Marekani, Ufaransa na Ujerumani ziliamua kutuma kifurushi kingine cha silaha nchini Ukraine.
Tusichukulie sentensi hili kirahisi maana wakati huu tunaweza kuzungumzia kuanzishwa kwa mifumo ya kubadilisha mchezo(game-changing systems).
- magari 50 ya mapigano ya Bradley yaliyotengenezwa Marekani (IFV),
- IFV 40 za Ujerumani “Marder”,
- na idadi isiyojulikana ya AMX-10 RC ya Ufaransa.
View attachment 2472547
Pichani ni German Armored Infantry (Panzergrenadiere) wakiwa na gari la kivita la kijeshi la "Marder".
Na hii labda ni mwanzo tu, kuna mengi zaidi yajayo. Mara tu silaha hizi zitakapokuwa kwenye uwanja wa vita, Vikosi vya Wanajeshi wa Ukraine vitaweza kufanya kile kinachoitwa operesheni za vita vya pamoja vya silaha (combined arms warfare operations), kwa mara ya kwanza kabisa:
Mifumo yote kuu ya silaha unayohitaji kwa shambulio la kivita lenye ufanisi sasa inapatikana kwao.
- Mizinga (T 72 nk. pamoja na AMX 10)
- IFVs (Marders na Bradleys)
- Mifumo ya Kupambana na Anga (Gepards ya Ujerumani)
- Artillery (Panzerhaubitze 2000 na wengine)
Bila Bradleys na Marders, askari wa miguu wa Ukraine hawakuweza kufuata mizinga yao. Magari yao ni ama yalikuwa na ngao pamoja na silaha nyepesi sana kutumiwa kwenye uwanja wa vita moto (kwa mfano, M113) au hawakuweza kuendana na mizinga katika maeneo yenye ardhi nzito (Boxers, na magari mengine yote ya magurudumu).
Sasa kila gari ambalo Jeshi la Ukraine linahitaji kufanya operesheni ya kivita ya pamoja "kwa ufanisi mkubwa" lina ngao na silaha nzito . Hii ina maana wanaweza kufanya kazi pamoja.
Tunaweza kutarajia operesheni kuu za mapigano zinazohusisha magari haya mwishoni mwa Machi au Aprili. Kulingana na kile tumeona hadi sasa kwenye uwanja wa vita, tunaweza kutarajia opresheni hizi kuwa na mafanikio makubwa.
Na hakuna chochote ambacho Warusi wanaweza kufanya juu yake. Hawana njia za kukabiliana na aina hii ya mashambulizi. Wanachoweza kufanya ni kutumaini kwamba Wamarekani na Wajerumani hawataamua kutoa mizinga yao ya kisasa ya Vita Kuu (Abrams na Leopard 2) kwa Ukraine. Hili likitokea, nisingependa kuwa mmoja wa wanajeshi wa urusi waliopo Donetsk au Crimea.
Kujibu swali: Ukraine haipotezi vita hii. Ulimwengu uko upande wao na kwa pamoja, watashinda.
NB: kama urusi ingeshinda vita hii, ungekuwa mwanzo wa WW III, Anacopy exactly alichofanya Adolf Hitler.