Je, uanzishapo mahusiano/umuoe nani kulingana na nyota yako?

Je, uanzishapo mahusiano/umuoe nani kulingana na nyota yako?

Kuna mdada namtaka, nimemwambia jana kuwa nampenda.. akaniuliza nimezaliwa tarehe ngapi? Nikamtajia.

Akasema nyota zetu haziendani!

Nikamuuliza kivipi? Akanambia nyota yangu mimi ni ya samaki (Pisces)- ambayo haiendani ya kwake, hivyo kama nataka mpenzi wa kudumu basi niwe na kawaida ya kutembea beach. Kule ndio nitapata mwanamke wa kuendana na mimi na si vinginevyo!

Waatalamu wa mambo vipi, kuna ukweli wowote hapo??
Ulimpa pesa akakataa?
 
Mama yangu ni libra na baba ni cancer. Sijaona kuendana lakini mpaka leo wako pamoja. Naomba hizi ramli chonganishi zifutwe. Kudumu ni Mungu awepo na aabudiwe kwa roho na kweli. Yeye ndo mwanzilishi..yeye ndo atamaliza kila kitu.
Mchimbe ndani kama hujakuta kuna jamaa alimzimiaga ni vile tamaduni zetu kuforce mambo...
 
Utabiri wa nyota ni uongo mtupu, masheikh kibao wanaishi hapa mjini kudanganya watu kutokana na elimu hii fake kutoka kwenye vitabu vyao vya dini. Hajabu hawasemi kuwa hii ni nguvu ya giza kwa kuwa tu wanatumia kitabu ila kama angekuwa babu yangu ananitabiria haya tena kwa ufanisi zaidi kina Abdallah wangemuita mchawi. Waafrika sijuwi nani katuroga mpaka tunajisahau namna hii.
 
Back
Top Bottom