Je, ubinafsishaji ni mbaya? Kisa cha uuzwaji wa Port Harcourt na Kaduna refinary nchini Nigeria.

Dr Adam Francis

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2011
Posts
790
Reaction score
1,316
Kwa nyakati tofauti tumekuwa na mijadala mizito kuhusu ubinafsishaji wa mashirika ya umma ambayo yamekuwa hayafanyi vizuri.

Mijadala hii kwa imekuwa ikiibua hisia tofauti miongoni mwa wananchi, wanasiasa na wadau wa maendele. Kwasababu hiyo leo ningependa kusimulia kisa cha serikali ya Obasanjo nchini Nigeria kutaka kumuuzia Dangote na Otedora, Port Harcourt and Kaduna refinary.

Mwisho mwa utawala wake mwaka 2007, Serikali ya Obasanjo nchini Nigeria iliuza asilimia 51 ya hisa katika Kiwanda cha kusafisha mafuta cha Port Harcourt na Kiwanda cha Kaduna. Mnunuzi alikuwa muungano uitwao Bluestar Oil, uliokuwa na:
Aliko Dangote
Femi Otedola
Kampuni ya Transcorp
Dangote alikuwa na hisa kubwa zaidi kwenye mpango huu.

Uuzaji huu ulipingwa vikali mara baada ya tangazo la uuzaji. Sababu za upinzani zilikuwa:
(a) Ukiukwaji wa taratibu
Sheria ilitaka uuzaji uidhinishwe na Baraza la Ubinafsishaji (NCP)
Inadaiwa mchakato huu haukufuata utaratibu rasmi
(b) Migongano ya maslahi
Kulikuwa na madai kuwa Obasanjo alikuwa na uhusiano na Transcorp
(c) Bei ndogo
Wengi walidai viwanda viliuzwa kwa bei ya chini sana kuliko thamani yake halisi
(d) Upinzani wa vyama vya wafanyakazi
Vyama vya mafuta (NUPENG, PENGASSAN) vilifanya mgomo mkubwa wa kitaifa
(e) Wasiwasi wa kiuchumi
Wanunuzi walikuwa pia wanafanya biashara ya kuagiza mafuta kutoka nje

Kutokana na upinzani mkali, mara tu baada ya kuchaguliwa, Rais Musa Yar'Adua, aliagiza uchunguzi wa mchakato wa manunuzi ufanywe mara moja ambapo ikakundulika kuwa:
1. Mchakato haukufuata sheria kikamilifu.
2. Haukuwa na manufaa ya taifa

Kutokana na ugunduzi huo, uuzaji ulifutwa kabisa na viwanda vikarudishwa serikalini

Baada ya hapo serikali iliendelea kumiliki viwanda lakini vilikuwa vikiharibika mara kwa mara
havikufanya kazi kwa ufanisi
pesa nyingi zilitumika kwa matengenezo bila mafanikio

Wakati huo huo Aliko Dangote akaamua kujenga kiwanda chake binafsi kikubwa cha kusafisha mafuta chenye uwezo mkubwa kuliko viwanda vya serikali kwa dola za kimarekani bilioni 20. Wakati huohuo inakadiriwa matengenezo ya viwanda hivyo vya serikali yameshaghalrimu dola za kimarekani bilioni 25 na mpaka sasa havijawahi kutengamaa.

Hapa kwetu Tanzania ni rahisi sana ukipita pale buguruni kuwaambia watu ona haya majengo yalikuwa ya national milling sasa yana mtajirisha Bakhresa, lakini pengine hiyo national milling ingekuwepo pale wangejaa popo.
 
Dangote amejenga lini kiwanda chake cha kusafisha mafuta na serikali imeuza lini kiwanda chake? Uhusiano wa kufilisika kiwanda cha serikali na kiwanda cha Dangote ni upi?
 
Ukiona ubinafsishaji unazuiwa jua kuna mianya ya ufisadi inalindwa kupitia mikataba ya matengenezo.
 
Tusimchoshe mleta mada. Tumuulize AI

Majibu

Ndiyo, ni kweli. Bilionea Aliko Dangote amejenga kiwanda kikubwa cha kusafisha mafuta (refinery) nchini Nigeria kinachoitwa Dangote Refinery.

Hapa kuna mambo muhimu kuhusu kiwanda hicho:

  • Mahali kilipo: Kiko katika eneo la Lekki Free Zone, mjini Lagos, Nigeria.
  • Ukubwa: Ni kiwanda kikubwa zaidi cha kusafisha mafuta duniani ambacho kiko kwenye eneo moja (single-train refinery).
  • Uwezo: Kina uwezo wa kusafisha mapipa 650,000 ya mafuta ghafi kwa siku.
  • Bidhaa: Kiwanda hiki kinazalisha petroli, dizeli, mafuta ya ndege (jet fuel), na bidhaa nyingine za kemikali (petrochemicals).
  • Lengo: Lengo kuu ni kuifanya Nigeria ijitosheleze kwa mahitaji ya mafuta na kuacha kuagiza mafuta yaliyosafishwa kutoka nje ya nchi, jambo ambalo limekuwa likigharimu taifa hilo fedha nyingi.
Kiwanda hicho kilizinduliwa rasmi mwezi Mei 2023 na kimeanza kutoa bidhaa zake sokoni hivi karibuni (mwishoni mwa 2024 na kuendelea kuelekea 2025/2026).
 
Ukiona ubinafsishaji unazuiwa jua kuna mianya ya ufisadi inalindwa kupitia mikataba ya matengenezo.
Sio wakati wote ni upigaji, wakati mwingine ni mambo ya Maslahi binafsi. Chukulia mfano wa ATCL, pamoja na kuwa inatia hasara kila siku unadhani likiletwa wazo la kuibinafsisha litakubalika na wote? Wanaonufaika na hali ya ATCL ya sasa lazima watapinga.
Katika mfano nilioutoa, serikali ya Nigeria ilikataa kumuuzia Dangote refinary mwaka 2007, toka muda huo mpaka sasa imetumia zaidi ya dola bilioni 25 kwenye matengenezo ya hivyo viwanda bila mafanikio. Lakini Dangote kajenga chake, brand-new chenye capacity kubwa kuliko cha serikali kwa dola bilioni 20 tu!
Hii ni kwasababu miradi ya serikali ina urasimu na ubadhilifu mwingi kiasi kwamba haiwezi kushindana kibiashara na hata tu kujiendesha wakati mwingine.
Mzee Mkapa kwakulijua hili aliona ni bora kuyabinafsisha mashirika yote ya umma yanayotia hasara
 
Dangote amejenga lini kiwanda chake cha kusafisha mafuta na serikali imeuza lini kiwanda chake? Uhusiano wa kufilisika kiwanda cha serikali na kiwanda cha Dangote ni upi?
Serikali ya Nigeria ya Obasanjo ilifika makubaliano ya kumuuzia Dangote viwanda vya kuchakata mafuta 2007, Baada ya Rais YarAdua kuingia madarakani akafuta mkataba wa mauziano. Dangote akaamua kujenga chake ambacho kilikamilika 2023.
Wakati huo huo viwanda vya serikali vimeendelea kuwa na matengenezo yasiyokoma na uzalishaji duni
 
Sio wakati wote ni upigaji, wakati mwingine ni mambo ya Maslahi binafsi. Chukulia mfano wa ATCL, pamoja na kuwa inatia hasara kila siku unadhani likiletwa wazo la kuibinafsisha litakubalika na wote? Wanaonufaika na hali ya ATCL ya sasa lazima watapinga.
Katika mfano nilioutoa, serikali ya Nigeria ilikataa kumuuzia Dangote refinary mwaka 2007, toka muda huo mpaka sasa imetumia zaidi ya dola bilioni 25 kwenye matengenuzo ya hivyo viwanda bila mafanikio. Lakini Dangote kajenga chake, brand-new chenye capacity kubwa kuliko cha serikali kwa dola bilioni 20 tu!
Hii ni kwasababu miradi ya serikali ina urasimu na ubadhilifu mwingi kiasi kwamba haiwezi kushindana kibiashara na hata tu kujiendesha wakati mwingine.
Mzee Mkapa kwakulijua hili aliona ni bora kuyabinafsisha mashirika yote ya umma yanayotia hasara
Ndiyo maana nikasema " ukiona " maana yake ni situation ambayo haitokei kila siku.
 
Back
Top Bottom