Mm ni mwanafunzi wa chuo mwaka wa tatu
Kabla ya biashara ya sasa nimewah fanya biashara kadhaa huku nasoma toka o level kifupi nimejisomesha mimi mwwnyewe kwani sina wazazi mpka sasa nakaribia kumaliza chuo
Kufupisha story biashara ya nyuma kabla ya hii ni kuwa nilikua nauza makande yes makande haya haya ya mahindi na maharage
Kifupi najua sana kuyapika yan sana na nikipika nilikua nasifiwa sanaa so nikaona ni fursa kwani watu weng hasa dar wamezoea kula ugali au wali tu kwa mama lishe
Nikiwa mwaka wa pili chuo nilianza na mtaji wa elfu tano tu yan nilinunua mahindi nusu na robo maharage nusu sukar robo nazi moja karoti na hoho na mkaa wa buku
Nikawa naroweka mahindi na maharage usiku mzima ili yawah kuiva halafu nayaunga vizur sana kisha nilikua na makontena yan yale mabakuli ya mfuniko matatu nikaazima mengine matano nikawa napaki mule halafu sa sita mchana naenda kuuza kwenye vujiwe vya bodaboda kwa bei ya 1500 faida unapata 7000 baada ya kutoa mtaji wako na nikaendelea kukuza mpaka kuuza kontena 30 kwa siku na faida unapata 30 hiyohiyo baada ya kutoa mtaji
Kuhusu namna nilivokua nagawa muda wa masomo na biashara ni jambo lingine ambalo nitaeleza wakat mwingine ila haikua rahisi
Kwa sasa nimefungua kampuni nasambaza house maids yan house girls