Msamaha wa Kodi hua hauami isipokua kwa wale wenye sifa zinazofanana.
Kwakua wewe na Taasisi hamna sifa zinazofanana, lazima utalipia kodi ya Kuingiza gari, ila kodi hizo zita base baada ya hesabu ya Depreciation tangia gari imeingia.
Mfano: gari imeingia miaka 10 iliyopita na thamani yake ilikua 50M na Gari ilipata msamaha(inategemea na aina gani ya msamaha, maana ipo mingi), TRA watafanya hesabu za depreciation kwa miaka hiyo 10, na kupata thamani ya gari baada ya miaka hiyo, labda 10M, kodi zote zilizosamehewa zitalipwa kwenye hicho kiwango.
Mtu/Taasisi anaweza kusamehewe kodi zote. Au import duty(watu wa serikali) au VAT kwa baadhi ya project na kuendelea.