Mimi sio shabiki kindaki ndaki wa mpira lakini kwenye hili suala mashabiki inabidi na wao waoneshe msimamo wao. Wanachotakiwa kufanya ni kutokuingia uwanjani siku mpya ya mechi (itakayopangwa na bodi). Naamini kuna viongozi wa mashabiki wa hivi vilabu viwili, watoe msimamo wao kuwa pesa walizolipia kwenye mchezo huu zitumike kwenye michezo mingine ila sio mchezo mpya wa Yanga ya Simba. Wacheze wenyewe uwanjani bila mashabiki na mapato ya uwanjani ili liwe funzo waache kucheza na akili na pesa za mashabiki. Tofauti na hivyo hivi vilabu na hao TFF/Bodi hawataacha huu ujinga kamwe!