Jumong S
JF-Expert Member
- Jul 3, 2013
- 7,385
- 10,659
Wiki iliyopita nilitoka Moshi nikaenda kumtembelea classmate wangu pale Arusha. Jamaa ni engineer wa computer. Jumapili baada ya kula Ibada Safi na kwaya kali pale St. Theresa tuli-mount XR 250 na tukaenda kufunga Camera za usalama kwa nyumba mpya ya Tajiri mmoja wa Kanda ya Ziwa. Huyu mjuba kajenga mjumba wa kuishi wa ghorofa mbili. Pale kwake pazuri asee, kama Ikulu ati.
Basi tukiwa tunakomaa na kazi (mie sio mtaalam but nilikua Nampa kampani msela) jamaa alikuja na Range lake kutuletea Vifaa kadhaa. Baada ya kukabidhi alisepa. Basi jamaa yangu akawa ananiongelesha kwa kispanish chetu cha kuunga unga na solotepu. Akanambia huyu mjuba ni mchawi balaa. Pale kwake tulikuta watoto wawili wa kiume mandondocha wanatematema udenda tu.
Jamaa akanambia ni watoto wake wa kuzaa kabisa na ndo wanalinda business zake. Yes, jamaa Ana biashara kubwa ya Hardware na electronics. Nasikia pia Ana Real estate bila kuhesabu biashara nyingine huko kwao! Pale tu nilihesabu magari 4 makali bila kuhesabu maroli ya biashara. Alikua na chale Kadhaa usoni na mikononi. Inasemekana biashara zake kazizindika kwa makafara balaa!
Sasa tujiulize, je, Uchawi una nafasi gani katika kukuza Biashara? Kuna ukweli wowote katika kuinua biashara?
Je, kwa nini tusiusome ktk masomo ya vyuoni kwa maendeleo ya umma?