Kaka mkubwa
Pascal Mayalla utanisahihisha endapo nitakua nimekosea; kashfa almost zote nchi hi zimeibuliwa na vyombo vya habari, Loliondo scandal iliibuliwa na mwandishi wa habari wa gazeti la Mfanyakazi, huyu huyu ndio aliandika kwa kirefu pia kashfa ya safari ya wakulu kule Ridejeneiro Brasili, mwandishi alikua akiitwa Francis Katabalo. Kashfa ya IPTL katikati ya miaka ya 90 as well it was the media of that time, Escrow account scandal was also mentioned by the Citizen news paper na Kafulila ndio akaishikia bango. Labda kashfa ya EPA ndio sina kumbukumbu kama iliibuliwa na waandishi wa habari, hi ilizungumzwa sana na mhe Dr. Slaa. Buzwagi Saga again was one of the best job done by our media na Zitto Kabwe akaikomalia hadi kumpa umaarufu wa kutosha. Jukwaa hili la siasa those times likijulikana kama Jambo forum again was very hot. So waandishi wa habari wamekua wana play role yao muda wote, sema sasa hivi kuna Twitter/X na mitandao mingine ya kijamii, watu wanarusha vimeo kupitia huko then vinadakwa na wengine baada ya uchunguzi; hotest one is bwana Kigogo as za JPM, kwako kaka mkubwa
Pascal Mayalla