Je, Uchawi una mchango wowote katika kukuza Biashara?

Je, Uchawi una mchango wowote katika kukuza Biashara?

Huu ushahidi bado haujitoshelezi mkuu, mm nilifikiri baada ya ripoti kufika kwa mtaalamu pesa zikarudi katika mazingira ambayo na wewe ya kuliacha katika wakati mgumu bila kuelewa nini kilitokea.
Sijazungumzia hilo.

Baada ya wiki mbili sehemu ya walioniibia walikamatwa.

Waliwashirikisha boda boda wa eneo la karibu. Alipewa gawio la hela kidogo na maagizo ya kwenda kuitupa simu za miamala.

Bahati nzuri ama mbaya tamaa ikamuingia akaingia mtaani kuziuza. Tracking ikawakamata waliouziwa na kumtaja huyo ndugu.

Waajiri wake, walipigwa risasi baada ya kwenda kuvamia sehemu nyingine.

Sikupata hata mia, lakini simu na mashine zilirudi.
 
Hujui chochote wewe na kama kukumbatia hiyo imani yako utaendelea kuwa masikini daima, labda nikuulize ulishawahi kufanya kazi na wachina wanaojenga barabara unajua nini huwa kinafanyika ili kukamilisha ujezi? Sasa wale hata hawafichi watoa kafara live bila chenga
 
Sizungumzii kwa wengine, ila kwangu binafsi.

Nafanya biashara ya kifedha (za mtandao na benki). Mwaka 2018 nilipigwa tukio na wakulungwa wakaondoka na 28+ Million cash, simu na mashine za benki.

Nilimpigia simu mama yangu kumueleze maswaibu yaliyonipata. Alishangaa sana nimesurvive vipi zaidi ya miaka 5 bila kuzindika eneo langu la biashara.

Akanitaka niende nyumbani kwa mwitikio wa haraka. Baada ya kuandika maelezo polisi, jioni nikazama nyumbani.

Akanipeleka kwa mzee mmoja. Wala siyo mchawi, ila ni mtaalamu wa kuzindika.

Kuzindika siyo uchawi. Nikampeleka mjini. Akafanya yake akarudi.

Nimeshakosa majaribio matatu ya kuvamiwa.

Na ripoti zote nazipata kutoka polisi. Wakivamia na kukamatwa, wakihojiwa wanasema walipanga kuja kuniibia. Ila mikakati yao inafeli.

Zindiko ni muhimu sana.
Naona unaenda kuwa mchawi kamili. Hongera bwana. Kafara utaanza kutoa lini or is too soon, sadly ni mama yako mzazi ndo anakuendesha.
 
Naona unaenda kuwa mchawi kamili. Hongera bwana. Kafara utaanza kutoa lini or is too soon, sadly ni mama yako mzazi ndo anakuendesha.
nmecheka sana ,,,,jamaa anadai kuzindika sio uchawiiiiiiiii😀😀😀😀😀😀
 
Hujui chochote wewe na kama kukumbatia hiyo imani yako utaendelea kuwa masikini daima, labda nikuulize ulishawahi kufanya kazi na wachina wanaojenga barabara unajua nini huwa kinafanyika ili kukamilisha ujezi? Sasa wale hata hawafichi watoa kafara live bila chenga
Muwe mnaandika jounals kufundisha wengine na kuendeleza kipaji.
 
Sawa, kama ambavyo huniletei mkate mezani, kaa kwa kutulia.
Shida ni kwamba nikikuletea mkate unaweza nichinja kwa maagizo ya mama yako ili uzidi kutajirika. Kwa hiyo wewe na mama yako nani kamzidi mwenzie? Alafu we ni mtu mzima wa aina gani unachukua ushauri wa kijinga kiasi hiko? Kwa hiyo mama yako akikuambia utoe kafara wewe ni kitendo cha dakika zero au sio
 
Hii ni Vita Kama mlidhani Vita inaisha kirahisi au inashindwa kirahisi Kila mtu aamini anacho amini aingie na silaha anayoijua vitani ....kwenye kuleta ugali mezani sio kazini,kwenye siasa ,biashara,mashuleni hakujawai kua rahisi
 
Mkuu biashara nyingi zimezindikwa na zimepigwa kalilio la kivutia wateja, hakuna biashara mjini zinaenda kwa uzoefu . Mjini kuzito sana , last weekend nilitembelea night club flan hivi chugga nilishangaa nilipoingia mwili ulisisimka sana hata watu niliowakuta hawakuwa wakawaida na cha kushangaza club nzima nilikutana na sura ngeni halafu zinafanana we acha tu. Kipindi nipo mwanza niliwahi kuwa na mwenyeji alinisimulia mambo mengi kuhusu biashara na nguvu za Giza zinavyotumika . Duniani ni mapito tu kila mtu ashinde mechi zake kwa juhudi au kubebwa.Mjini kuzito sana , nenda kwa mfano hapa Arusha , soko kuu, Kilombero au maduka ya stendi ndogo Kama uko vizuri na Kinga za jadi utaona mengi . Wamama wa Kilombero ni nomana hata wale wauza matunda Kilombero .
Duh! Kwa hiyo tunakula uchafu wa waganga tuu?
 
Je, kwa nini tusiusome ktk masomo ya vyuoni kwa maendeleo ya umma?

Kuna elimu zimefichwa haiwezekani kuziweka katika masomo ya vyuoni

Lakini elimu hizo ukizitaka utazipata Kwa manufaa yako maana wengine wanaweza wasizihitaji
But nchi kama S Africa Kuna vyuo kabisa vya ulozi
 
Back
Top Bottom