Masokotz
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 3,973
- 6,750
Habari za wakati huu;
Ni matumaini yangu kwamba unaendelea salama na shughuli za Ujenzi wa Taifa.
Leo nimeleta andiko dogo na fupi najua litawasaidia wengi.Kuna watu waliamua kuanzisha Biashara wakiwa na maono fulani au matarajio fulani.Hata hivyo baada ya kuanzisha biashara kutokana na changamoto fulani wakajikuta ama wanayumba kibiashara au biashara zao zinakuwa DORMANT.Wengi wanapofikia hatua hii hujikuta wakifanya makosa mbalimbali ambayo huathiri sana uelekeo wao wa kibiashara.Andiko hili litakusaidia ili ufahamu nini cha kufanya iwapo kampuni yako iko Dormant.
Nianze kwanza kwa kusema maana ya kampuni Dormant.Kampuni Dormant ni kampuni ambayo imesajiliwa lakinihaifanya shughuli zozote zile za kibiashara,Haiuzi,hainunua,haizingatii matakwa ya kisheria(Compliance).Hali hii huwafanya baadhi ya wamiliki kujikuta wakijuta na kujilaumu kwa kufanya uamuzi wa kuanzisha Kampuni.Hali hutokea kwa sababu nyingi ila kubwa ni kukosa uelewa.
Kampuni ikishasajiliwa ni kama mtoto aliyezaliwa au mmea uliooteshwa.Ni lazima utunzwe ili uweze kukua na kuzaa matunda.Si kweli kwamba ukishaanzisha tu kampuni basi biashara zinaanza kukufuata na PESA zinakuja.Hata kama una mtaji mkubwa bado usimamizi na uendeshaji wa biashara unahitaji uellewe nini cha kufanya na wakati gani.
Kama mmiliki wa kampuni baada ya kusajili kampuni yako kuna shughuli kadhaa za kufanya ambazo ni kama ifuatavyo:
Sasa iwapo kampuni yako ni changa au shughuli zako zinabana basi hizi compliance issue unaweza ku outsourece kwa watoa huduma wengine kwa gharama nafuu zaidi.Gharama za Outsourcing huwa ni ndogo kuliko Penalties ambazo utapigwa kwa kutozingatia Sheria.
2. Shughuli ya Pili ya Kampuni ni Usimamizi wa fedha na Mtaji:Hapa napo watu wengi hukosea.Unapoanzisha Kampuni usichelewe kuweka hili sawa.Kwanza kabisa hakikisha unafungua akaunti za Kampuni Benki.Hakikisha unakuwa na LIPA number za Kampuni yako.Hii hatua ni muhimu maana inakusaidia kuanza kusimamia fedha za kampuni kama fedha za kampuni. Hapa utasimamia mwenyewe
3. Shughuli ya tatu ni utafutaji wa wateja:Sasa hapa inategemea na aina ya Biashara.Ila hapa utapaswa kutembelea watu kupigia watu simu,kutangaza matangazo ya biashara n.k.Hapa napo unaweza ku outsource kwa watoa huduma wengine iwapo muda na uwezo wako wa kufanya ni mdogo.
Sasa inawezekana katika hayo yote ulizembea na kampuni sasa ina mwaka na zaidi na ina penalties TRA,Ina penalties Brela,Haina bank account na wala haina wateja.Usife Moyo Hii ndio sababu ya andiko hili.Wahenga walisema Mtoto akijisaidia kwenye mkono wako hautoukata.So wewe kama mfanyabiashara kampuni yako ikizingua usiikimbie.Ufuatao ni muongozo wa hatua kwa hatua wa nini cha kufanya:
Gharama zetu ni nafuu na za Haraka.

- Shughuli ya kwanza ni Tax and Legal Compliance.Utapaswa kuzingatia kwamba kila mwezi unafanya filing za kodi mbalimbali hasa TRA.kodi za PAYE na SDL ni lazima ufanye filing hata kama Hujaajiri mfanyakazi yeyote.Kodi za Mapato za Kampuni ni lazima ufanye makadirio pamoja na kufanya return hata kama hujafanya Biashara.Return za Brela ni lazima ufanye kila mwaka hata kama umefanya biashara au hujafanya.Ada za leseni ni vibali ni lazima uwe nazo hata kama umefanya au hujafanya biashara.
Sasa iwapo kampuni yako ni changa au shughuli zako zinabana basi hizi compliance issue unaweza ku outsourece kwa watoa huduma wengine kwa gharama nafuu zaidi.Gharama za Outsourcing huwa ni ndogo kuliko Penalties ambazo utapigwa kwa kutozingatia Sheria.
2. Shughuli ya Pili ya Kampuni ni Usimamizi wa fedha na Mtaji:Hapa napo watu wengi hukosea.Unapoanzisha Kampuni usichelewe kuweka hili sawa.Kwanza kabisa hakikisha unafungua akaunti za Kampuni Benki.Hakikisha unakuwa na LIPA number za Kampuni yako.Hii hatua ni muhimu maana inakusaidia kuanza kusimamia fedha za kampuni kama fedha za kampuni. Hapa utasimamia mwenyewe
3. Shughuli ya tatu ni utafutaji wa wateja:Sasa hapa inategemea na aina ya Biashara.Ila hapa utapaswa kutembelea watu kupigia watu simu,kutangaza matangazo ya biashara n.k.Hapa napo unaweza ku outsource kwa watoa huduma wengine iwapo muda na uwezo wako wa kufanya ni mdogo.
Sasa inawezekana katika hayo yote ulizembea na kampuni sasa ina mwaka na zaidi na ina penalties TRA,Ina penalties Brela,Haina bank account na wala haina wateja.Usife Moyo Hii ndio sababu ya andiko hili.Wahenga walisema Mtoto akijisaidia kwenye mkono wako hautoukata.So wewe kama mfanyabiashara kampuni yako ikizingua usiikimbie.Ufuatao ni muongozo wa hatua kwa hatua wa nini cha kufanya:
- Kwanza kabisa fahamu hali halisi ya kampuni yako.Ingia katika mfumo wa Kodi,Mfumo wa Brela na Mfumo wa Leseni ili ufahamu hali ya kampuni yako ikoje kwa maana ya Kiwango cha Damage ambacho kimeshafanyika.Ukishaingi humo hakikisha unastop the Bleed.Kama ni TRA Hakikisha unafanya filings zote za nyuma kisha zile Penalties Ombea Remission TRA wanaelewa watakutaka ULIPE kidogo ila wataelewa hali halisi.Kwa upande wa Brela Fanya hivyo hivyo na kwa Upande wa leseni fanya hivyo hivyo.Usiiogope kampuni yako wala usiogope kudaiwa.Kudaiwa nako ni UTAJIRI.
- Pili angalia hali ya akaunti yako ya kampuni.Jitahidi unapofungua akaunti ya kampunikuchague benki na aina ya akaunti ambayo haina makato makato hasa haya ya mwezi sijui ledger fees etc.Hakikisha una akaunti active
- Tatu sasa hapa ni Pa muhimu.Zama hizi kuna aina nyingi sana za biashara ambazo unaweza fanya kwa njia ya kuingia kwa urahisi.Teknolojia imerahisishwa sana kiasi kwamba unaweza anzisha biashara nyepesi tu ambayo unaweza uza kwa commision huku ukiendelea na maisha.Hii ni muhimu ili kuonesha kwamba Biashara yako ni GOING concern.
- Ukishaweka haya sawa tulia na uwe mwepese wa kutafuta fursa.Jiunge na mfumo wa NEST,Sikiliza fursa mbalimbali hasa za kibiasha na uhudhurie maonesha ya kibiashara na kuitambulisha kampuniyako kwa watu.katika mtandao wako anaweza tokea mtu mwenye fursa inayokufaa na biashara yako ikatoka Shimoni.
Gharama zetu ni nafuu na za Haraka.