Je, Ukubwa wa Nchi yetu Tanzania ni kikwazo katika kuwafikia na kuwahudumia wananchi?

Je, Ukubwa wa Nchi yetu Tanzania ni kikwazo katika kuwafikia na kuwahudumia wananchi?

Tatizo ni ugatuzi wa madaraka. Huwezikupata maendeleo kama Kodi ya uwekezaji inalipwa makao makuu. Mamlaka za mikoa hazina mapato,haziwezi kujenga hata km 100 za lami. Raslimali hazitumiki ipasavyo maana usimamizi na msimamizi Yuko serikali kuu. Serikali za mikoa zingeachwa zikusanye Kodi,zianzishe na kukusanya Kodi za uwekezaji.TRA wapewe gawio, mikoa kama geita ungekua mkoa namba 2 kimaendeleo baada ya Dar.
Sahihi
 
Kikwazo ni chadema na vibaraka.
Mkuu kivipi? To be fair fafanua vizuri! Uliowataja hapo juu hawakusanyi kodi, hawaandai bajeti ya serikali na hawapo Bungeni kwa sasa. Ni miaka 60 sasa hawajawahi kushika dola wala serikali, wanakuwaje kikwazo?
 
Kumanage population kubwa hili ichochee maendeleo ni kazi kubwa inayoitaji miaka mingi sana .
Kwa akili ya haraka haraka unaweza ukasema population kubwa ndio yenye kuchangia Kodi nyingi hivo maendeleo yatachochewa haraka sana .
Lakini kwa jinsi nionavyo population kubwa ndiyo yenye kutumia Kodi nyingi na kuchochea umaskini wa haraka sana, nawasikia wakubwa wangu wanasema enzi za Nyerere Kuna favour nyingi walikuwa wakizipata Sasa awazipati, kwenye elimu uko, mahospitalini uko Sasa akuna Nini tafsiri yake kipindi kile ilikuwa ni raisi kufanya yote hayo kulingana na hile population.
Saizi ni kazi kubwa sana mfano hii population ya zaidi ya mil 61 tafuta takwimu ujue ni wangapi kweli wanalipa Kodi kwa ajili ya maendeleo ya nchi Yao utachoka na hapo ndo utajua panya wengi awachimbi mshimo na hii population kubwa ni mzingo inanyonya watu wachache na hivyo tutachelewa kufika malengo .
Nb; Ni mtizamo wangu
 
Hii siyo excuse yenye nguvu. Kuna nchi kubwa kuliko yetu, na zina idadi kubwa ya watu kuliko sisi, lakini zimeendelea kuliko sisi.
China wanapiga hatua kubwa za kimaendeleo kuliko sisi, pamoja na ukubwa wa eneo na idadi kubwa ya watu.
Kuwa na idadi kubwa ya watu ni opportunity ya kuwa na idadi kubwa ya consumers, na hivyo kuwa na idadi kubwa ya walipa kodi. Kinachotakiwa ni kujenga uchumi imara utakawahusisha hao watu wengi kujipatia mapato na hatimaye kutumia sehemu ya income zao ktk kuendeleza huo uchumi kwa kununua vitu na kulipa kodi.
Ukubwa wa nchi au idadi kubwa ya watu ni visingizio tu. Tatizo letu kubwa liko kwenye UONGOZI na policies tunazofuata.

Mkuu nakuunga mkono! 👍👍
 
Tatizo sio ukubwa, tatizo ni viongozi kuwa wabinafsi na wabadhilifu wa mali za umma.
Kila Mwaka CAG anatoa taarifa yake huku akifichua ubadhirifu mkubwa sana wa fedha za umma, fedha ambazo kama zisingefanyiwa ufisadi zilinufaisha taifa kwa namna nzuri na kupunguza au kuondoa kabisa kero mbalimbali ndani ya taifa hili
 
Salaam, Shalom!!

Nimelazimika kupandisha mada hii baada ya kusoma comment ya mdau wa JF aitwaye Voice of Tanzania alipokuwa akichangia mada katika thread isomekayo,

Ni Lini Serikali ya CCM itanunua laptop Kwa Kila mwanafunzi kuanzia shule za kata?

Nilipotoa mfano wa Nchi ndogo ya Rwanda kuweza kuhakikisha wanafunzi wa shule za msingi wanapata laptop za kusaidia kujifunza darasani Ili kuendana na Kasi ya mabadiliko yanayotokea katika mfumo wa Elimu na teknolojia ya mawasiliano, alijibu kuwa, jambo Hilo limewezekana sababu Nchi ya Rwanda ni ndogo!!

Nilipohoji, ikiwa Udogo wa Nchi ya Rwanda ni fursa kupeleka maendeleo na mabadiliko ya kimfumo wa ELIMU nchini mwao, ikiwa nasi tutaigawa Nchi yetu vipande vidogo vidogo vyenye kulingana na ukubwa wa Rwanda, tutaweza kuwafikia na kuwapita kimaendeleo katika sekta mbalimbali, Elimu ikiwamo?


Pia, nimewahi kumsikia kiongozi mmoja mkubwa akijenga HOJA kama ya ndugu Voice of Tanzania kwamba,

Mwalimu Nyerere katika utawala wake, aliweza Kutoa chakula mashuleni na huduma nyingine kirahisi sababu tulikuwa idadi ndogo kulinganisha na sasa tumeongezeka sana.

Maswali ya kujiuliza Watanzania,

1. Je, ni Kweli ukubwa wa Nchi yetu, ni kikwazo Kwa Serikali yetu kushindwa kupeleka maendeleo Kwa haraka?

2. Je, ni Kweli wingi wetu wananchi walipakodi ni kikwazo kikuu ya Serikali yetu kushindwa kutuhudumia wananchi?

Karibuni 🙏.
Somehow but with brain,Nchi hii ni ndogo sana
 
Tatizo si ukubwa wa nchi, wala idadi ya watu...hivi vimekuwa visingizio vya wachache wenye uvivu wa kufikiri. Tatizo letu ni kurundika kila kitu, kila jambo, kila makusanyo, nk. kwa serikali kuu(mfuko mkuu/hazina). Na hiki ndiyo kinatoa mwanya kwa wapigaji. Kwanza nchi ingegawanywa katika kanda za kiuchumi (Economic Zone); na siyo hizi za kisiasa. Kwa rasilimali zilizopo hapa nchini, kila kanda (angalau ziwe 5) inazo raslimali za kutosha kuendeleza maeneo hayo, kuanzia kilimo, mifugo, uvuvi, madini, utalii, nk. Mapato yote yakusanywe katika kanda na kuhudumia maendeleo ya kanda husika. Asilimia kidogo sana ya makusanyo ipelekwe hazina kuu kwa shughuli za utawala..hapo tutapunguza upigaji. Na huku kwenye kanda viongozi wote wachaguliwe na wananchi na kudhibitiwa na wananchi wenyewe. HEBU TUJARIBU MUUNDO HUU TOFAUTI, TUONE KAMA KUNA SHULE ITAKOSA MADAWATI AU MATUNDU YA VYOO!
 
Tuangazie katika ngazi ya familia!!

Ikiwa kuzaa sana Kwa maskini, ni sababu kuu ya Umaskini wa Watanzania wengi wa KIPATO Cha chini, sasa kwanini matajiri pia hawana watoto wengi pamoja na kumiliki ukwasi wa kutosha kuwahudumia?
 
Back
Top Bottom