Pre GE2025 Je, Uchawa unazorotesha Uwajibikaji? Ipi ni namna bora ya kuhakikisha Uwajibikaji unakuwa sehemu ya Utamaduni wa Kisiasa?

Pre GE2025 Je, Uchawa unazorotesha Uwajibikaji? Ipi ni namna bora ya kuhakikisha Uwajibikaji unakuwa sehemu ya Utamaduni wa Kisiasa?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ona ulivyopanic sasa Mkuu :KEKWlaugh::KEKWlaugh:... asante kwa kunijuza zaidi kuhusu wewe
Kawaida unaona ni panic!

Hatuko katika wavelengths zilizo sawa ndo maana [1] umeshangaa jambo ambalo ni dhahiri kabisa na [2] wala sijakujuza chochote kuhusu mimi.

Una tatizo la kusoma na kuelewa. Sijakujuza chochote halafu unatoa shukrani!

Shuleni ulikuwa unapata alama gani wewe? 🤣
 
Uchawa ni tabia ya unyumbu wa kisiasa, unyumbu wa kisiasa ni tabia ya wanaopewa dhamana kuahirisha kufikiri kwa nafsi kwasababu ya kujipendekeza ama kulitumikia kundi fulani kwa masilahi binafsi na uoga wa kuigiza kwa viongozi wao, (unafiki), tuseme kuahirisha kufikiri kizalendo kwasasa uchawa ama kujizima data

Human herding in politics is an occurrence of entrusted people suspending their individual reasoning because of flattering or working towards group objectives and hypocrite
 
Usikose kujiunga nasi katika Mjadala wa "Je, 'Uchawa' unakwamisha Uwajibikaji?" Alhamisi hii ya Februari 27, 2025, kuanzia Saa 12 jioni hadi 2 usiku, kupitia Xspaces ya JamiiForums

'Washtue' ndugu, jamaa au marafiki ili wawe sehemu ya Mjadala huu muhimu kwa 'kesho' ya Nchi yetu.

Washiriki watapata fursa ya kutoa maoni au mapendekezo na kuuliza maswali Wazungumzaji wetu

Kushiriki bofya https://jamii.app/KujipendekezaSpace

Khalifa Said

"Uchawa sidhani kama unazorotesha uwajibikaji, ninavyodhani mimi kitu kikubwa kinachodhorotesha uwajibikaji ni uimla, ukatili wa kidola, matumizi ya nguvu kwa polisi na mbinu nyingine za kihuni na za kishenzi zinazotumiwa na waliopa madarakani kuwanyamazisha watu ikiwemo kuwateka"

"Vijana wengi wanajikaribisha kwenye nafasi za Viongozi kwa kuwa wanaona hiyo ndio njia salama ya wao kufanikisha mambo yao mbalimbaliKama tunataka kuondoa hali hiyo tunatakiwa kuweka msingi ambao kila mchango wa Mtu unaweza kuheshimiwa tofauti na ilivyo sasa, mfano Msanii ukiimba nyimbo tofauti na wale waliopo Madarakani inakuwa ngumu kufanikiwa"

Carlos Buto

Carlos amezungumzia kuhusu historia ya Uchawa, ameeleza uchawa haujanza leo katika nchi yetu, uchawa umekuwepo kuanzia kipidni cha mfumo wa chama kimoja lakini kwa hivi sasa unaonekana sana kutokana na uwepo wa mitandao ya kijamii. Ameeleza kuwa mifumo bora ya uchaguzi ndiyo inayoweza kuondoa kadhia hii ya uchawa.

Annastazia Rugambwa

Annastazia ameeleza na kukubali kuwa uchawa ni tatizo kubwa sana na ili kuweza kutatua uongozi wa kiimla inabidi uchawa ukomeshwe. Ameleza pia kutokana na utafiti walioufanya watanzania zaidi ya 53% wanazungumzia kuhusu hali ngumu ya maisha, wengine wameelezea kuhusu ukosefu wa ajira. Ameeleza kuwa Chanzo cha uchawa ni hali ngumu ya maisha, kama wangekuwa na hali nzuri za maisha isingekuwa rahisi kwa wao kufanya uchawa kwani uchawa ni aibu.

Uchawa unawalemaza viongozi, wanaweza wakawa na nia ya kuwasaidia wananchi lakini wanapokutana na uchawa wanasifiwa hivyo kupelekea siku wakihojiwa kuhusu uwajibikaji wao wanakuwa wakali. Amesisitiza kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya uchawa na umasikini.

Ameeleza pia kuwa umasikini ndiyo mtaji wa viongozi na hiyo ndiyo sababu ya wao kutokupambana na umasikini kwa sababu ndiyo mtaji wao. Ameuliza kama umasikini ukiondoka machawa watatoka wapi?
Uchawa ndio Tunu ya Taifa kwa Sasa. Next Month nitaanza kujiunga Uchawa full combat
 
Uchawa unakera mpaka basi. Aliyeanzisha huu upuuzi alaaniwe milele.
 
Kawaida unaona ni panic!

Hatuko katika wavelengths zilizo sawa ndo maana [1] umeshangaa jambo ambalo ni dhahiri kabisa na [2] wala sijakujuza chochote kuhusu mimi.

Una tatizo la kusoma na kuelewa. Sijakujuza chochote halafu unatoa shukrani!

Shuleni ulikuwa unapata alama gani wewe? 🤣
Asante tena kwa kuendelea kunijuza kuhusu wewe Mkuu:BearLaugh::BearLaugh: yaani unafunguka tuu
 
Uchawa sio tu unazorotesha uwajibikaji bali pia unapunguza uadilifu, uaminifu, ukweli uzalendo, weledi na viwango nchini.

Unachochea zaidi ubinafsi na kuangalia tumbo tu. Ili kufanikiwa kwenye mfumo wa uchawa inabidi upige kelele kusifia hata kama unajua unasifia uongo.
 
Back
Top Bottom