Je, tunaweza kujenga Tanzania ya viwanda bila kutegemea mabeberu? Ukaribu beberu na 'next door' ni fimbo au biashara tu?

Nimekwambia leta ushahidi wewe unazunguka mbuyu. Wacha porojo!
Chukua huu,kushuka kwa bei za frem kwa kukosa wapangaji,kufungwa kwa frem nyingi na maduka,kufa kwa mabenk,kupungua kwa makusanyo ya kodi,kupungua kwa watu sehemu za starehe eg mabaa,kupungua kwa sadaka,kwa uchache
 
Kenya mnailaumu tu bure

Historia yetu ndiyo inayotuangusha,.
Kuherere cha mwalimu ndiyo kinatufanya tuwe hivi,
Tuliweza sana kwenye azimio la arusha, tukaendesha nchi kwa mazao japo yalipilata changamoto hasa uuzaji wa nuts kule marekani, je, ni kwa nini tuliamua kujibebesha africa mabegani?
Tazama nchi tulizozisaidia kupata uhuru zimetufaidisha nini? Tukang'oa reli ya kusini, tukaacha kujenga barabara ya Kusini , tukaachana na Mtwara corridor kwa kigezo cha ukombozi wa kusini mwa afrika, rais anajenga nchi changa huku anapigana vita hata vita uganda ni kutokana akili mbovu za mwalimu na haiba binfsi.

Tuassume nchi hii tusungejiingaje huku kote leo tungekuwa wapi?
Mwalimu pia alikuwa na akili kidogo aliamini hatuwez kutoboa bila elimu kwa watu wetu ikiwezekana wote, alijenga viwanda huku anatusomesha lkn elimu ya chini kwa watu wachache angalau angejenga shule nyingi hata waliomfuta hawakujua kama elimu ni mtaji kidogo mkapa mwishoni akagundua.
Tulipo leo katika elimu ya kata wao walikuwa miaka 80-90 na Moi aliahakikisha wakenya wanasoma tena la nane lao lilikuwa bora kuliko la saba letu na mpaka leo elimu yao ni bora kuliko yetu
Tazama bharesa alianza na wakenya kibao wakati anaanzisha kiwanda na hapa tz course nyingi za viwandani hatuna ukizipata ni kuanzia degree nawakati kenya unaanza na cheti.

Tusiwalaumu kenya waliwekeza kwenye elimu na walikuwa wabunifu,
Wao ndio wa kwanza kuwa na kiwanda cha kuchakata minofu ya samaki, walivumbua uvuvi WA dagaa ziwa Victoria na soko LA kwanza LA dagaa ni Kenya badae sirari na arusha ambapo wanunuzi wengi wakiwa wakenya kote huko.

Ebu tuangalie viwanda vilivyopo Kenya miaka 20 iliyopita ndiyo tunayoangaika kuvianzisha leo Tz na ndio maana elimu ya kitaalamu ilipanuka mapema, uzalishaji WA maziwa Kenya, chai, nyama na matunda ni makubwa kuliko hapa, viwanda vidogo Kenya n vingi ambavyo mtaji ni ml 15-30-50 je tungekuwa na elimu nzuri tusingejua hili, wakati tunabinafsisha kuuma viwanda vikubwa wenzako uchumi WA viwanda wakawakabidhi wananchi na wageni waaminifu.

Nilishituka sana siku hiyo kumuona Kenyatta white house lkn Kenyatta katumia nafasi ya taarifa ya kamanda WA marekani Africa kwenye Congress na jinsi Kenya ilivyoamua kutumika na marekani lkn nao wameamua kuitumia sasa kwa faida.
Soon senate itatoa huo mkataba na utasainia ikiwa tayari Kenya ndio nchi inayouza vitu vya afrika mashariki nje kwa wingi, wakati mayala unataja nyanya tayari wamefika kwenye avocado na Magu anajua maana naye mwaka huu anaenda kuuza kwa wakenya tena wananunua mtini ukiwa mchanga.

Tujiulize tu mh alivyoenda Mara alitumia sh .ngapi tukijumuisha na perdiem zinazplipwa na mikoa, wilaya, halmashauri na mashirika utagundua n pesa inayotosha kumpeleka UN na kujadili mambo vema, lkn tukumbuke Kenyatta hotuba mwaka Jana UN alitoa siku ya kwanza na aliaddress mambo ya nchi yake kama leading country in Afrika.

Elimu
Elimu
Elimu itatuweka pazur

Nimesikia wanafanya review ya Sera ya elimu ya mwaka 2014 lkn hatujashirikishwa wadau WA nje ya taasisi kubwa

Napenda tupunguze madarasa ya msingi tena yabaki manne .

Viwanda na mabeberu kama watu wako hawana elimu ya viwanda kitaalamu n bure kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 


Kenya walikuwa koloni. Unaandika kama umetoka kunywa togwa. Katika zama hizi za uwazi na uchumi wetu unavyokwenda sina shaka yoyote na nchi kama Kenya. The price is higher than that.
 
Wako bize kuuwa upinzani kuliko kuwa bize kuuwa umasikini wakenya wako bize kuuwa umasikini
 
Umeangalia takwimu ya FID uingiaji wa makampuni mapya ya nje kwenye uwekezaji mpya,umeangalia export, umeangalia purchasing power?Umeangalia marejesho ya mikopo ktk mabenk ? Au unatoa porojo tu

Hilo swala nakuuliza wewe na umegota kutegemea Mabeberu, nchi inajengwa na wananchi haijengwi na mabwenyeye. Pesa tunazo sisi wenyewe kama hupendi nenda kajinyonge. Serikali hii inapokopa pesa kutoka nje unafikiri inacheza upatu. Enzi zenu za JK kula na kusaza bila kunawa zimepitwa na wakati.

Unaweza kupita hata hapa chini kujirizisha. Nchi yetu ipo pazuri kuliko jana.



Why Tanzania continues to borrow despite huge reserves
 
Kada huyo. Pole sana kwa taarifa yako tunaelekea Zimbabwe .muda utaongea
 
Miaka 60 hata kujenga vyoo tunategemea misaada, tumeshindwa tokomeza nyumba za nyasi watu wanaishi kama wanyapori kwenye nyasi.No country is self sufficient ili uendelee ni lazima uliwe.Kama unakopa na kuwekeza kwenye miradi ya kisiasa je
 
Moja Nchi 25 zilizopewa mkopo kuokoa uchumi usianguke Kutokana na Janga la Corona Tanzania imenyimwa.Pili nchi 27 zilizosamehewa Madeni Kutokana na Corona Tanzania haimo.Sasa mabeberu...
Duh...!. Mabeberu buana, hii Corona wanataka kuitumia kama fimbo ya kutuchapia!.
P
 
Tanzania imekuwa na ujinga wa miaka mitano mitano ya Maendeleo (Five years development plan) toka wakati wa Nyerere ambayo hadi leo imefeli vibaya. Magufuli na wenzake wamebaki kulalamikia mabeberu tu. Miaka yote tangu uhuru wa Tanganyika tumekuwa tukipewa misaada lakini badala ya kutumia kufanyia miradi ya maana imekuwa ikiendeshea serikali hizo za kidhalimu za Nyerere hadi huyo Magufuli ambaye ndiyo bomu kabisa. Leo anataka asamehewe mkopo kisa CORONA....Kwani hizo pesa zilitumika kwa ajili ya kutibu CORONA au kwa matumizi mengine.
Paskali, Magufuli na Musukuma mtalaamu sana mabeberu lakini tatizo lipo kwenye hao viongozi wabovu.
 
Duh...!. Mabeberu buana, hii Corona wanataka kuitumia kama fimbo ya kutuchapia!.
P

Mkuu the financial sector ya sasa hivi duniani inawapendelea mabeberu ie exchange rate mechanism waliyoiweka. FYI UK hivi sasa wanajikopesha £60 billion for the next three months kutokanana Covid-19. (Just look at that figure ….. ….. ……. without Covid-19 huwa wanaweka average ya 5-6 billion kila mwezi. Hii vita ni kubwa sana.
 
Nafikiri mkuu wa nchi,mzalendo namba moja alishatoa majibu. Masuala madogo madogo kama kutafuta wawekezaji ni ishu za kushughulikiwa na mabalozi wanaomuwakilisha. Yeya acha achape kazi hapa hapa nchini. Na kwa kufanya hivyo anaokoa pesa nyingi tu ambazo zingetumika kwa safari zisizo na ulazima sana sababu wanaomuwakilisha wapo huko na wanaweza kufanya kazi kwa niaba yake.
 
Hivi kwa nini sisi wa waafrika tusipambane na hili janga kwa umoja wetu? Eu inatoa stimulus package kwa member states. Kwa nini Au isikae na African development Bank na kutoa pesa za kuchochea uchumi? Au kila kitu mpaka kulaumu mabeberu. Au African development Bank hawana pesa?
 
Hivi ule mradi wa kuchimba helium gas umefikia wapi?
 

Mkuu financial sector ipo tofauti sana na jinsi unavyofikiri ……. ...….. UK wanachapisha hizo billion 60 kila mwezi then wanakwambia kila £ moja wanabadili kwa gharama ile ile kabla ya Covid-19 kutua. Au kwa maana nyingine wanachapisha hizo £ kwenye machine haiwa-cost kitu chochote kwa sababu wanatakiwa kununua dawa kutoka kwa mchina au popote pale wewe unakubali kwamba hiyo ndio thamani yake wakati ki-kweli thamani yake ilibidi ipungue. Ni kama wakati ule R G Mugabe alipoamua kuchapisha dola zake kule Zim na matokeo yake unayaona. Hawa jamaa wametukalia kooni sana wanajifanya wajuzi sana tuamke Afrika. £ thamani yake ishuke. Hata USA nao lazima wameanza kufanya haka kamchezo.
 
Mh...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…