Uchaguzi 2020 Je, Tundu Lissu ana nguvu gani dhidi ya wagombea wengine wa urais?

Na hii ndio itakayompoteza mazima. Mtu akisikia tu jamaa katumwa na mabeberu basi kwisha kazi

Senti bai yuzingi tecno T301

Dunia hii nani anaamini hiyo propaganda ya kizee? Labda ww na wazee wenzako mlioishi kabla ya mwaka 90. Wapiga kura wengi ni wa miaka ya 90 kwenda mbele, ambao ni wapiga kura wa upinzani, hizo slogan za kizee hazina maana yoyote kwao. Hii ndio sababu ccm inatumia mabavu kukaa madarakani, maana haina mvuto wa kizazi hiki.
 
Kwani kuna ubaya gani akigombea mwaka huu na iwapo akashindwa agombee tena mwaka unaoutaka mkuu??

Ni kweli kabisa, kwanza unapoingia kwenye ushindani kuna kushinda na kushindwa, cha muhimu ni kushinda au kushindwa kihalali.
 
Uchambuzi mwanana, Ila ujue tu siasa sasa inaanza na TL anashida pia ya kuuhakikishia uma kwamba hajatumwa na Wazungu .. Hii ni propaganda ndogo lakini kwa aina ya mtanzania inamnyima kura.

Hii propaganda mfu ina nguvu kwa wanaccm, ambao bila hata hiyo propaganda hawawezi kumpa Lisu kura.
 
Mkuu October nikaribu sana kuwa mpole

Senti bai yuzingi tecno T301
 
Sina tatizo na umbali au ukaribu wa mwezi Oktoba, ninajali uchaguzi wa haki tu.
Usije kimbia humu. Watanzania wa leo sio wajinga, wanajua nani Rais nani msindikozaji.

Senti bai yuzingi tecno T301
 
Asee, unampamba lisu as ni mumeo! Anyway, 98% ya ulichoandika is rubbish. Ungeweka angalau matokeo ya study uliyofanya juu ya hayo uliyoweka hapo at least ungeeleweka. Kwa ushauri tu better not to generalise unapoamua kujenga hoja hasa iwapo huwezi ku-support hoja yako kwa facts. Kwa mfano how do you define "jamii"? Ni jamii ipi inayomuona lisu ni Shuja wake?
 

..dah!

..wewe inaelekea unahemkwa kwa CHUKI.

..TL angekuwa ni mtu wa hovyo tusingekuwa tunamzungumzia hapa.
 
Umedadavua vizuri kuliko yule jamaa anaitwa Wakudadavua.
 
Mkuu
Una vivu. Kama kampamba basi na wewe sema japo kidogo unavyomdahamu Lissu.
 
Kweli kabisa hatujawahi kupata mgombea asiye na doa wala mawaa kama TL
 
..dah!

..wewe inaelekea unahemkwa kwa CHUKI.

..TL angekuwa ni mtu wa hovyo tusingekuwa tunamzungumzia hapa.
Uwelewa wako una mashaka na huna sifa ya kuwa great thinker iwapo uchambuzi wako ndio umekufikisha hapo! Read between lines ni wapi nimemtaja lisu ni wa hovyo au nimeonyesha chuki wapi dhidi ya lisu?
 
Ninachoona kwenye maelezo marefu haya ni woga wako juu ya Lissu. Kwanini unataka Lissu agombee mwaka 2025 na sio sasa. Eti asubiri jpm aondoke why?? What is special 2025 na kwanini not now! Nini kitakuwa kimebadilika??
Acha alione mwenyewe. Lissu is the number One Choice for Tanzanins.
 
Leo nitapingana na wewe Genta. Hapana Huu ndo wakati sahihi wa Lissu kupambana na CCM na huu ndo wakati sahihi wa Lissu kupambana na JPM.

Ni rahisi sana Lissu kumshinda JPM mwaka huu hapo October kuliko kupambana na mwana CCM mwingine 2025.

Ni ukweli usiopingika kuwa Magufuli ameonesha makosa ya waziwazi ambayo kwa makosa hayo ni rahisi sana kumuadhibu yeye.

kuwatukana wakazi wa kagera, maamuzi ya hovyo yaliyoharibu soko la korosho, mbaazi na mahindi, kusababisha kupanda bei ya sukari na kuua sekta binafsi kulikosababisha ukosefu mkubwa wa ajira na kubambikia watu makesi na kuwapoteza ni makosa ya wazi ya magufuli ambayo nina uhakika yatamgharimu yeye na Chama chake sana mwaka huu.

Hakuna mwaka ambao ni rahisi kuiangusha CCM kama mwaka huu kwa sababu pia Magufuli kafanya makosa hadi kwa wana CCM. Kuwanyanyasa wazee kama Kinana na Makamba na kumfukuza wazi membe kwa kumchallenge tu ni makosa makubwa ya magufuli kwa sababu imefanya hata ushawishi wake ndani ya CCM kuwa mdogo sana. Kuwa acha wana CCM na kuwapa vyeo wapinzani wanaonuunga mkono pia kumeondoa morali ya wana CCM kumtetea na kumpigania.

Napenda kumaliza kwa kusema kama mbuzi kuelekea kibra ndo CCM kwa mwaka huu. Nampa asilimia 70 Lissu kumshinda magufuli kwa sababu Magufuli hana nguzo ya kuegamia. Ameharibu kote na Ndo mana Lissu anakuwa na kujiamini sana maana hata hao watumishi wa umma watakaosimamia uchaguzi wanaweza kumnawa Magufuli.


Namtakia Heri raisi mtarajiwa wa Tanzania Tundu Antupas Lissu
 
Katika karata CHADEMA wamepatia ni kumpa nafasi TL ,vumbi linakaribia kutimka waungane na ACT nguvu iongezeke ila wawe makini pia.
 
Mkuu upo sawa kabisa tangu mfumo wa vyama vingi uanze hapa nchini Upinzani haujawahi kuwa na mgombea Uraisi mwenye sifa na vigezo vingi kama 2020 hakika nakwambia lisu atawashangaza wanaoishi kwa kukalilishwa, hakuna malefu ya siyokuwa na mwisho
 
Wewe sema ndiyo utamnyima kura lkn wengine watampigia kura za kutosha
Uchambuzi mwanana, Ila ujue tu siasa sasa inaanza na TL anashida pia ya kuuhakikishia uma kwamba hajatumwa na Wazungu .. Hii ni propaganda ndogo lakini kwa aina ya mtanzania inamnyima kura.
 
Uchambuzi mwanana, Ila ujue tu siasa sasa inaanza na TL anashida pia ya kuuhakikishia uma kwamba hajatumwa na Wazungu .. Hii ni propaganda ndogo lakini kwa aina ya mtanzania inamnyima kura.
Watanzania wa sasa ni smart. Mfano mdogo ni kutoka kWa wajumbe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…