Ukikopa unaweza kukimbia mkopo wako i.e. kuacha kulipa (huenda hata kushikwa kwako kukawa shida) ndio maana Taasisi kubwa huwa zina-writeoff baadhi ya madeni kama Bad Debt na kuyauza kwa wengine (hao wanaonunua huwa wana muda zaidi wa kula sahani moja na wewe, vitisho na simu za hapa na pale pamoja na usumbufu)
Lakini issue ya maana kabisa ni kwamba ulipaji wako ukiwa mbaya CREDIT RATING yako inashuka na kuwa mbovu hivyo hata kama una mkopo wa SONGESHA na haujalipa siku ukienda CRDB watavuta mkeka wako wa Madeni kuona kwamba wewe sio MLIPAJI hivyo either kukosa Mkopo au kushauriwa kalipe kwanza kabla hatujakufikiria (NIDA imesababisha details zako zipatikane popote) Ingawa ni vigumu Taasisi fulani ilazimishe kuchukua pesa zako / kuzikata bila kukutaarifu au idhini yako