Uchaguzi 2020 Je, Tundu Lissu ana nguvu gani dhidi ya wagombea wengine wa urais?

Uchaguzi 2020 Je, Tundu Lissu ana nguvu gani dhidi ya wagombea wengine wa urais?

Na hii ndio itakayompoteza mazima. Mtu akisikia tu jamaa katumwa na mabeberu basi kwisha kazi

Senti bai yuzingi tecno T301

Dunia hii nani anaamini hiyo propaganda ya kizee? Labda ww na wazee wenzako mlioishi kabla ya mwaka 90. Wapiga kura wengi ni wa miaka ya 90 kwenda mbele, ambao ni wapiga kura wa upinzani, hizo slogan za kizee hazina maana yoyote kwao. Hii ndio sababu ccm inatumia mabavu kukaa madarakani, maana haina mvuto wa kizazi hiki.
 
Kwani kuna ubaya gani akigombea mwaka huu na iwapo akashindwa agombee tena mwaka unaoutaka mkuu??

Ni kweli kabisa, kwanza unapoingia kwenye ushindani kuna kushinda na kushindwa, cha muhimu ni kushinda au kushindwa kihalali.
 
Uchambuzi mwanana, Ila ujue tu siasa sasa inaanza na TL anashida pia ya kuuhakikishia uma kwamba hajatumwa na Wazungu .. Hii ni propaganda ndogo lakini kwa aina ya mtanzania inamnyima kura.

Hii propaganda mfu ina nguvu kwa wanaccm, ambao bila hata hiyo propaganda hawawezi kumpa Lisu kura.
 
Dunia hii nani anaamini hiyo propaganda ya kizee? Labda ww na wazee wenzako mlioishi kabla ya mwaka 90. Wapiga kura wengi ni wa miaka ya 90 kwenda mbele, ambao ni wapiga kura wa upinzani, hizo slogan za kizee hazina maana yoyote kwao. Hii ndio sababu ccm inatumia mabavu kukaa madarakani, maana haina mvuto wa kizazi hiki.
Mkuu October nikaribu sana kuwa mpole

Senti bai yuzingi tecno T301
 
Sina tatizo na umbali au ukaribu wa mwezi Oktoba, ninajali uchaguzi wa haki tu.
Usije kimbia humu. Watanzania wa leo sio wajinga, wanajua nani Rais nani msindikozaji.

Senti bai yuzingi tecno T301
 
..kwanza, TL ana HISTORIA ya kutetea wananchi tangu akiwa kijana mdogo, tena akiwa hana ulinzi wala cheo.

..hiyo ni tofauti na wale wanaotetea wananchi baada ya kupata ulinzi, walipokuwa hawana ulinzi walikuwa upande wa madhalimu.

..pili, TL ktk macho ya jamii ni SHUJAA. tukio la kumshambulia limemuongezea imani, huruma, na mapenzi ya wananchi.

..tatu, ni msomi na ni miongoni mwa wanasiasa wachache wenye kipaji cha kujenga hoja. TL akianza kuongea siyo rahisi kumchosha msikilizaji wake kwani huwa hatabiriki.

..nne, ni muelewa wa mambo mengi sana ya kisheria, kiutawala, na kiuongozi. hili ni eneo ambalo amewazidi wanasiasa wengi. kama utagundua siku hizi wanasiasa wengi wamejificha kwenye dini na maandiko ya misahafu. TL ni tofauti kabisa.

..kwa maoni yangu, upinzani haujawahi kuwa na mgombea mwenye vigezo vingi vizuri, imara, na maarufu, kama Tundu Lissu.
Asee, unampamba lisu as ni mumeo! Anyway, 98% ya ulichoandika is rubbish. Ungeweka angalau matokeo ya study uliyofanya juu ya hayo uliyoweka hapo at least ungeeleweka. Kwa ushauri tu better not to generalise unapoamua kujenga hoja hasa iwapo huwezi ku-support hoja yako kwa facts. Kwa mfano how do you define "jamii"? Ni jamii ipi inayomuona lisu ni Shuja wake?
 
..dah!

..wewe inaelekea unahemkwa kwa CHUKI.

..TL angekuwa ni mtu wa hovyo tusingekuwa tunamzungumzia hapa.
 
Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kiliyapitisha majina matatu kati ya wachukua fomu takribani saba waliogombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho.

Kisha wajumbe wa Baraza Kuu walipigia kura majina hayo na jina la Tundu Antiphas Mughwai Lissu likaibuka na ushindi wa kishindo wa kura 405 kati ya 442.

Majina mengine mawili ni Lazaro Nyalandu aliyepata kura 36.

Mwanasiasa huyu kihistoria alikuwa Chama cha Mapinduzi (CCM), akiwa Mbunge wa Singida Kaskazini. Alihudumu katika nyadhifa hiyo kwa mihula minne mfululizo tangu mwaka 2000, hadi alipotangaza kuondoka mwaka 2017 na kuhamia Chadema.

Waziri huyo wa zamani wa Maliasili alijiuzulu kwa kile alichoeleza; kutoridhishwa na mwenendo wa hali ya kisiasa nchini pamoja na ukiukwaji wa haki za binaadamu, ongezeko la vitendo vya dhulma dhidi ya baadhi ya Watanzania.

Jina la tatu ni Dkt. Mayrose Majige aliepata kura 1.

Alikuwa mwanamke pekee kati ya wanaume hao wawili. Jina lake sio maarufu katika siasa za Tanzania, na huenda sio maarufu hata ndani ya Chadema.

Lakini amekuwa ni mwanaharakati wa kuheshimika akiongoza mapambano dhidi ya ufisaidi.

Kwa hesabu hizo, Tundu Lissu anakuwa mpeperushaji wa bendera ya chama chake, pindi tu mkutano mkuu utakapo mpitisha rasmi.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa mwanasiasa huyo na mwanasheria kitaaluma kukiwakilisha chama chake kugombea urais.

Mmoja kati ya atakaochuana nao hapo Oktoba ni hasimu wake kisiasa na Rais wa sasa Dkt John Pombe Magufuli wa CCM. Kama ni kabumbu tungesema mtanange huu hatumwi mtoto dukani.

Kipi kimempa nguvu?
Katika nyakati hizi ambazo kukosoa-kosoa kunaonekana kuhatarisha nafasi ya mtu kuendelea kubaki uraiani.

Mtu kama Lissu ambaye hajawahi kuogopa kukosoa kabla na hata baada kushambuliwa, anatazamwa kama shujaa kwa wale ambao wanatamani kufumbua midomo yao kwa kutoridhishwa na baadhi ya mambo ya utawala lakini wanaogopa.

Upinzani wake wa kusema bila kuogopa ndiyo karata iliowashawishi wajumbe kumpa kura nyingi dhidi ya wagombea wengine. Kwa Chadema huyu ndiye mgombea imara na sahihi zaidi kwa kuiangalia ramani ya siasa za sasa.

Si hivyo tu, upinzani wake kwa utawala unampa mvuto pia kwa raia ambao hawaridhishwi na namna mambo yalivyoendeshwa kwa miaka mitano. Anapata uungwaji mkono hadi kutoka kwa wafuasi wengine wa vyama vya upinzani na wanaharakati ambao hawako katika vyama.

Wapo wanaodhani kutokuwepo nchini kwa takribani miaka mitatu akiwa nje kwa matibabu kumeathiri ushawishi wake wa kisiasa. Ukweli wa mambo ni kinyume chake, kushambuliwa na kwenda ughaibuni kumezidisha ushawishi wake ndani ya Chadema na nje ya chama hicho.

Bado ana mvuto na ushawishi mkubwa ambao ni tishio kwa wagombea wengine hasa yule wa chama tawala.

Kupitishwa kwake ni salamu za wazi wazi kwa wagombea hao wanaokitaka kiti cha Urais, kwamba wasitegemee shughuli kuwa nyepesi katika kinyanganyiro hicho.

Ni jambo lisilo na uhakika ikiwa vyama vya upinzani hasa kile cha ACT Wazalendo kitashirikiana na Chadema au la. Ikitokea wakikubali kushirikiana na wakamkubali Lissu kuwa mgombea wao wa urais, nguvu na kitisho chake vitazidi maradufu.

Kabla ya kupigwa risasi alikuwa ni mkosoaji hai wa utawala wa Rais Magufuli, hivyo kupambana na mgombea huyo wa chama tawala katika sanduku la kura, kwake itakuwa ni mbinu nyengine katika muendelezo wa mapambano yake dhidi ya mtawala anayemkosoa kwa sera na utendaji wake.

Changamoto zinazomkabili
Moja ya changamoto kubwa inayomkabili ni kuirudisha imani ya wapiga kura na wafuasi wa Chadema.

Miaka mitano iliyopita wafuasi wengi wa vyama vya upinzani kikiwemo cha kwake, wamepoteza imani na vyama hivyo kwa sababu ya utitiri wa wanasiasa waliokuwa wanavihama na kwenda CCM.

Wapo Wabunge, madiwani na hata mgombea wao wa urais katika uchaguzi wa 2015 ndugu Edward Lowassa.

Katika mazingira hayo Lissu atakuwa na kazi ya ziada kuwashibisha imani wafuasi kwamba wagombea wa ngazi zote wanaopitishwa watathamini kura za wafuasi wao. Wala hawatoifanya Chadema kuwa daraja la kuelekea Bungeni kisha wakabadili muelekeo angani.

Usalama wake ni changamoto nyengine inayomkabili. Waliotekeleza mpango wa kutaka kumuua hakuna taarifa za kukamatwa kwao, tafsiri yake ni kwamba bado wako huru kama yeye alivyo huru. Hakuna ajuaye ikiwa dhamira yao ya kumuua wameibatilisha ama bado iko pale pale.

Pia lipo swali kuhusu afya ya mguu wake uliojeruhiwa kwa risasi za moto; atakuwa na nguvu ya kuvinjari katika mizunguko ya kampeni za nchi nzima? Kwa maslahi mapana ya kisiasa na mbio zake za urais atahitajika kuwathibitishia kivitendo wafuasi wake kwamba anao uwezo huo bila ya tatizo lolote.

Lissu na Chadema
Lissu aliyezaliwa Januari 1968 ni makamo mwenyekiti wa Chadema Tanzania bara. Aliwahi kuwa Mbunge wa jimbo la Singida Mashariki kupitia chama hicho kinachofuata nadharia za mrengo wa wastani wa kulia.

Chadema kipo hai tangu uchaguzi wa kwanza 1995 baada ya mfumo wa vyama vingi kurejea tena nchini. Kimekuwa chama kikuu cha upinzani Tanzania bara tangu uchaguzi wa 2010. Kimeitikisa vyema CCM.

Kwa mujibu wa ripoti ya taasisi ya Utafiti ya Twaweza ya jijini Dar es Salaam, ya mwaka 2017, inakielezea Chadema kama chama kinachowavutia zaidi vijana na wasomi.

Hiyo ikiwa ni tofauti na chama tawala ambacho ripoti ilieleza kinavutia zaidi wazee.

Swali la ikiwa Lissu atashinda uchaguzi au la, hilo halina jawabu kwa sasa.

Sio kwake tu, bali hata kwa wagombea wengine wa nafasi hiyo, hakuna mwenye jawabu kuhusu nani atashinda.

Lenye uhakika ni kuwa ushindani utakuwa mkubwa hadi pale mshindi atakapo tangazwa.

Je, Tundu Lissu ataandika historia ya kuipindua meza ya CCM na kuking'oa madarakani chama hicho kikongwe?

Ama atapita na kukiacha kama walivyopita wengine?

Hayo yote hayahitaji utabiri, ni kusubiri na kuona kile kitakachotokea katika uchaguzi wa mwaka huu.

Chanzo

Je, Tundu Lissu ana nguvu gani dhidi ya wagombea wengine wa urais? - BBC News Swahili

View attachment 1526684
Umedadavua vizuri kuliko yule jamaa anaitwa Wakudadavua.
 
Mkuu
Asee, unampamba lisu as ni mumeo! Anyway, 98% ya ulichoandika is rubbish. Ungeweka angalau matokeo ya study uliyofanya juu ya hayo uliyoweka hapo at least ungeeleweka. Kwa ushauri tu better not to generalise unapoamua kujenga hoja hasa iwapo huwezi ku-support hoja yako kwa facts. Kwa mfano how do you define "jamii"? Ni jamii ipi inayomuona lisu ni Shuja wake?
Una vivu. Kama kampamba basi na wewe sema japo kidogo unavyomdahamu Lissu.
 
..kwanza, TL ana HISTORIA ya kutetea wananchi tangu akiwa kijana mdogo, tena akiwa hana ulinzi wala cheo.

..hiyo ni tofauti na wale wanaotetea wananchi baada ya kupata ulinzi, walipokuwa hawana ulinzi walikuwa upande wa madhalimu.

..pili, TL ktk macho ya jamii ni SHUJAA. tukio la kumshambulia limemuongezea imani, huruma, na mapenzi ya wananchi.

..tatu, ni msomi na ni miongoni mwa wanasiasa wachache wenye kipaji cha kujenga hoja. TL akianza kuongea siyo rahisi kumchosha msikilizaji wake kwani huwa hatabiriki.

..nne, ni muelewa wa mambo mengi sana ya kisheria, kiutawala, na kiuongozi. hili ni eneo ambalo amewazidi wanasiasa wengi. kama utagundua siku hizi wanasiasa wengi wamejificha kwenye dini na maandiko ya misahafu. TL ni tofauti kabisa.

..kwa maoni yangu, upinzani haujawahi kuwa na mgombea mwenye vigezo vingi vizuri, imara, na maarufu, kama Tundu Lissu.
Kweli kabisa hatujawahi kupata mgombea asiye na doa wala mawaa kama TL
 
..dah!

..wewe inaelekea unahemkwa kwa CHUKI.

..TL angekuwa ni mtu wa hovyo tusingekuwa tunamzungumzia hapa.
Uwelewa wako una mashaka na huna sifa ya kuwa great thinker iwapo uchambuzi wako ndio umekufikisha hapo! Read between lines ni wapi nimemtaja lisu ni wa hovyo au nimeonyesha chuki wapi dhidi ya lisu?
 
Atakuwa ni 'Mshindani' mzuri kwa Mgombea Urais wa CCM Dkt. Magufuli ila ' Timing' ya ujio wake na 'Kujikita' zaidi katika Kuutaka Urais kwa manoni yangu kama GENTAMYCINE umekuja wakati mbaya. Siyo Siri japo Rais Dkt. Magufuli ana 'Changamoto' zake kadhaa za 'Kiuongozi' na hata 'Kitabia' ila katika Kuisukuma Tanzania katika 'Maendeleo' ya Kimsingi kabisa amefanya mengi, makubwa na yanayoonekana labda ni kwa 'Mpumbavu' tu pekee.

Nilisema mahala hapa hapa JamiiForums kuwa sishauri Mheshimiwa Tundu Lissu 'agombee' Urais wa Tanzania kwa mwaka huu bali 'nilipendekeza' kuwa angejengwa na kujijenga zaidi kwa mwaka 2025 ambao kwa Mimi 'Mtazamo' wangu naona kuwa ndiyo unaweza kuwa 'Anguko' kubwa la CCM ( kama nayo isipojitathmini ) kutokana na kwamba kuna 'Matabaka' makubwa, Chuki kubwa na hata Kuhasimiana Kwingi ila kwa sasa Mweyekiti Taifa ( CCM ) anajitahidi 'Kufunika' hilo 'Fukuto' kwa Mamlaka yake.

Pamoja na kwamba nimesema huenda kwa mwaka 2025 ingekuwa ni vyema na wakati sahihi kwa Mheshimiwa Tundu Lissu 'Kugombea' na angeweza kuwa na 'impact' kubwa nchini kwakuwa Rais Dkt. Magufuli ( CCM ) atakuwa anaondoka, lakini ubaya ( hasara Kwake na kwa CHADEMA ) ni kwamba hata kwa mwaka huu 2020 ambapo Lissu atakuwa 'Flag Bearer' wa CHADEMA bado CCM watafaidika na kuzidi ' Kujiimarisha' zaidi Kisiasa hasa kwa 'Changamoto' ambazo atakuwa akizitoa / akizinadi Jukwaani wakati wa Kampeni.

CHADEMA imemuharakisha sana Tundu A. Lissu 'Kugombea' kwa mwaka huu ila kwa mwaka 2025 nina uhakika angeleta 'Ushidani' ule ninaoutaka.
Ninachoona kwenye maelezo marefu haya ni woga wako juu ya Lissu. Kwanini unataka Lissu agombee mwaka 2025 na sio sasa. Eti asubiri jpm aondoke why?? What is special 2025 na kwanini not now! Nini kitakuwa kimebadilika??
Acha alione mwenyewe. Lissu is the number One Choice for Tanzanins.
 
Atakuwa ni 'Mshindani' mzuri kwa Mgombea Urais wa CCM Dkt. Magufuli ila ' Timing' ya ujio wake na 'Kujikita' zaidi katika Kuutaka Urais kwa manoni yangu kama GENTAMYCINE umekuja wakati mbaya. Siyo Siri japo Rais Dkt. Magufuli ana 'Changamoto' zake kadhaa za 'Kiuongozi' na hata 'Kitabia' ila katika Kuisukuma Tanzania katika 'Maendeleo' ya Kimsingi kabisa amefanya mengi, makubwa na yanayoonekana labda ni kwa 'Mpumbavu' tu pekee.

Nilisema mahala hapa hapa JamiiForums kuwa sishauri Mheshimiwa Tundu Lissu 'agombee' Urais wa Tanzania kwa mwaka huu bali 'nilipendekeza' kuwa angejengwa na kujijenga zaidi kwa mwaka 2025 ambao kwa Mimi 'Mtazamo' wangu naona kuwa ndiyo unaweza kuwa 'Anguko' kubwa la CCM ( kama nayo isipojitathmini ) kutokana na kwamba kuna 'Matabaka' makubwa, Chuki kubwa na hata Kuhasimiana Kwingi ila kwa sasa Mweyekiti Taifa ( CCM ) anajitahidi 'Kufunika' hilo 'Fukuto' kwa Mamlaka yake.

Pamoja na kwamba nimesema huenda kwa mwaka 2025 ingekuwa ni vyema na wakati sahihi kwa Mheshimiwa Tundu Lissu 'Kugombea' na angeweza kuwa na 'impact' kubwa nchini kwakuwa Rais Dkt. Magufuli ( CCM ) atakuwa anaondoka, lakini ubaya ( hasara Kwake na kwa CHADEMA ) ni kwamba hata kwa mwaka huu 2020 ambapo Lissu atakuwa 'Flag Bearer' wa CHADEMA bado CCM watafaidika na kuzidi ' Kujiimarisha' zaidi Kisiasa hasa kwa 'Changamoto' ambazo atakuwa akizitoa / akizinadi Jukwaani wakati wa Kampeni.

CHADEMA imemuharakisha sana Tundu A. Lissu 'Kugombea' kwa mwaka huu ila kwa mwaka 2025 nina uhakika angeleta 'Ushidani' ule ninaoutaka.
Leo nitapingana na wewe Genta. Hapana Huu ndo wakati sahihi wa Lissu kupambana na CCM na huu ndo wakati sahihi wa Lissu kupambana na JPM.

Ni rahisi sana Lissu kumshinda JPM mwaka huu hapo October kuliko kupambana na mwana CCM mwingine 2025.

Ni ukweli usiopingika kuwa Magufuli ameonesha makosa ya waziwazi ambayo kwa makosa hayo ni rahisi sana kumuadhibu yeye.

kuwatukana wakazi wa kagera, maamuzi ya hovyo yaliyoharibu soko la korosho, mbaazi na mahindi, kusababisha kupanda bei ya sukari na kuua sekta binafsi kulikosababisha ukosefu mkubwa wa ajira na kubambikia watu makesi na kuwapoteza ni makosa ya wazi ya magufuli ambayo nina uhakika yatamgharimu yeye na Chama chake sana mwaka huu.

Hakuna mwaka ambao ni rahisi kuiangusha CCM kama mwaka huu kwa sababu pia Magufuli kafanya makosa hadi kwa wana CCM. Kuwanyanyasa wazee kama Kinana na Makamba na kumfukuza wazi membe kwa kumchallenge tu ni makosa makubwa ya magufuli kwa sababu imefanya hata ushawishi wake ndani ya CCM kuwa mdogo sana. Kuwa acha wana CCM na kuwapa vyeo wapinzani wanaonuunga mkono pia kumeondoa morali ya wana CCM kumtetea na kumpigania.

Napenda kumaliza kwa kusema kama mbuzi kuelekea kibra ndo CCM kwa mwaka huu. Nampa asilimia 70 Lissu kumshinda magufuli kwa sababu Magufuli hana nguzo ya kuegamia. Ameharibu kote na Ndo mana Lissu anakuwa na kujiamini sana maana hata hao watumishi wa umma watakaosimamia uchaguzi wanaweza kumnawa Magufuli.

Namtakia Heri raisi mtarajiwa wa Tanzania Tundu Antupas Lissu
 
Katika karata CHADEMA wamepatia ni kumpa nafasi TL ,vumbi linakaribia kutimka waungane na ACT nguvu iongezeke ila wawe makini pia.
 
..kwanza, TL ana HISTORIA ya kutetea wananchi tangu akiwa kijana mdogo, tena akiwa hana ulinzi wala cheo.

..hiyo ni tofauti na wale wanaotetea wananchi baada ya kupata ulinzi, walipokuwa hawana ulinzi walikuwa upande wa madhalimu.

..pili, TL ktk macho ya jamii ni SHUJAA. tukio la kumshambulia limemuongezea imani, huruma, na mapenzi ya wananchi.

..tatu, ni msomi na ni miongoni mwa wanasiasa wachache wenye kipaji cha kujenga hoja. TL akianza kuongea siyo rahisi kumchosha msikilizaji wake kwani huwa hatabiriki.

..nne, ni muelewa wa mambo mengi sana ya kisheria, kiutawala, na kiuongozi. hili ni eneo ambalo amewazidi wanasiasa wengi. kama utagundua siku hizi wanasiasa wengi wamejificha kwenye dini na maandiko ya misahafu. TL ni tofauti kabisa.

..kwa maoni yangu, upinzani haujawahi kuwa na mgombea mwenye vigezo vingi vizuri, imara, na maarufu, kama Tundu Lissu.
Mkuu upo sawa kabisa tangu mfumo wa vyama vingi uanze hapa nchini Upinzani haujawahi kuwa na mgombea Uraisi mwenye sifa na vigezo vingi kama 2020 hakika nakwambia lisu atawashangaza wanaoishi kwa kukalilishwa, hakuna malefu ya siyokuwa na mwisho
 
Wewe sema ndiyo utamnyima kura lkn wengine watampigia kura za kutosha
Uchambuzi mwanana, Ila ujue tu siasa sasa inaanza na TL anashida pia ya kuuhakikishia uma kwamba hajatumwa na Wazungu .. Hii ni propaganda ndogo lakini kwa aina ya mtanzania inamnyima kura.
 
Uchambuzi mwanana, Ila ujue tu siasa sasa inaanza na TL anashida pia ya kuuhakikishia uma kwamba hajatumwa na Wazungu .. Hii ni propaganda ndogo lakini kwa aina ya mtanzania inamnyima kura.
Watanzania wa sasa ni smart. Mfano mdogo ni kutoka kWa wajumbe.
 
Back
Top Bottom