Bufa
JF-Expert Member
- Mar 31, 2012
- 12,599
- 26,263
Sizungumzii kwa wengine, ila kwangu binafsi.
Nafanya biashara ya kifedha (za mtandao na benki). Mwaka 2018 nilipigwa tukio na wakulungwa wakaondoka na 28+ Million cash, simu na mashine za benki.
Nilimpigia simu mama yangu kumueleze maswaibu yaliyonipata. Alishangaa sana nimesurvive vipi zaidi ya miaka 5 bila kuzindika eneo langu la biashara.
Akanitaka niende nyumbani kwa mwitikio wa haraka. Baada ya kuandika maelezo polisi, jioni nikazama nyumbani.
Akanipeleka kwa mzee mmoja. Wala siyo mchawi, ila ni mtaalamu wa kuzindika.
Kuzindika siyo uchawi. Nikampeleka mjini. Akafanya yake akarudi.
Nimeshakosa majaribio matatu ya kuvamiwa.
Na ripoti zote nazipata kutoka polisi. Wakivamia na kukamatwa, wakihojiwa wanasema walipanga kuja kuniibia. Ila mikakati yao inafeli.
Zindiko ni muhimu sana.
Huu ni utopolo.