko aliko - hata kama anafaidi mabikra 72 kando ya mito ya pombe isiyokauka!
Amefanya kila kitu kwa bidii kubwa sana katika kuijenga nchi yenu.
Nchi yenu unamaanisha Zanzibar? 🤔
 
Kuendelea kumlalamikia Nyerere mtu aliyetoka madarakani over 30yrs ago ni upumbavu wa hali ya juu. Nyie hamna akili ya kujiendesha miaka yote hiyo hadi kumlaumu Nyerere tu? Hii ni sawa na mtu kumlaumu babu yake for his shortcomings. Ni ufinyu wa akili.
Wapumbavu sana hawa wafuasi wa Nyoka mwenye sumu wa Msoga
 
Takataka kama hizi watu huwa mnapata wapi muda wa kuziandika na kuzileta hapa?

Andiko reeefu ambalo hata halieleweki unaeleza jambo lipi hasa.

Hicho kichwa cha mada kinahusiana vipi na maneno meengi uliyojaza kwenye andiko?

Mwelekeo ni ule ule wa kuweka maslahi ya imani juu ya utaifa wetu!

Kikwete atakuwa ameshinda kitu gani badala ya kuingia kwenye kumbukumbu ya hovyo kabisa kwenye historia ya nchi hii?

Hovyo Kabisa.
Mkuu nimemsoma jamaa lakini sielewi lengo lake hasa ni nini. Kuwa kundi la mtandano ni kundi zuri na lina nia nzuri ila lilichokozwa na Nyerere? Kuwa Kkwete alipochukuwa fomu kwa mara ya kwanza angeachiwa basi tungekuwa na hali nzuri? Hai-make sense yoyote kwa alichoandika.
 
Takataka kama hizi watu huwa mnapata wapi muda wa kuziandika na kuzileta hapa?

Andiko reeefu ambalo hata halieleweki unaeleza jambo lipi hasa.

Hicho kichwa cha mada kinahusiana vipi na maneno meengi uliyojaza kwenye andiko?

Mwelekeo ni ule ule wa kuweka maslahi ya imani juu ya utaifa wetu!

Kikwete atakuwa ameshinda kitu gani badala ya kuingia kwenye kumbukumbu ya hovyo kabisa kwenye historia ya nchi hii?

Hovyo Kabisa.
Hivi ni kwanini watu tunapokutana na maoni yalio kinyume na mitazamo yetu tunatukana namna hii?
Haudhani hata maoni yako wewe kuna mwingine anaona takataka ila Ile freedom ya kila mtu kutoa hoja yake na maoni yake mtu hustahimili hata kama hoja ipo kinyume na mitazamo wake.

Mtu anachukua muda wake kutafakari, anachukua muda wake kuandika na kupangilia kwa mtiririko ulio rahisi kusomeka bado pia anatumia gharama za data kisha mtu anakuja kusema no takataka!
 
Nijenge msingi kwanza! Rais Obama aliwahi kusema Africa inahitaji Strong institution tu kujikomboa. Kwa maneno mengine Taasis imara hususan za Dola.

Nije kwenye mada. Ukiwasikiliza Wahenga na simulizi zao na hata ndugu Polepole miezi ya karibuni utagundua kuwa katika uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995 ndani ya CCM baada tu ya mfumo wa vyama vingi kurejeshwa aliibuka mgombea mwenye nguvu ndani ya Chama aliyeitwa Bwana Jakaya Kikwete. Huyu alipambana na Bwana Benjamin Mkapa (Chaguo la Nyerere) kwa karibu kabisa.

Kutokana na kukosekana kwa Taasis Imara labda ilibidi Nyerere atumie ukubwa wake kumzima Kikwete. Nafikiri hapa ndipo kosa lilipofanyika. Nyerere alipaswa kuwaacha vijana wachuane na atakayeshinda ashinde wakadhibitiwe na Taasis imara huko mbele ya safari.

Kitendo Cha Nyerere kuingilia mchakato na kuchagua upande huku yeye akiwa Baba Taifa kiliacha chuki na uhasama wa kisiasa kati ya watoto wake wawili Kikwete na Mkapa (Huo ni ubinadamu kisaikolojia).

Ukiendelea na simulizi hizo za wahenga utagundua kuwa Kikwete hata kama alichukizwa aliamua kufuata mifumo ya kidemokrasia na kisiasa kuendelea mapambano yake. Ndipo likaibuka neno mtandao. Rostam Aziz alitetea vizuri dhana ya mtandao. Ni kama vile MAGA ya Sasa ya Rais Donald Trump.

Mtandao ulimwezesha Kikwete kushinda uchaguzi uliofuata baada ya Mkapa kumaliza awamu yake ya pili na Kikwete akawa Rais.

Kikwete alianza kuharibu kwa lengo la kujilinda kwa kuwaingiza wanamtandao na siasa zao kwenye Taasis za Dola. Kukaanza mambo ya unanijua Mimi nani!?
Kikwete akaweka mapandikizi hadi kwenye vyama vya upinzani hivyo siasa yetu ikaingia unafiki, Hila, gilba, na Sanaa. Ikawa kila chombo cha wapinzani wa Kikwete Cha wapinzani wake kupumulia kikawa na mamluki wanaolipwa pesa kwa mlango wa nyuma kuwa snitch wapinzani wa Kikwete.

Mambo ya nchi yakaanza kupelekwa kwa kujuana na nchi ikaanza kutoka kwenye kufanya kazi kimfumo na ki haki. Vikaanzishwa vyuo mpaka vya online. Kama unatakiwa unaambiwa katafute cheti tu ulete hata kama hukukaa darasani tutakupigania utachukua nafasi nzuri. PhD uchwara na degree uchwara zikaibuka nyingi na watu wakalamba vyeo.

Alipokuja Magufuli ambaye ni timu Mkapa/Nyerere na ambaye kisiasa na kwa kufuata mifumo kama kungekuwa na kura za wanachama au kampeni za primary Magufuli asingetoboa dhidi ya Lowassa, hili likatonesha majeraha ya zamani.

Wanamtandao wakawa optimistic na positive kuwa muda wa siasa za kujipanga umefika. Wakaanza harakati za mapema, lakini Magufuli ama kwa mawazo yake au kwa kushauriwa na Mkapa au yoyote akaanza kutumia nguvu na amri zake binafsi badala ya mifumo, Taasis na Sheria. Wanamtandao walipotaka kuutumia upinzani wa Tanzania kusukuma ajenda zao Magufuli akaushughulia upinzani. Badala ya siasa kuendeshwa kama vilabu vya mpira ikaanza kuendeshwa kama Dini au kiapo. Ikafika hatua hata kumtembelea mgonjwa wa chama kingine mtu anaogopa.

Utawala wa Magufuli ukambananga Kikwete huku Mkapa akishuhudia. Matokeo yake kibinadamu JK akaweka kisasi na kuanza harakati zake za kuwa KINYAGO NILICHOKICHONGA mwenyewe hakiwezi kunitisha. JK akawa akipata nafasi ya kuongea anarusha makombora.

Binafsi naamini tofauti za kisiasa na kirafiki kati ya Kikwete na Mkapa ziliongezeka sana kipindi cha Magufuli. Alipokufa Mkapa basi Magufuli alibaki bila mtu mwenye nguvu juu yake kama Mkapa alivyobaki bila Nyerere kwenye uongozi wake.

Kilichofuata hadi kufikia mwaka 2020 Magufuli akabakia mwenyewe ila akafunga mianya yoyote ya kisiasa ya kumng'oa au kumpinga. Wapinzani wake ndani ya CCM akawafukuza uanachama na vijana wake wakamkweza mno huku nae akimshambulia Kikwete ambaye alikuwa ni senior kwake na mwenye kujua siasa kuliko yeye maana alianza mapambano tangu na Nyerere wakati Magufuli akiwa mwalimu huko.

Katika harakati za Kikwete na timu yake kujipanga ndipo likaibuka neno WATOTO WA MJINI. Hawa wanajua kila mtu ni wazoefu wa mtaa na Dunia. Wanajua uchawi, uongo, gilba, Hila, wema, subira, fitina n.k wapo fit idara zote. Unavyotaka wewe na wao wanataka hivyo hivyo.

Alipofariki Magufuli wakati watu wanafikiria namna ya kupindua meza Makamu akatangaza msiba juu kwa juu.

Baada Samia kushika madaraka lile kundi la Nyerere na Mkapa na baadae Magufuli likaanza kulilia uhuru wa siasa ambao liliwanyima Wanamtandao. Wanamtandao nao wakaamua kuacha mifumo ya siasa na Sheria na kuamua kuwaendesha waliojiita Wazalendo kibabe kibabe kama na wao walivyokuwa wanawafanyia.

Walitekwa nao wakawateka, waliuliwa nao wakaamua kuwaua. Walizuiwa kuandamana nao wakawazuia, walicheza na Taasis na Sheria ili kukandamiza nao wakafanyiwa hivyo hivyo.

Mwisho wa picha Wazalendo pumzi ikawaishia wakaamua kutengeneza chaos. Siasa lazimishi matokeo yake ndio hayaaa wamekufa na waliokuwamo na wasiokuwamo.

Nafikiri haya yametokea kama namna ya Mungu kuwakumbusha wagombanao na washindanao wapatane maana wamekuja kufa wajukuu kisa ugomvi wa akina babu.

Kikwete umeshinda na wewe ndio Babu uliyebakia. Waachie wajukuu nchi yenye amani na upendo usifuate nyayo za JK mwenzako Nyerere kuachia watoto ugomvi.

Turudishe Taasis imara. Kutunishiana misuli hadi Balozi tumempoteza pamoja na wanasiasa wengi chipukizi wa upinzani
Kwamba uhasama ulitokea kati ya Jakaya na Mkapa... ni hisia zako tu.

Nyerere hahusiki na kadhia za sasa. Labda alaumiwe kwa katiba ya 1977.

Msihamishe magoli
 
Kobazi? Wakatoliki ndiyo wanateka na kuua watu? Wakatoliki ndiyo wanafanya maisha yawe magumu kwa Watanzania walio wengi huku mafisadi wakila kwa urefu wa kamba zao kama wapo peponi? Wakatoliki ndiyo wanatangaza Matokeo feki na kumwapisha rais feki? Una hata fununu ni kwa nini vijana wanaandamana?🚮🚮🚮

Hata sheikh majini atakupinga huko aliko - hata kama anafaidi mabikra 72 kando ya mito ya pombe isiyokauka!

Nchi yenu unamaanisha Zanzibar? 🤔
Wewe mbona hujatekwa? Unatarajia kusanyiko la wapiga nyeto litakuwa na akili za maana sana?
 
Kwa mujibu wa mtoa mada ni kwamba Nyerere alimzima Kikwete kibabe kwa kumpitisha Mkapa. Na kwamba angeacha uwanja Sawa wa mchuano ili wa kushinda kwa HAKI ashinde. Huu ndio ubaguzi ambao mtoa mada ameuzungumzia. Ruksa kunirekebisha kama nimeelewa tofauti
Hapana, sitakurekebisha. Andiko hilo sikulisoma lote, kwa hiyo hiyo sehemu unayoizungumzia wewe sikuifikia baada ya kuona kichwa cha mada na yale ya mwanzo niliyosoma haviendani.

Nakushukuru kwa kunifafanulia hilo. ingawa hata hili bado sioni uhalali wa matumizi ya maneno "dhambi ya ubaguzi ya Nyerere"Kwa nini iwe ni "ubaguzi" kumkataa Kikwete na kumkubali Mkapa; msingi wake ni upi? ukilifuatilia hili unarudi kule kule kwenye hayo niliyo mambo niliyo yaelezea juu ya chuo kikuu cha kariakoo; siyo zaidi ya hapo!

Kikwete alinyimwa HAKI au hakuwa na hoja za kuonyesha kuwa HAKI yake imeporwa? Nyerere alimlazimisha nani kwa mabavu ili Kikwete asipate haki yake!
 
  • Sick
Reactions: Tui
Mkuu nimemsoma jamaa lakini sielewi lengo lake hasa ni nini. Kuwa kundi la mtandano ni kundi zuri na lina nia nzuri ila lilichokozwa na Nyerere? Kuwa Kkwete alipochukuwa fomu kwa mara ya kwanza angeachiwa basi tungekuwa na hali nzuri? Hai-make sense yoyote kwa alichoandika.
Sikulisoma andiko lake lote baada ya kuona sipati habari yoyote inayoendana na kichwa cha mada yake.

Kwa ufafanuzi wako huu, ina maana haya ya Samia ni mwendelezo wa yale mazuri aliyofanya Kikwete!
Mawazo haya ni sehemu ya kundi zima la AMANI likijumuishwa na BAKWATA, na kumhusisha Nyerere ni hoja zile zile zinazotoka chuo kikuu cha Kariako, kwa mzee Mohamed Said.

Inajulikana wazi kuwa Kikkwete kawatuza hao wazee wa kariakoo na kwa sasa ndiye kiongozi wa kundi hilo.
 
Back
Top Bottom