Je, uanzishapo mahusiano/umuoe nani kulingana na nyota yako?

Je, uanzishapo mahusiano/umuoe nani kulingana na nyota yako?

Laiti ungekuwa umejua hiyo elimu ya nyota ungeelewa kwanini imefichwa
kunatetesi kuwa trump asingepita baada ya kumulika katika nyota, lakini ikafanyika hesabu karibia karatasi nne (inasemekana) ili jamaa awekewe msingi wakushinda bila shida.
sasa jiulize kama kingekuwa ni kitu chepesi na kipo bila kufichwa unadhani watu wangeshindwa kusoma tu mtandaoni na wakatoboa?

nyota inahusianisha sana na vitu vitatu sana tena sana Nyota yenyewe+Hesabu+Asili(Mizimu au wazee wako au tuseme historia ya ukoo wako nk)

ndio maana jiulize kwanini watu walichaguliwa mke wa kuoa na ndoa zikadumu, jiulize kwanini wahindi wanachaguliwa mke na hawachomoi,

SABABU KUBWA YA KUFICHWA NIBAADA YA UTUMWA KUINGILIA MISINGI YA KIAFRIKA NA KUFANYA ELIMU ZETU NA TAMADUNI ZETU TUAMINI NI USHETANI NA UCHAWI, PIA WAZUNGU HAWAWEZI KUZIWEKA HADHARANI SABABU ITAKUSAIDIA WEWE KUAMKA NA KUWA UPANDE SALAMA.
PIA UNAWEZA UKASOMA HATA KWENYE VITABU NK ILA UWE NA MWALIMU AMBAYE NDIO ANAWEZA KUKUAMBIA HIKI SOMA HIKI SIO HIKI SOMA HIKI SIO NK
Hapana mkuu hapa umetudanganya

Hakuna anaeificha elimu ya nyota.Elimu ya nyota sio formal na mara nyingi inahusishwa na mambo ya imani.Issue ikishahusisha imani inakua na complication kidogo.Na pia watu wanaoifahamu sio wengi

Kuna kitu kinaitwa OCCULT ambayo hii imebeba hizi elimu (Astrology,Palmistry na Tarot).Ni study kuhusu hizi supernatural issues.
 
Kuna mdada namtaka, nimemwambia jana kuwa nampenda.. akaniuliza nimezaliwa tarehe ngapi? Nikamtajia.

Akasema nyota zetu haziendani!

Nikamuuliza kivipi? Akanambia nyota yangu mimi ni ya samaki (Pisces)- ambayo haiendani ya kwake, hivyo kama nataka mpenzi wa kudumu basi niwe na kawaida ya kutembea beach. Kule ndio nitapata mwanamke wa kuendana na mimi na si vinginevyo!

Waatalamu wa mambo vipi, kuna ukweli wowote hapo??
 
Kwan Mkuu si Kuna sun, moon and rising sign Au tunashika tuliozaliwa nayo tu!!?
 
Kwan Mkuu si Kuna sun, moon and rising sign Au tunashika tuliozaliwa nayo tu!!?
Mara nyingi ambayo ina mashiko sana ni Sun sign (tarehe ya kuzaliwa).Jua huwa linazingatiwa sana maana ndio mhimili wa Astrology.

Hivyo vingine inabidi uende deep sana.Ukijua umezaliwa saa ngapi na mahali gani ndo unaweza kujua hizo rising sign na sayari nyingine zinakuangukia kwenye nyota ipi.
 
Kuna mdada namtaka, nimemwambia jana kuwa nampenda.. akaniuliza nimezaliwa tarehe ngapi? Nikamtajia.

Akasema nyota zetu haziendani!

Nikamuuliza kivipi? Akanambia nyota yangu mimi ni ya samaki (Pisces)- ambayo haiendani ya kwake, hivyo kama nataka mpenzi wa kudumu basi niwe na kawaida ya kutembea beach. Kule ndio nitapata mwanamke wa kuendana na mimi na si vinginevyo!

Waatalamu wa mambo vipi, kuna ukweli wowote hapo??
Itakua alikuaambia ukweli.

Wanawake wengi hasa hasa hawa mabinti wa kileo huwa wanafatilia hivi vitu vya nyota.

Ukifatilia vizuri utangundua wengi kwenye Bio zao za Instagram wameweka Zodiac Sign zao na tarehe zao za kuzaliwa.
 
Ila haya mambo Yana kufuru ndani yake kwakweli.

Kuna wakati huko nyuma nilikuwa namfuatilia marehemu Sheikh Yahya channel ten,na sijui siku flan uvae nguo ya rangi flan,mara sijui na uvae Pete yenye jiwe flan nah! Nikaona hapa napotea,nikaacha hata kuangalia kabisa,kifupi sina mpango nayo kabisa hayo Mambo.
 
Nyota ukianza kuingia deep sana ndio inaweza kukufanya ukakufuru.

Tumia nyota kukupa muongozo tu wa maisha mengine achana nayo.Itakuongoza umuoe nani,ufanye shughuli gani na namna ya kuishi baada ya kugundua madhaifu yako.

Mengineyo achana nayo
 
Mim ni Sagittarius ♐️ (mshale)... haya mdada mwenye nyota ya Leo, Aries, Gemini, Aquarius, Libra akuje fasta niende ukweni kwao nkatoe posa 😂
 
Hapana mkuu hapa umetudanganya

Hakuna anaeificha elimu ya nyota.Elimu ya nyota sio formal na mara nyingi inahusishwa na mambo ya imani.Issue ikishahusisha imani inakua na complication kidogo.Na pia watu wanaoifahamu sio wengi

Kuna kitu kinaitwa OCCULT ambayo hii imebeba hizi elimu (Astrology,Palmistry na Tarot).Ni study kuhusu hizi supernatural issues.
Sawa ndugu haya mambo mimi sitaki kubishana, kuna wengine wanabisha sababu wanasoma vitabuni wengine wanabisha sababu wanayaishi
all the best
 
Scorpio (Ng'e)-23 October hadi 21November

Hapa ndio KONKII Kabisa kila niliyewahi kuwa naye nabugi Ile mbaya,alafu kama ni me unakuwa mwakitombeli Ile mbaya sijui lini ntapata match yangu.
 
Pasipo kumumunya maneno mkuu,hio ni short term pleasure but in long term she is not worth.

Wewe ni Pisces asili yako ni maji na mwenzako ni Aries asili yake ni moto.

Nyie ni watu wawili tofauti kabisa.
Watachemsha hayo maji na huo moto, wataoga, watapata chai, na pia mengine yatakuwa ya kunywa. Hebu acha kuharibu ndoa ya watu bwana. [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mama jusi
Kuamini utabiri ni jambo baya Sana watabiri Hawana tofauti na wachawi Hawa mama jusi ndo waliofanya watoto wadogo wakiume wauwawe lakini tunajifunza Mungu akiamua kuingilia Kati utabiri si kitu chochote kitachoweza fanya kazi si kwenye mahusiano au kazi
 
Watachemsha hayo maji na huo moto, wataoga, watapata chai, na pia mengine yatakuwa ya kunywa. Hebu acha kuharibu ndoa ya watu bwana. [emoji23][emoji23][emoji23]
Sikuwa na lengo baya.Ila nmejaribu kusema vitu kama vilivyo.Sio utabiri ila ni nature.

Ni kama kusema mbuzi na chui wanaweza kuishi sehemu moja.Nature haiwarusuhu wakae pamoja ila ukiwaona wamekaa pamoja ujue mda wowote mambo yatakua tofauti
 
Kuamini utabiri ni jambo baya Sana watabiri Hawana tofauti na wachawi Hawa mama jusi ndo waliofanya watoto wadogo wakiume wauwawe lakini tunajifunza Mungu akiamua kuingilia Kati utabiri si kitu chochote kitachoweza fanya kazi si kwenye mahusiano au kazi
Utabiri(Horoscope)ni kitu tofauti kidogo na Unajimu( Astrology ).Japo utabiri ni sehemu ya unajimu lakini ni kitu kingine.

Ila hapa kinachoongelewa ni Nature,vitu kama vilivyo na wala sio utabiri.

Mbuzi na Chui hawakai pamoja (hio ni nature).
Siku moja Mbuzi na Chui wataweza kukaa pamoja(Huo ni utabiri).
 
Back
Top Bottom