Je Ukinunua gari la Taasisi lililosamehewa kodi utapaswa kulipa?

Je Ukinunua gari la Taasisi lililosamehewa kodi utapaswa kulipa?

Bautaweza kubadili jina, unless ulipie kodi ndio Transfer inakubali hii iliwah kunisumbua sana, sitasahau
Kulipa ni lazima ndio maana nilikuwa nauliza nijue kama kiwango kinapungua ama vipi
 
Wadau,
Naomba mwenye ufahamu anisaidie,nikitaka kununua gari ambalo lilisamehewa kodi ya serikali(Tax exempted) linalomilikiwa na taasisi kidini,Je ni nitapaswa kulipia ile gharama ya kodi iliyosamehewa au sitalipia?

Na kama lina miaka 10 nyuma tangu taasisi hio iagize gari hilo na nitatakiwa kulipia kodi itakuwa ni ileile,itapanda au itashuka?

Naombeni ufafanuzi.
habari
kama umenunua gari lolote lenye exemption ni lazma ulilipie kodi japo kodi hyo inaweza kupungua kutokana na uchakavu wa chombo husika.

mfano kama gari ya 2007 haiwez kuwa sawa na gari ya 2002 hivyo lazma kodi iwe tofauti kama vile ununuavyo gar japan
 
Msamaha wa Kodi hua hauami isipokua kwa wale wenye sifa zinazofanana.

Kwakua wewe na Taasisi hamna sifa zinazofanana, lazima utalipia kodi ya Kuingiza gari, ila kodi hizo zita base baada ya hesabu ya Depreciation tangia gari imeingia.

Mfano: gari imeingia miaka 10 iliyopita na thamani yake ilikua 50M na Gari ilipata msamaha(inategemea na aina gani ya msamaha, maana ipo mingi), TRA watafanya hesabu za depreciation kwa miaka hiyo 10, na kupata thamani ya gari baada ya miaka hiyo, labda 10M, kodi zote zilizosamehewa zitalipwa kwenye hicho kiwango.

Mtu/Taasisi anaweza kusamehewe kodi zote. Au import duty(watu wa serikali) au VAT kwa baadhi ya project na kuendelea.

Haya maelezo sahihi ya kufata mkuu.
Kisha chukua documents za gari nenda TRA kama uko dar nenda posta jengo la bandari floor ya saba utapigiwa hesabu zako vizuri kabisaa
 
Back
Top Bottom