Mkuu Henoko hakuwa muisrael.... Kibiblia Henoko ni mtu wa nane baada ya Adam ila waisrael wameanza kutajwa miaka zaidi ya 2000 toka Enoko Afe so hakuna namna anaweza kuwa Muisrael.
Sababu ya Henoko kuwa mweusi ni kutokana na hicho kitabu kutambuliwa na kanisa la Ethiopia Tawahedo Orthodox ambalo ndio kanisa pekee linalotumia kitabu cha Henoko kama part ya Biblia kamili hivyo roots zake za Ethiopia ndio zinafanya Henoko wamchore akiwa mweusi.
Sababu ya Pili kitabu cha Henoko kinamkariri Henoko mwenyewe akielezea uzao wa Nuhu ambapo mjukuu wake yake alipozaa mtoto MWEUPE peee yaani akapigwa na butwaa akadhani ni mtoto wa malaika (Mnefili) na sio wake hivyo akakimbia hadi kwa Methuselah kumueleza kisa hiki na ikawa utata sana hadi alipokuja kuamini ni mwanae so wengi wakatafsiri kwamba hapa ndio uzao wa wazungu ulipoanzia hivyo kuanzia methuselah mpaka Henoko hadi Adam walikuwa black watupu kwa sababu hii ndio maana picha nyingi za Henoko wanamuweka kama black.
NB: Mkuu napendaga mada zako sana za wanefili natarajia siku moja uje na mada kuhusu wanefili waliishia wapi na kama wapo leo ni wapi.
Cc
theriogenology