Je, tunao wataalam (Pharmacists) wa kutengeneza dawa hapa nchini Tanzania ?

komasalonde

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2024
Posts
2,742
Reaction score
3,523
Sekta ya afya ni moja ya eneo nyeti linalogharimu pesa nyingi za serikali inaponunua madawa toka nchi za nje kwa pesa za kigeni.

Wakati huo huo,. serikali inasomesha maelfu ya wafamasia ngazi za stashada (diploma) shahada (degree) masters mpaka PHD.

Najiuliza tu, ya kwamba katika maelfu ya wataalam hao wa madawa, hajawahi kutokea mgunduzi yeyote wa dawa iliyothibitishwa kuponya ?

Ni vikwazo vya wazungu wenye viwanda, au ni viongozi na watawala wetu kutokuwa na maono ? India, China, Uturuki wameweza kuwa na viwanda vyao. Je sisi hatuwezi ?
 
Tatizo lako hujui ya nchi yako

Mbona dawa kibao zibatengenezwa na watanzania pharmacist

Kama vile mansoor daya,Shellys nk uliza hata duka lolote la madawa watakwambia ziko kibao
 
Tatizo lako hujui ya nchi yako

Mbona dawa kibao zibatengenezwa na watanzania pharmacist

Kama vile nansoor daya,Shellys nk uliza gata duka lolote la madawa watakwambia ziko kibao
Kwa hiyo madawa hatuagizi tena nje kwa vile yanatengenezwa hapa ? Naomba kuelimishwa tu mkuu.
 
Kwanza lazima upate haki ya kuzalisha dawa kutoka kwa wamiliki, wakupe formula yao ,chemicals wanazochanganya kutengeneza hiyo dawa, vinginevyo ugundue dawa yako ndio utengeneze.
 
Hao wataalamu sasa hivi wanafikiria waende VETA wakafundishwe jinsi ya kutengeneza sabuni za magadi🐒
 
Mengi hatuagizi kwa asilimia kubwa sio yote hakuna nchi duniani ambayo asilimia 100 inajitegemea madawa lazima mengine iagize nje
Ikiwa hatuogopi tishio la viwanda vikubwa toka nje (kama lipo) na kama kweli tunao wasomi , wabobezi katika fani hiyo ya madawa, kwa nini serikali isiwekeze, nguvu, mtaji, na msaada wowote unaohitajika ili eneo hili, kwanza liokoe pesa za kigeni, pili litoe ajira, na utaalam kwa kuanzisha viwanda vya dawa za hospitalini ? Magonjwa kama ukimwi, cancer, kisukari, nk hayawezi kufanyiwa utafiti na dawa zikagunduliwa ?
 
Kwanza lazima upate haki ya kuzalisha dawa kutoka kwa wamiliki, wakupe formula yao ,chemicals wanazochanganya kutengeneza hiyo dawa, vinginevyo ugundue dawa yako ndio utengeneze.
Hoja yangu, hapajawahi kuwepo ugunduzi wowote thabiti ulioweza kuzalisha dawa ?
 
Hatujawahi kugundua dawa yoyote nadhani Africa nzima hakuna nchi iliyogundua dawa ikaingia kwenye soko la dunia.Nchi nyingi zina viwanda tu vya kuzalisha lakini wao sio wamiliki wa hivyo viwanda. Kama ilivyo dawa ya paracetamol inazalishwa nchi nyingi kwa majina tofaut(brands) kama HEDEX,Panadol na mengine la kini wenye haki miliki ni ni ha paracetamol
 
Ikiwa hatuogopi tishio la viwanda vikubwa toka nje (kama lipo) na kama kweli tunao wasomi , wabobezi katika fani hiyo ya madawa, kwa nini serikali isiwekeze, nguvu, mtaji, na msaada wowote unaohitajika ili eneo hili, kwanza liokoe pesa za kigeni, pili litoe ajira, na utaalam kwa kuanzisha viwanda vya dawa za hospitalini ? Magonjwa kama ukimwi, cancer, kisukari, nk hayawezi kufanyiwa utafiti na dawa zikagunduliwa ?
Viwanda vyote duniani vya dawa ni vya private sector ukiona fursa wekeza

Ukisubiri serikali utakesha

Tanzania sasa hivi tuna hospitali kibao za watu binafsi madaktari kubwa mno mfano hospitali ya Dr.Kairuki Dar es salaam yenye hadi chuo kikuu cha kuandaa madaktari ,wafamasia nk ada kubwa kuliko hata kusoma Muhimbili lakini hakupewa hata shilingi moja na serikali kuanzisha hiyo hospitali

Uko gizani wewe Ukiona fursa tafuta mtaji mwenyewe au tafuta mbia ndani ya nchi au nje mfanyie kazi wazo lenu liwe la kibiashara
 
Back
Top Bottom