Je, Uchawi una mchango wowote katika kukuza Biashara?

Je, Uchawi una mchango wowote katika kukuza Biashara?

Binafsi siamini katika uchawi,imagine kwenye duka lako mtaji ni mdogo na hauna baadhi za vitu mfano unafanya biashara ya phone Accessories mtu amekuja kununua lcd na wewe huna je utamuuzia uchawi?
 
Natafuta mchawi mnoma kabisa, nizindike nyumba yangu
 
Ngoja nikupe elimu kidogo kuhusu utajiri

Kwanza kuanzia Leo utambue hili, Mungu alipomuumba Adam na Eva aliwapa utajiri wote wa duniani na fahari zake wazimiliki, lakini walipohasi kwa Mungu kwa kumsikiliza shetani, utajiri wote wa duniani ukawa ni Mali ya shetani, wanadamu hatumiliki tena utajiri wa hapa duniani.

Sasa ili kuwa tajiri una options mbili tu
(1) umuombe shetani akupe sehemu ya utajiri anaomiliki, hii inawezekana kama ukikubaliana na masharti yake, na siku ukienda kinyume anakunyang'anya.
(2) umuombe Mungu akupe sehemu ya utajiri alioushikilia Shetani, na hii inawezekana kama utakuwa muombaji sana na mtakatifu haswa, kumyang'anya shetani sehemu ya utajiri wake si rahisi kihivyo.

Usijidanganye kama unaweza kuwa tajiri kwa kufuata seminar za motivation speaker peke yake, utajiri wote anao shetani, ni either uungane naye au upambane kumyang'anya.
nami nitakupa hazina za gizani, na mali zilizofichwa za mahali pa siri, upate kujua ya kuwa mimi ni BWANA, nikuitaye kwa jina lako, naam, Mungu wa Israeli. Isaya 45:3.
 
Back
Top Bottom