Kwani siku zote wanapata kura wapi watashinda tu kwa kishindo CCM ni ileile wezi wa kura, Jasiri haachi asili. Wagombea wote wa upinzani watakatwa watawabakisha wachache kisha hao wachache wataenda kudhurumiwa kwenye sanduku la kura. hakuna uchaguzi Bongo tena kama Zanzibar ambako kuna uchaguzi wa mapema ile uchaguzi wa Mapema tu CCM wanakuwa tayari wameshinda ACT wanapewa viti vyao viwili vya kupozwa, kazi imeisha. Mimi sijisumbui kwenda kupiga kura mwaka huu hata kwa mizinga kwa mazingira haya, nitajipikia ugali wangu tu najilia nasikiliza matokeo, wala hainiumi kwasababu utawafanya nini wababe. Tena safari hii mapema kuna mijigari ya ajabu ajabu ya Mapolisi fanya fyoko kama hajakutoa utumbo. Wanao jidai kupiga piga vikelele ni CHADEMA wala hata nao hawana kitu, Lisu na heche wake watashikwa kama kuku wenye mdondo kwio, kwio, kwio, kwio hao wanaenda kufanywa Mboga, hii mikiki ya safari hii si kitoto.