Logikos
JF-Expert Member
- Feb 26, 2014
- 15,460
- 24,233
Tumetukuwa tukitegemea Vyama vya Upinzani kuibua Madudu ya Chama Tawala; Binafsi naamini kwamba Vyama ni Muunganiko wa Watu wenye Mawazo yanayofanana ya jinsi gani tunaweza kutoka hapa na kufika pale..... Kama tunakwenda mjini wengine wanaweza kuamini tutembee kwa miguu ili tujenge Afya na kupunguza vitambi hivyo tukifika mjini tufanye shopping..., Wengine wanaweza kuona kwamba tupande magari ili tufike haraka na tutumie muda mfupi kwenda Gym kupunguza vitambi na kupata muda mrefu zaidi kufanya shopping...., kwahio mwananchi ataungana na watembea kwa miguu au watumia magari kwa kutumia utashi wake wa kuona faida na hasara ya kufanya atakachofanya.
Kwa kutegemea Wapinzani ndio wafumue / waonyeshe madudu ya Watawala ni kweli watafanya hivyo kama kufanya hivyo kutawasaidia wao kutawala lakini kama kile watawala wanachofaidika nacho na wao kinawanufaisha basi hawatakikemea, mfano katika suala la kupandishiana mishahara Bungeni pande zote mbili zitaungana na kutetea kwamba kinachofanyika ni sawa.
Hivyo basi watu pekee wenye motive ya kuibua madudu haya ni Tasnia ya Habari na waandishi wa habari wenye moyo, ujasiri, uzalendo na wasio na njaa na wanaolindwa kisheria kuweza kuibua madudu yoyote kwa yoyote wakati wowote. Na wanaweza kufanya hivyo iwapo tu Sheria itawalinda na Taasisi yao kuwa na uwezo wa kifedha na kutokutegemea hisani ya hao Wanasiasa... Pia wao Kama Muhimili mwingine wanaweza wakawa pia na Muwakilishi wao Bungeni (Na sio kuwakilishwa na Mwanasiasa / Waziri wa Chama Tawala)
Pili itungwe Sheria ya Mwanasiasa yoyote tunayempa Kodi zetu (Ruzuku) angalau mara moja kila mwezi kwa lazima aweze kutenga muda ambapo mwanahabari anaweza kumuuliza chochote kuhusu shughuli zake na aweze kujibu bila kukataa wala kupinga wala kuchagua ni nani wa kumuuliza au kumuhoji.
Iwapo Legislative (Bunge) Limeshindwa kuisimamia Serikali huenda ni wakati wa Tasnia ya Habari iweze Ku-balance mambo katika nyakati hizi ambazo hakuna checks and balances na wanasiasa wamekuwa na ubinafsi, umimi na kuangalia maslahi yao kuliko ya Common Mwananchi... Karne hii ya Siasa za Kushambuliana ili Wapinzani wapate Kula; NA wengine kujilinda ili waendelee kula na Kutawala - Tunahitaji a Different Player in the Mix.