binti kiziwi
JF-Expert Member
- Aug 4, 2014
- 16,966
- 47,296
Hapana, unless waniruhusu nikawahoji wao, sio wao wanihoji mimi.
Hapana hata kidogo huu unaofanyika ni uduwanzi na mkakati wa kujisafisha ndani na nje ya nchi! Hakuna uwajibikaji wa kweli unaofanyika hapaUnawezaje kuua halafu ujipeleleze na kujihukumu mwenyewe?.
La kujiuliza, je watakaotoa Ushahidi wa Jinai utatumika na vyombo vya Sheria kuleta haki stahiki. Au ni pima maji ya uzito wa Ushahidi utaotolewa huko ICC 🥺Tume ilivyoundwa tu kwa taswira ya muhusika, ni chombo cha kushusha joto na hasira za wananzengo.
Mbili, kupata hoja za rejea na hatua kuelekea kinachoitwa maandalizi ya Katiba mpya
29 Oktoba tayari imeitwa vurugu, watu wakafa (sio mauwaji). Tume ije na majibu ya hayo kutojirudia. Si ajabu na tusistaajabu, zikapendekezwa baadhi ya Sheria kurekebishwa hapa na pale. Hatua za uwajibishwaji akaachiwa mwenyewe aliyeunda Tume
La kujiuliza, je watakaotoa Ushahidi wa Jinai utatumika na vyombo vya Sheria kuleta haki stahiki. Au ni pima maji ya uzito wa Ushahidi utaotolewa huko ICC
Tume itatoa taarifa fupi ya muhutasari wa Ripoti yao wakati wa kuwasilisha kwa mamlaka iliyowateua. Je taarifa ya kina itawekwa wazi kwa wote ijadiliwe au funika mwanaharamu kombe apite...
Wavurunde yote wawaache watu waseme na wakosoe kwa uwazi.
Mambo ya woga na watu kupotea ni shimo kubwa tunajichimbia sote makapuku na vigogo.
Tuendelee Kuvuna Gharama za Upumbavu unapotawala
Wanachunguza nini wakati ukweli unajulikana kwamba wananchi walidhulumiwa haki yao ya kuchagua katika uchaguzi mkuu 2025 baada ya mgombea wao Tundu Antpas Lissu kukamatwa na kufunguliwa mashtaka ya uongo ya uhaini ili asigombee Urais.