Je Ukinunua gari la Taasisi lililosamehewa kodi utapaswa kulipa?

Aisee mbona balaa sasa,kama walisamehe kwanini sasa ulipie?
Wanasamehewa kwa ajili ya kutoa huduma, umiliki unapohama itakulazimu ulipie may be utumie hivyo hivyo bila kubadili jina la taasisi
 
Bautaweza kubadili jina, unless ulipie kodi ndio Transfer inakubali hii iliwah kunisumbua sana, sitasahau
Kulipa ni lazima ndio maana nilikuwa nauliza nijue kama kiwango kinapungua ama vipi
 
habari
kama umenunua gari lolote lenye exemption ni lazma ulilipie kodi japo kodi hyo inaweza kupungua kutokana na uchakavu wa chombo husika.

mfano kama gari ya 2007 haiwez kuwa sawa na gari ya 2002 hivyo lazma kodi iwe tofauti kama vile ununuavyo gar japan
 

Haya maelezo sahihi ya kufata mkuu.
Kisha chukua documents za gari nenda TRA kama uko dar nenda posta jengo la bandari floor ya saba utapigiwa hesabu zako vizuri kabisaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…