The Assassin
JF-Expert Member
- Oct 30, 2018
- 4,942
- 20,077
Biblia inasema Mungu anajua kila kitu, all knowing, alpha na Omega, mwanzo na mwisho, mjuzi wa vyote.
Sasa nakua najiuliza, kabla ya kuomba ama wakati unaanza kuomba, je mungu anakua anajua in advance unachotaka kuomba ama anakua hajui hadi uombe kwanza?
Na kama anakua anajua utakachokiomba, je maombi yako tayabadilisha maamuzi yake ambayo tayari anakua ameshayafanya baada ya kua ameshajua unachotaka kuomba.
Na je kama anakua anajua in advance, kwa hiyo ukiwa unaomba anakua anakuchora tu 'anakuinjoi' wewe unaomba weeeee hadi machozi yanatoka huku yeye alishaamua ama ana maamuzi yake mkononi.
Swali la pili, kama hajui unachoenda kumuomba, maana yake hajui kila kitu ama pia unapoenda kumuomba unaenda kumshtukiza na maombi ama mahitaji yako ambayo yeye alikua hayajui kabla hivyo atahitaji muda kidogo kuchakata na kupata majibu sahihi ya maombi yako.
Na kama ndio hivyo, leo ukaomba, kesho ama kila siku, mungu atahutaji muda mrefu sana kujibu ombi lako moja moja na hivyo unaweza kufa hujajibiwa hata ombi moja ama leo hii ndio ukapokea majibu ya maombi yako ya mwaka 1980.
Watu wa dini naomba kufahamishwa.