Je, ukioa au kuolewa mali zako zinakua za mwenza wako pia?

Je, ukioa au kuolewa mali zako zinakua za mwenza wako pia?

Atukuzwaye

Senior Member
Joined
Oct 5, 2026
Posts
191
Reaction score
250
Sasa wakuu, hili suala kisheria kumbe liko hivi;


Kifungu cha 58 cha sheria ya ndoa, sura ya 29, kinaeleza kuwa ndoa haibadilishi moja kwa moja umiliki wa mali za mume au mke.

Maana yake ni kwamba, mali uliyokuwa nayo kabla ya ndoa haibadiliki moja kwa moja kuwa mali ya mwenza wako kwa sababu tu mmeoana. Aidha, hata ukiwa ndani ya ndoa, una haki ya kununua, kumiliki na kuuza mali zako binafsi, kwa kuzingatia sheria.

LAKINI KUNA TOFAUTI KWA NYUMBA YA NDOA AU NYUMBA YA KUKAA FAMILIA (MATRIMONIAL HOME)ambapo kwa mujibu wa Kifungu cha 59, hata kama nyumba ya ndoa au nyumba ya kukaa familia (matrimonial home) imeandikwa kwa jina lako pekee, huwezi kuiuza, kuiweka rehani au kuhamisha umiliki wake bila ridhaa ya mwenza wako wakati ndoa inaendelea.

JE, HII INAMAANISHA KILA MWANANDOA ANA HAKI YA 50/50? Jibu ni hapana! kutokana na Kifungu cha 59 ambacho kinalinda nyumba ya ndoa au nyumba ya kukaa familia (matrimonial home) dhidi ya kuuzwa au kuhamishwa bila ridhaa ya mwenza, lakini hakimaanishi kuwa kila mwanandoa ana haki ya kupata asilimia 50 ya nyumba hiyo ndoa inapovunjika.

Aidha, Kwa mujibu wa Kifungu cha 114, mgawanyo wa mali za ndoa huzingatia mchango wa kila mwanandoa katika upatikanaji wa mali hizo. Mchango unaweza kuwa wa kifedha au usio wa kifedha, ikiwemo kazi za nyumbani na malezi ya familia.

KUMBUKA: Kulindwa kwa nyumba ya ndoa siyo sawa na kumiliki nusu ya nyumba hiyo. Haki ya mgao hutegemea ushahidi wa mchango na vigezo vingine vya kisheria.
 
Back
Top Bottom