Je, tunaweza kujenga Tanzania ya viwanda bila kutegemea mabeberu? Ukaribu beberu na 'next door' ni fimbo au biashara tu?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Wanabodi, Ijumaa ya leo nimepata fursa ya kuendelea na zile makala zangu za kwa Maslahi ya Taifa, leo nikiulizia kuhusu msimamo wa rais Magufuli kutosafiri nje hata kwa zile safari zenye maslahi makubwa kwa taifa, jee msimamo huo una Maslahi kwa Taifa?

Bandiko hili ni la swali moja kuu, kuwa Tanzania tumedhamiria kujenga Tanzania ya Viwanda, Jee tunaweza kuijenga hiyo Tanzania ya Viwanda bila kutegemea mitaji ya FDI kutoka nchi za nje zikiwemo nchi za Mabeberu?. Namna mzuri ya kuhamasisha FDI ni kupitia kwenye ziara za nje za rais, tuliona kwa JK, tukaona kwa Kagame na sasa tunaona kwa Uhuru, jee rais wetu Magufuli aendelee tuu kujifungia ndani tukitumai hizi FDI zitatufuata zenyewe?

Msimamo wa Rais wetu Dr. John Pombe Joseph Magufuli , JPM, wa kutosafiri nje una maslahi kwa taifa kwenye hili, hivyo kama tunategemea FDI kutoka nje, lazima rais Magufuli akubali kutoka awafuate ili kuvutia FDI zao au azidi kushikilia msimamo, tukomae nao, kwa hoja ya mgonjwa ndio hufuata mganga, kama wana shida waje?.

Kwa wavivu wa kusoma makitu marefu, tuishie hapa, wengine tuendeleeni.
Tena nashauri, baada ya Uchaguzi Mkuu ujao, yule kijana "pendwa" asipogombea ubunge popote, rais amteue tuu awe Mbunge wa kuteuliwa amfanye deputy wa MFA, na ataandamana nae UNGA, halafu tupimane ubavu na kubwa la mabeberu, nani zaidi kati ya Hapa Kazi akiongozana na Dogo Janja na Pempei na Kubwa Jinga!.

Tena kwa sasa bara zima ka Africa tuko kwenye kukamilisha kusaini African Continental Free Trade Area (AfCFTA) Agreement, lakini sisikii Tanzania tunajipangaje. Hivyo Kenya akisaini FTA na Marekani, then njia ya bidhaa za Africa Mashariki kuingia Marekani ni kupitia Kenya.

Hitimisho, kwa vile nimesema mengi humu, naomba kumalizia na lile swali la msingi la hoja hii kwa Maslahi ya Taifa, kuhusu msimamo wa rais Magufuli kutosafiri nje hata kwa zile safari zenye maslahi makubwa kwa taifa, jee msimamo huo una Maslahi kwa Taifa?.

Kwa kuwa Tanzania tumedhamiria kujenga Tanzania ya Viwanda, Jee tunaweza kuijenga hiyo Tanzania ya Viwanda bila kutegemea mitaji ya FDI kutoka nchi za nje zikiwemo nchi za Mabeberu, kuna umuhimu kwa rais wetu kusafiri nchi katika ziara za kimkakati ili kuvutia FDI?.

Kwa wale wa swala, Ijumaa Kareem
Kwa sisi wengine, Furahi Dei Njema

Paskali
 
Baada ya uchaguzi october atasafiri tu alikuwa kwenye kupanga mikakati na kuweka misingi imara kabla ya kuwashukia hao mabeberu!
 
Hiyo approach ya mtu mmoja awe raisi au whoever kwenda kuzurura nje kutafuta sijui mwekezaji naiona kama upuuzi tu.FDI ya kwenda kuwatafuta ni approach chovu na yenye impact ndogo mno

Tunatakiwa turuhusu watanzania kununua hisa kwenye masoko makubwa ya hisa Duniani yaliyoko Ulaya, Marekani na Japan. Huko ndiko matajiri wa dunia huzalishwa kwenye hayo masoko

Pia Kuwezesha nchi kuwa na pesa nyingi za kigeni badala tu ya kutegemea mauzo ya mazao ya korosho sijui dengu na mazao mengine ya mashambani yanayotegemea Hali ya hewa

Kwenye hayo masoko ndiko kwenye mikampuni mikubwa Duniani inayoongoza kupata faida ambayo huuza hisa na kununua

Ina maana sisi wenyewe tunakuwa wamiliki wa hayo makampumi na faida tunayopata tunaileta ndani ya nchi

badala ya kuleta mitaji ya nje ndani ya nchi tunaleta faida ndani ya nchi na faida hiyo tunaitumia kujenga uchumi wetu wa ndani

ndicho nchi zilizoendelea zinafanya wanawekeza kwako faida ndio inaenda endeleza kule kwao.
Tulenge zaidi kwenye upataji faida sio mitaji
FDI unazurura kutafuta ntu wa kukuchomoa faida!!! ndio maana tunalia lia ohhh wawekezaji wanatunyonya wanachukua faida kubwa kupeleka kwao si na wewe ukawekeze kwao upate faida kwa kununua hisa kule kwao? kampuni ikipata faida kwenye shughuli zake duniani kote unapata gawio lako unakula nchini kwako

niseme wazi mimi hiyo FDI naiona upuuzi mtupu inachangia tu kufanya nchi zetu kuwa tu tegemezi na maskini

Tanzania tusiposhiriki na kuwa active kwenye uchumi wa dunia kwa kushiiriki kwenye hayo masoko ya hisa ya dunia umaskini kwisha utakuwa mgumu

tutalalamika ohhh migodi iko kibao ,wawekezaji wapo lakini mbona umasikini hauishi? FDI ya makampuni ya migodi ina gesi ipo lakini unashangaa watu bado wako choka mbaya

Si recommend utalii wa FDI kwa kisingizio cha kutafuta wawekezaji
 
Dunia ya leo tunategemeana sana. Japo sehemu kubwa ya mipango na maamuzi inatuhusu kama taifa.
Mfano kuwekeza katika ATCL ndege ndogo na za kati usafiri wa ndani na majirani,soko la nje yapo mashirika mengi yamejipanga,ni kufanya link pekee, pesa midege mikubwa tungewekeza kilimo na mifugo, multiplier effect yake usipime.Tutamlaumu beberu kwa maamuzi hayo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Safari za nje ya nchi zina umuhimu mkubwa sana katika kujenga uchumi wa viwanda na kukuza private sector na kuvutia mitaji, dunia ya sasa inahitaji ushirikiano, chukulia mfano wa China, kuna wawekezaje wangapi kutoka nje especially mataifa ya magharibi?

Sisi tuna economic diplomacy kwenye makaratasi sio Kichwani, ndio maana matatizo kibao vijana hawana ajira, sababu private sector haikuwi, serikali haina uwezo wa kuwekeza kwenye miradi inayoweza kutengeneza ajira nyingi. Wanasiasa wamebaki kusema vijana wajiajiri, kwa mitaji IPI? Kwa masoko yapi?

Africa tunafail sana sababu watu smart hawapati nafasi ya kutuongoza...wanaojua ushirikina na kujipendekeza ndio watunga Sera.

Lazima akili kubwa zipewe nafasi...watu wenye maono mapana na taifa. Watu wakikosoa kidogo ili Ku improve government's performance kwenye uchumi wanataka kutolewa roho!

Bahati mbaya sana kuzaliwa hili bara, no wonder karne hii watu weusi wanakufa kwenye bahari wakijaribu kukimbia mateso ya watawala walioshindwa kujenga uchumi!

Hawa viongozi hawaoni aibu karne hii watu wanakimbilia ulaya sababu wameshindwa kujenga uchumi? MTU anakwambia tuzaliane ili tukuze uchumi, siku niliposikia hiyo kauli nilitupa kwenye dustbin kabisa. Hatuna viongozi hapa.
 
MTU anakwambia tuzaliane ili tukuze uchumi, siku niliposikia hiyo kauli nilitupa kwenye dustbin kabisa. Hatuna viongozi hapa.
Hapa umechemka nchi zote zenye population kubwa zina matajiri wakubwa wengi

mfano mimi ninauza nguo za watoto.Wanavyozaliana kwa wingi ndivyo uchumi wangu unavyopaa kwa spidi ya mwewe.Kwa hili namuunga mkono raisi.Watu wazae sana uchumi wangu upae.Kwa hiki hotuba yake nimeitunza pazuri
 
Jibu ni rahisi "haiwezekani'' hata wewe unajua,Vipi Obama angezaliwa an kukulia Kibera si angekua anauza chang'aa na bibi yake mpaka leo. kila tunaposafiri tunajifunza na kukutana na vitu na watu mbali mbali, ni kama mtu alie kijijini au anaeishi shambani asitoke huko alipo vipi "mind set" yake itakuaje, maana yake potential yake iatakua chini sana, ndio maana kuna mambo mengi yanayofanyika TZ yanaonekana yamepitwa na wakati, lakini bado yanatiliwa mkazo kila siku yaendelee. kifupi tunatakiwa kuiga yale mazuri ya wengine na kuyakataa mabaya wala tusi feel threaten by other success. kama sivyo Ndio maana tuanafikiraia hata cherehani ni kiwanda.
 
Kagame unamuona jinsi anavyopambana. Kila sehemu huko dunia ya kwanza kukitokea fursa utamuona frontline hatumi waziri . Pamoja u dikteta wake lakini unaona anajitahidi kuacha kizuri kitu kwa ajili ya Taifa lake.

Kingine huyu ni kipenzi cha Mataifa ya Magharibi. Hata afanye nini nadra kusikia mabeberu wanaongea chochote. Sasa kama tunamuiga tuige mazuri yake sio tunaiga mabaya tu ya kutekana na kuuana. Sisi tumeiga mabaya sasa jumuiya za kimataifa zimeanza kutunyooshea vidole. Tukipotea kama Taifa hao wanaojiita marafiki majirani ndio fursa zaidi kwao kama ilivyo sasa.
 
Kuzaliana hakuleti uchumi. Issues ni quality ya watu mtaani.
 
nani kakudanganya? Suala ni income sio population, Finland INA watu wangapi? 5m! Unajua soko lao ni kubwa kuliko nchi zote za UAE? Suala ni kipato cha watu sio wingi wa watu, watu mil 5 wenye kipato, wanaolipa kodi ni bora kuliko watu mil 50 ambao 80% wanaishi chini ya dola moja na umasikini uliotopea. Watu wanaoishi chini ya dola moja wanakuwaje soko lako? Au ndio burden kwenye society? Si ndio hao wanaolilia elimu bure? Sababu they cannot afford kulipa ada ya elfu 20? Hao watu unataka waongezeke ili ujenge uchumi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…