Wewe una maarifa upande wa pili.
Kwa upande wa Mungu mafanikio yanawezekana kama ukiwa muombaji na mtoaji na utakatifu, inawezekana kabisa.
Bila Baba yangu mzazi(marehemu sasa) alikuwa mchungaji, yeye nilipomwambia nataka niwe mjasiriamali, aliniambia kabisa mwanangu please kaajiriwe, sababu utaashia kuwa mshirikina tu, na itakuwa aibu mtoto wa mchungaji kuwa mshirikina.
Nikamwambia baba sitaenda kwa mganga.
Akaniambia ukitaka kuwa mfanyabiashara inabidi uache huo ulokole wa kusali jumapili, inabidi uwe muombaji wa kila siku.
Nikaanza biashara na ulokole wa kuunga unga kilichonipata, niliuza mpaka gari yangu, kiwanja changu nilivyovipata kwenye ajira, baba yangu akaniambia, nilikuambia mwanangu rudi kwenye ajira, biashara inahitaji uchawi sana au muombaji sana.
Kwa mara ya kwanza nikaanza kufunga na kuomba.
Unajua Nini nilifunga siku 30 ili nirudi kwenye biashara again....
Nilifanikiwa lakini ilinichukua almost 3 years kurudi kwenye ramani.
Leo hii, mimi siwezi kufungua duka bila kupitia Kijitonyama KKKT, kusali misa ya asubuhi. Ijumaa lazima niende kwenye mkesha, yale yale aliyoniambia baba yangu ilinidi nikubali ili biashara iende