Je, tutegemee wapinzani kuibua madudu ya Chama Tawala au tupate Wanahabari wazalendo wenye nguvu za Kisheria kuibuia madudu ya wanasiasa

Hao majizi wa chadema serikali na vyombo vyake wameshindwa kuwachukulia hatua za kisheria ili wafungwe kwa ubadhirifu wa fedha za umma?
Exactly my point kama hakuna / hawawezi kufungana Gavana / Kutupiana Mawe sababu wote wanaishi kwenye nyumba za Vioo; Inabidi tutafute wanaoishi kwenye Msonge ili waweze kuwatupia Mawe kila inabobidi na tuhakikishe tunawalinda katika utupaji wao wa mawe
 
Usema vyema mkuu, wandishi wa habari ndio jukumu lao kuelimsha wanainchi juu ya ufisadi, uwachawa, Rushwa.
 
Kaka mkubwa Pascal Mayalla utanisahihisha endapo nitakua nimekosea; kashfa almost zote nchi hi zimeibuliwa na vyombo vya habari, Loliondo scandal iliibuliwa na mwandishi wa habari wa gazeti la Mfanyakazi, huyu huyu ndio aliandika kwa kirefu pia kashfa ya safari ya wakulu kule Ridejeneiro Brasili, mwandishi alikua akiitwa Francis Katabalo. Kashfa ya IPTL katikati ya miaka ya 90 as well it was the media of that time, Escrow account scandal was also mentioned by the Citizen news paper na Kafulila ndio akaishikia bango. Labda kashfa ya EPA ndio sina kumbukumbu kama iliibuliwa na waandishi wa habari, hi ilizungumzwa sana na mhe Dr. Slaa. Buzwagi Saga again was one of the best job done by our media na Zitto Kabwe akaikomalia hadi kumpa umaarufu wa kutosha. Jukwaa hili la siasa those times likijulikana kama Jambo forum again was very hot. So waandishi wa habari wamekua wana play role yao muda wote, sema sasa hivi kuna Twitter/X na mitandao mingine ya kijamii, watu wanarusha vimeo kupitia huko then vinadakwa na wengine baada ya uchunguzi; hotest one is bwana Kigogo as za JPM, kwako kaka mkubwa Pascal Mayalla
 
Binafsi naamini hadi mtu awe mwandishi wa habari lazima ana hobbie ya hicho kitu kwahio ni kumuwezesha kunuondokana na njaa yake na vilevile alindwe Kisheria (asiweze kushitakiwa kama whistle blower)

Binafsi nadhani bora tuache kuvipa hivi Vyama Ruzuku (Hususan CCM) na hata tuwe na mfuko wa waandishi wa Habari kwa kazi mahususi ya kuchunguza na kutuhabarisha; na wanasiasa walazimishwe kutenga muda wa kuwahabarisha hawa watu na kujibu maswali ya lolote wakati wowote....
 
Sahihi kabisa bro.
 
Hakuna mkate mgumu mbele ya chai - ni msemo uliopata umaarufu sana katika kipindi hiki cha awamu ya sita.

Kwa maneno mengine kila mtu unayemuona mbele ya macho yako anayo bei yake, ananunulika tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…