Je, uanzishapo mahusiano/umuoe nani kulingana na nyota yako?

Je, uanzishapo mahusiano/umuoe nani kulingana na nyota yako?

Billy Kimber

Member
Joined
May 20, 2022
Posts
89
Reaction score
207
Elimu ya nyota/Unajimu (Astrology) ni elimu kama zilivyo elimu nyingine japo wapo wanaoihusianisha na imani za giza lakini fikra hio nafikiri ni potofu.Unajimu ni uhusiano wa nyota na maisha ya binadamu.Hasa hasa tunaangalia mahusiano ya wakati wa kuzaliwa na sayari zilizopo katika mfumo wa jua Jua.

Binadamu wote tumeumbwa katika mojawapo ya makundi 12 ya nyota (Zodiac signs).Kila kundi katika makundi nyota 12 lina tabia tofauti,mtizamo tofauti,nguvu na haiba zinatofautiana.

Ili uishi vizuri na watu inatakiwa utambue utofauti na uheshimu hilo kwa maana hatuwezi kufafanana.Ukiachana na issue za makuzi,mazingira na malezi issue ya nyota katika maisha ya mtu inaplay part kubwa katika haiba,mitazamo pamoja na tabia ya mtu.

MAKUNDI NYOTA

Makundi nyota kama tulivyoona awali kuwa yapo 12 na yamepangwa katika mtiririko kuanzia nyota ya kwanza hadi ya mwisho.

1)Aries (Punda)- 21 March hadi 19 April (in between hizo tarehe)

2)Taurus (Ng'ombe)-20 April hadi 20 May
3)Gemini (Mapacha)-21May hadi 20June
4)Cancer (Kaa)-21June hadi 22July
5)Leo (Simba)-23July hadi 22August
6)Virgo (Mashuke)-23August hadi 22September
7)Libra (Mizani)-23 September hadi 22 October
8)Scorpio (Ng'e)-23 October hadi 21November
9)Sagittarius (Mshale)-22November hadi 21 December
10)Capricon(Mbuzi)-22December hadi 19 January
11) Aquarius(Ndoo)-20January hadi 18 February
12) Pisces (Samaki)-19 February hadi 20 March

CHAGUO SAHIHI

Ukitaka kuanzisha mahusiano/kuoa na kujihakikishia mahusiano ya muda mrefu na yenye kudumu basi chagua mojawapo ya partner katika makundi yafuatayo,

i)Kama wewe ni Aries basi chagua:Leo,Sagittarius,Libra,Gemini au Aqurius

ii)Taurus:Virgo,Capricon,Cancer,Scorpio au Pisces
iii)Gemini:Aries,Leo,Libra,Sagittarius au Aquarius
iv)Cancer😛isces,Scorpio,Virgo,Taurus au Capricon
v)Leo:Aries,Sagittarius,Libra,Gemini au Aquarius
vi)Virgo:Taurus,Capricon,Cancer,Pisces au Scorpio
vii)Libra:Gemini,Aquarius,Leo,Sagittarius au Aries
viii)Scorpio😛isces,Cancer,Virgo,Taurus au Capricon
ix)Sagittarius:Leo,Aries,Gemini,Aquarius au Libra
x)Capricon:Virgo,Taurus,Cancer,Scorpio au Pisces
xi)Aquarius:Aries,Leo,Gemini,Sagittarius au Libra
xii)Pisces:Cancer,Scorpio,Virgo,Taurus au Capricon

Tofauti na machaguo haya mahusiano yako yatakua na short term pleasure lakini in long term hayatokua na maisha marefu.
 
Binafsi mimi ni Pisces ila nina wife to be Aries.Mtoto kadata kinoma,of course mimi pia nimedata.

Sometimes utabiri wa nyota haupo sahihi kwa 100%.
Pasipo kumumunya maneno mkuu,hio ni short term pleasure but in long term she is not worth.

Wewe ni Pisces asili yako ni maji na mwenzako ni Aries asili yake ni moto.

Nyie ni watu wawili tofauti kabisa.
 
Elimu ya nyota/Unajimu (Astrology) ni elimu kama zilivyo elimu nyingine japo wapo wanaoihusianisha na imani za giza lakini fikra hio nafikiri ni potofu.Unajimu ni uhusiano wa nyota na maisha ya binadamu.Hasa hasa tunaangalia mahusiano ya wakati wa kuzaliwa na sayari ya Jua.
Nini kifanyike ukiwa umeoa mtu ambae mko tofauti kinyota?
 
Pasipo kumumunya maneno mkuu,hio ni short term pleasure but in long term she is not worth.

Wewe ni Pisces asili yako ni maji na mwenzako ni Aries asili yake ni moto.

Nyie ni watu wawili tofauti kabisa.
Huu mwaka wa pili katika uchumba na penzi bado limenoga.

Hivyo vyote unavyosema nilishafatilia sana.

Utasema maji yanazima moto ila maji yanameesha ardhi.Upepo unakoleza moto.

Pisces-introvert.
-emotional intelligent with empathy.
-detective.
-...

Ninachozungumza ninamaanisha.Utabiri wa nyota haujawahi kuwa sahihi kwa 100%.Huo ni utabiri sio uhalisia kamili wa future.Inaweza kuwa au isiwe.
 
Pasipo kumumunya maneno mkuu,hio ni short term pleasure but in long term she is not worth.

Wewe ni Pisces asili yako ni maji na mwenzako ni Aries asili yake ni moto.

Nyie ni watu wawili tofauti kabisa.
Naunga mkono hoja mimi mwenza wangu yeye ni arie na mimi ni gemnn yaani kila siku ni wapya kila nikitafta kasoro siipati ndoa imedumu mda sana na hatuchokani
 
Huu mwaka wa pili katika uchumba na penzi bado limenoga.

Hivyo vyote unavyosema nilishafatilia sana.

Utasema maji yanazima moto ila maji yanameesha ardhi.Upepo unakoleza moto.

Pisces-introvert.
-emotional intelligent with empathy.
-detective.
-...

Ninachozungumza ninamaanisha.Utabiri wa nyota haujawahi kuwa sahihi kwa 100%.Huo ni utabiri sio uhalisia kamili wa future.Inaweza kuwa au isiwe.
Yes sio 100% but inaplay part kubwa sana.Recall mahusiano yako ya nyuma utagundua kitu Mkuu
 
Yes sio 100% but inaplay part kubwa sana.Recall mahusiano yako ya nyuma utagundua kitu Mkuu
Mahusiano ya nyuma na yupi?

Kama huyu huyu aries ♈ mapenzi ndiyo yanazidi kunoga...

Hivi mkuu unajua kama katika elimu ya nyota kuna dhana ya kuwepo nyota ya 13 inayohisiwa kucheza katikati ya Pisces ♓ na aries ♈?
 
Binafsi mimi ni Pisces ila nina wife to be Aries.Mtoto kadata kinoma,of course mimi pia nimedata.

Sometimes utabiri wa nyota haupo sahihi kwa 100%.
Sababu kubwa nikwamba elimu ya nyota imefichwa sana haiko wazi kama hivi watu wanakuwa wanasomasoma tu mitandaoni,
Ndio maana ukifuata nyota za mitandaoni ni ngumu sana kutoboa kwa kufuta hayo mausia yake,
hivyo nikuwa makini sana tena sana juu ya hizi mambo.

Ila kama siku ukitaka kujua for real uhalisia wa nyota yako rudi kwenu tafuta wazee wako, ukiwa umeonekana muhitaji kweli utafunguliwa njia kujua mengi na ukweli kabisa.
Pia kwa hawa waganga nikuwa makini sana maana unaweza enda na ukaacha copy ya nyota yako huko huko kwa mganga, ila kama umehitaji kwenda huko hakikisha upate waganga wanaotumia mizimu.
ambao uganga wao sio wakufundishwa niwakurithi tu mizimu ndio humuongoza , huko unapata majibu mazuri sana na utajishangaa namna umeishi ukijua unajiamulia kumbe nyota yako inakuongoza.

katika yote mitandaoni na elimu za nyota ni matopeni tu hakuna ukweli nikubahatisha tu
 
Mahusiano ya nyuma na yupi?

Kama huyu huyu aries [emoji749] mapenzi ndiyo yanazidi kunoga...

Hivi mkuu unajua kama katika elimu ya nyota kuna dhana ya kuwepo nyota ya 13 inayohisiwa kucheza katikati ya Pisces [emoji760] na aries [emoji749]?
Boss mimi nakuelewa kwa ni nini umeshikiria huo msimamo.Ni nature ya binadamu hapendi kuambiwa mambo ambayo yanakinzana na kile ambacho anakipenda na kukiamini.

Ukweli utabaki kuwa ukweli tu
 
Sababu kubwa nikwamba elimu ya nyota imefichwa sana haiko wazi kama hivi watu wanakuwa wanasomasoma tu mitandaoni,
Ndio maana ukifuata nyota za mitandaoni ni ngumu sana kutoboa kwa kufuta hayo mausia yake,
hivyo nikuwa makini sana tena sana juu ya hizi mambo.

Ila kama siku ukitaka kujua for real uhalisia wa nyota yako rudi kwenu tafuta wazee wako, ukiwa umeonekana muhitaji kweli utafunguliwa njia kujua mengi na ukweli kabisa.
Pia kwa hawa waganga nikuwa makini sana maana unaweza enda na ukaacha copy ya nyota yako huko huko kwa mganga, ila kama umehitaji kwenda huko hakikisha upate waganga wanaotumia mizimu.
ambao uganga wao sio wakufundishwa niwakurithi tu mizimu ndio humuongoza , huko unapata majibu mazuri sana na utajishangaa namna umeishi ukijua unajiamulia kumbe nyota yako inakuongoza.

katika yote mitandaoni na elimu za nyota ni matopeni tu hakuna ukweli nikubahatisha tu
Nani ameificha elimu ya nyota mkuu?Nani alipaswa afundishe watu?
 
Boss mimi nakuelewa kwa ni nini umeshikiria huo msimamo.Ni nature ya binadamu hapendi kuambiwa mambo ambayo yanakinzana na kile ambacho anakipenda na kukiamini.

Ukweli utabaki kuwa ukweli tu
Hii comment nairudisha kwako huku mimi nikichukuwa nafasi ya msemaji.
 
Nani ameificha elimu ya nyota mkuu?Nani alipaswa afundishe watu?
Laiti ungekuwa umejua hiyo elimu ya nyota ungeelewa kwanini imefichwa
kunatetesi kuwa trump asingepita baada ya kumulika katika nyota, lakini ikafanyika hesabu karibia karatasi nne (inasemekana) ili jamaa awekewe msingi wakushinda bila shida.

Sasa jiulize kama kingekuwa ni kitu chepesi na kipo bila kufichwa unadhani watu wangeshindwa kusoma tu mtandaoni na wakatoboa?

Nyota inahusianisha sana na vitu vitatu sana tena sana Nyota yenyewe+Hesabu+Asili(Mizimu au wazee wako au tuseme historia ya ukoo wako nk)

Ndio maana jiulize kwanini watu walichaguliwa mke wa kuoa na ndoa zikadumu, jiulize kwanini wahindi wanachaguliwa mke na hawachomoi,

SABABU KUBWA YA KUFICHWA NIBAADA YA UTUMWA KUINGILIA MISINGI YA KIAFRIKA NA KUFANYA ELIMU ZETU NA TAMADUNI ZETU TUAMINI NI USHETANI NA UCHAWI, PIA WAZUNGU HAWAWEZI KUZIWEKA HADHARANI SABABU ITAKUSAIDIA WEWE KUAMKA NA KUWA UPANDE SALAMA.
PIA UNAWEZA UKASOMA HATA KWENYE VITABU NK ILA UWE NA MWALIMU AMBAYE NDIO ANAWEZA KUKUAMBIA HIKI SOMA HIKI SIO HIKI SOMA HIKI SIO NK
 
Back
Top Bottom