Pre GE2025 Je, Ugumu wa Maisha na Ukosefu wa ajira kwa vijana inawezekana kikawa Chanzo cha CCM kushindwa Uchaguzi ujao?

Pre GE2025 Je, Ugumu wa Maisha na Ukosefu wa ajira kwa vijana inawezekana kikawa Chanzo cha CCM kushindwa Uchaguzi ujao?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Sio kwa bongo! Haohao wakikusanywa shamba la bibi ni jokate wakapewa buku 5 na T-shirt kesho yake wanaimba mama kawapigia mwingi! Elimu yetu inahitaji mabadiliko makubwa ili iwape vijana ufahamu kwanza
 
Asilimia kubwa sana ya Watu wana MAISHA MAGUMU

Asilimia kubwa ya vijana hawana AJIRA

Lazima CCM watashindwa au kuwa wa mwisho au kushika Mkia

Je, CCM watapata kura wapi wakati asilimia kubwa ya watu wana hali ngumu?
Ni endapo wanajitambua, vinginevyo ccm wataendelea kushinda
 
Kwani siku zote wanapata kura wapi watashinda tu kwa kishindo CCM ni ileile wezi wa kura, Jasiri haachi asili. Wagombea wote wa upinzani watakatwa watawabakisha wachache kisha hao wachache wataenda kudhurumiwa kwenye sanduku la kura. hakuna uchaguzi Bongo tena kama Zanzibar ambako kuna uchaguzi wa mapema ile uchaguzi wa Mapema tu CCM wanakuwa tayari wameshinda ACT wanapewa viti vyao viwili vya kupozwa, kazi imeisha. Mimi sijisumbui kwenda kupiga kura mwaka huu hata kwa mizinga kwa mazingira haya, nitajipikia ugali wangu tu najilia nasikiliza matokeo, wala hainiumi kwasababu utawafanya nini wababe. Tena safari hii mapema kuna mijigari ya ajabu ajabu ya Mapolisi fanya fyoko kama hajakutoa utumbo. Wanao jidai kupiga piga vikelele ni CHADEMA wala hata nao hawana kitu, Lisu na heche wake watashikwa kama kuku wenye mdondo kwio, kwio, kwio, kwio hao wanaenda kufanywa Mboga, hii mikiki ya safari hii si kitoto.
Duh!
 
Sio kwa bongo! Haohao wakikusanywa shamba la bibi ni jokate wakapewa buku 5 na T-shirt kesho yake wanaimba mama kawapigia mwingi! Elimu yetu inahitaji mabadiliko makubwa ili iwape vijana ufahamu kwanza
🤣
 
Back
Top Bottom