Je, tunaweza kujenga Tanzania ya viwanda bila kutegemea mabeberu? Ukaribu beberu na 'next door' ni fimbo au biashara tu?

Nimesoma comment nyingi sana lakini nimefka sehemu nilitaka kusema Elimu ni kitu muhimu Sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uchumi wa nchi unajengwa na Duka la nguo na duka la chakula? Aiseee unaweza kuta wewe ni mwalimu unafundisha watoto wa watu. Aiseee

Sent using Jamii Forums mobile app
kuna macro economics ambao ni uchumi wa nchi na kuna micro economics uchumi wa mtu mmoja mmoja mmoja.Mimi naongelea wa mtu mmoja mmoja .Kwa mmoja mmoja yes .Bakheresa ni tajiri na bilionea kwa sababu ya kuuza vyakula anauzia population kubwa huo wa nchi baki nao mwenyewe.Mimi napambana na hali yangu watoto wakizaliwa wengi mimi ndio nauza sana nguo na uchumi wangu unakuwa juu

uchumi wa nchi nzima kwangu ni hopelesss mimi.najitizama kwa my micro level yangu binafsi umbeya wa nchi nzima baki nao wewe
 
Haiwezekani tunahitaji 'grobal levalage and investment' ambapo serikali ndiyo mdhamini mkuu
 
Ulikuwa upaswi kucomment chochote kwenye post hii.

Pia ni njema ungeazisha post yenye mada yako.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani rais alisema wewe peke yako ndo ufyatue watoto?
 
Pamoja na hoja yako ambayo unafikiri kwamba rais anaposafiri ndio analeta maendeleo na kukuza uchumi sio sahihi. Katika ulimwengu wa leo na technology ilivyokuwa hivi sasa sio lazima usafiri nje ndio unaweza kufanya yale ambayo yanaonekana kwa macho hivi sasa Tanzania.

Watanzania wengi ni wabinafsi hawaangalii benefits ambazo zinatokana na kuwa na Kiongozi kama JPM. Sio nyinyi mliombatiza JK jina la Vasco da Gama? Je, JK alifanikiwa vipi katika kuendeleza maendeleo ya Tanzania katika miaka 10 aliyokaa? Tulichokuwa tumeambulia ni baadhi ya wachache kujitajirisha, hata watoto wake nao walikuwa marais.

Mwacheni JPM aivushe Tanzania kwenye level nyingine ambayo nyinyi hamkuizoea. Hakuna kiongozi yeyote duniani ambaye hatamani kukutana na JPM, lakini hivi sasa ana kazi moja tu kuisafisha hii nchi ili kizazi kijacho kiondokane na umasikini uliokubuhu. We deserve better than what JK, BWM did for our Country. Those FDI in actual fact we do not need them, as we have everything to develop with our own abundant resources. Those few individuls who used to think Tanzania ni shamba la bibi watakiona cha mtema kuni.

Maendeleo hayaletwi na wewe kujaziwa noti mfukoni bila kuwa na elimu na uwezo wa kutatua matatizo yako wewe mwenyewe. Huu ujinga ambao Western Countries wamewaloga nao ni kama ukoma. Nchi ina kila aina ya utajiri kupiga hatua, tumuunge mkono JPM kwa hali na mali na kuachana na vibaraka wanaojitembeza na bakuli.
 
"Those FDI in actual fact we do not need them, as we have everything to develop with our natural resources"
Ni statement inayoonyesha uelewa wako mdogo sana wa global economy, pia maendeleo ya nchi mbali mbali duniani, nchi nyingi sana kwa mfano Canada, China, South Korea, Vietnam, Malaysia, Australia, etc zimeendelea kwa kuvutia wawekezaji and technology kutoka nje, harafu nani kakudanganya au uchumi wa wapi umesoma kwamba ukiwa na abundant resources then you have everything? Resources ambazo hauzibadili kuwa commodities or raw materials, or finished goods hazina maana wala thamani kwenye uchumi, resources zina maana pale tu unapozitumia kwa kuzitoa huko zilipo. Kwa mfano gas yako haina maana ikibaki huko ardhini, it will never transform your economy! Swali: do you have the technology? Capital? And necessary expertise kuitoa huko ilipo? Jibu hamna, hamna elimu sababu hata hao maprof tulionao vituko majukwaani, mtaji? Hauna, unaweza hata gundua hiyo gas IPO kwa kufanya exploration? Hamna!! Sasa unatamba nini? Ndio maana sasa linakuja suala la kuhitaji kuwekeza, tunahitaji technology transfer, tunahitaji expertise,

Na hauwezi pata vyote hivyo kwa Rais anaejifungia ndani bila Ku influence , bila kuwa na predictability kwenye investment policies, etc. Sio kila jambo ni kutetea tu, mada ya paskari IPO sahihi, Leo tunaenda mwaka wa 5 na mwaka wa uchaguzi Mh. Anaogopa kutoka nje ya bara hili. Kwa maslahi mapana ya taifa amwachie mtu mwingine.

Maendeleo unayoongelea ndio hayo yanayopaisha national debt, cz we are too poor kujenga hizo economic infrastructure ie SGR etc bila kukopa, kwa kodi zipi? Za kitambulisho cha wamachinga? Za ukwaju wa Azam? Ndio maana unaona tunashindwa kuajiri, tunashindwa kuchangamsha uchumi through money circulation sababu ya kutaka kuwekeza kwenye miradi ambayo hatuna uwezo nayo kiuchumi, kina JK na mapungufu yao hawakuwa wajinga kwenda kutafuta wawekezaji nje! Sio KILA JAMBO KUTETEA TU! Unaweza tumia ubongo wako kwa muda bila kuuwazima kwa wanasiasa.
 
Wachina hawakuweza kufanya uwekezaji kwa kutumia watu wao na natural resources zao za ndani licha ya kwamba wana natural resources za ndani nyingi maradufu kuizidi Tanzania. Ni Ulaya na America waliwekeza heavily ina China. Mpaka leo China inaongoza kwa kuvutia FDI toka Ulaya. Wachina mpaka leo, kila mara mkuu wao wa nchi yupo Ulaya kutafuta wawekezaji lakini Watanzania wanaoamini China imeendelea sana wanaona hakuna haja ya uwekezaji wa kimataifa!! Ama kweli watanzania wengi elimu yao ni ya kujua kuandika tu lakini siyo ya kutafakari na kuchambua.

Waustralia hawakuweza. Walihitaji uwekezaji mkubwa toka UK.

South Korea hawakuweza. Ni US iliwekeza heavily in South Korea. North Korea walioamini wanaweza kuwekeza wenyewe ndani kwa ndani, mpaka leo wanasumbuliwa na ukosefu wa mahitaji muhimu kama chakula!

Ni uwekezaji mkubwa Wa US ndio ulioibadili Mexico.

When you are in poverty cycle, you need an external force to break the loop.

Sasa hivi uwekezaji umeporomoka toka 28% ya 2015 mpaka 4%; ukuaji wa utalii umeporomika toka 15% mwaka 2015 mpaka 3.6%. Labda uwe na dosari fulani kichwani ndiyo utaamini kuwa eti kuna misingi ya uchumi inajengwa! Lakini siyo jambo la ajabu - wapo Wazimbabwe mpaka leo wanaamini kuwa Mugabe ameweka msingi mzuri wa Zimbabwe kujitegemea kuliko kuwategemea mabeberu.
 
Nimesoma kila comment mpaka mwisho namimi nimeamua kuandika..

Mijadala kama hii ni muhimu sana kwa maendeleo ya Taifa letu, tena ni muhimu ikafanyika kwenye vyuo vikuu na ihusishe watu mbalimbali wenye utalaamu tofauti tofauti ila tu wasiwe wanasiasa na hiyo mijadala isihusishe hizi siasa zetu za kipuuzi, kifupi watu wawe huru kutema madini na hoja mezani..
 
Taifa la Tanzania linapopulation ya zaidi ya watu 50milioni, idadi hii ya watu ni mtaji tosha kama itatumika vizuri kwa maana ya uzarishaji..Watu 50 milion hawawezi kuzarisha kama hujawaandaa na kutengeneza uelekeo. Kwenda kuwaleta wawekezaji halafu wanakuja wanakuta your 50milions population ni consumers and they are not productive bado ni hasara kwa Taifa. Muwekezaji anatakiwa aje akute tayari jamii yetu iko tayari with smart brains and skilled labor force.

Kama unawatu halafu haufanyi uwekezaji kwenye vichwa vyao basi Tambua utakuja kuwa na Taifa lenye watu wengi tegemezi, ukiwa na watoto ukashindwa kuwaandaa basi tambua huko mbele watakuja kuwa mizigo isiyo na msaada.. Ni vyema uwekezaji mkubwa ukafanyika kwenye vichwa vya watu na mifumo ikaruhusu sasa smart brains kuingia ndani ya mifumo na tukaachana kabisa na kutumia politics kama ground yakupata think tanks yetu..
 

Nafikiri pia ni vizuri huo uwekezaji ukaja ukakuta nasisi tayari tuna enough skilled work force with favourable ground for investments kama miundo mbinu, umeme wa kutosha and good social services..

Ninachokiona investors wengi walikimbilia China kwasababu ya low production cost iliyokuwa inapatikana China ambayo ilichagizwa na uwepo wa cheap workforce ambayo ni highly skilled, enough raw materials, good infrastructures and reliable power supply..

Binafsi naona tumewekeza sana siasa kwenye vichwa vya watu na si kuiandaa jamii kwa kufanya uwekezaji kwenye vichwa vya watu wetu kwa maana ya Elimu bora kwa watu wetu itakayozarisha high numbers of skilled work force ambayo pamoja na uwekezaji wa wageni inaweza pia kutusaidia nasisi kufanya ya kwetu kwa kutumia vitu kama reverse engineering na teknology copy..
 
I concur. Kunaweza kuwepo na mambo mengine ya kuzingatia lakini uliyoaandika dhahiri ni mambo muhimu.
 
Hatuwahitaji Mabeberu sisi,
Sisi tuko na Mchina,hata Kama Kuna Corona,au Kuna Angalizo LA WHO na Kututaja tumuache china,Hatumuachi Ng'oo,hizo ni mbinu za Mabeberu tuu,kututenganisha na Mchina,China ni Rafiki wa Kweli!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani China siyo beberu??

Kazi kubadili mabwana tu, wala hakuna asiye na ubeberu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watetezi wa chama hawa ni vichwa maji kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…