SahihiTatizo ni ugatuzi wa madaraka. Huwezikupata maendeleo kama Kodi ya uwekezaji inalipwa makao makuu. Mamlaka za mikoa hazina mapato,haziwezi kujenga hata km 100 za lami. Raslimali hazitumiki ipasavyo maana usimamizi na msimamizi Yuko serikali kuu. Serikali za mikoa zingeachwa zikusanye Kodi,zianzishe na kukusanya Kodi za uwekezaji.TRA wapewe gawio, mikoa kama geita ungekua mkoa namba 2 kimaendeleo baada ya Dar.
Mkuu kivipi? To be fair fafanua vizuri! Uliowataja hapo juu hawakusanyi kodi, hawaandai bajeti ya serikali na hawapo Bungeni kwa sasa. Ni miaka 60 sasa hawajawahi kushika dola wala serikali, wanakuwaje kikwazo?Kikwazo ni chadema na vibaraka.
Hii siyo excuse yenye nguvu. Kuna nchi kubwa kuliko yetu, na zina idadi kubwa ya watu kuliko sisi, lakini zimeendelea kuliko sisi.
China wanapiga hatua kubwa za kimaendeleo kuliko sisi, pamoja na ukubwa wa eneo na idadi kubwa ya watu.
Kuwa na idadi kubwa ya watu ni opportunity ya kuwa na idadi kubwa ya consumers, na hivyo kuwa na idadi kubwa ya walipa kodi. Kinachotakiwa ni kujenga uchumi imara utakawahusisha hao watu wengi kujipatia mapato na hatimaye kutumia sehemu ya income zao ktk kuendeleza huo uchumi kwa kununua vitu na kulipa kodi.
Ukubwa wa nchi au idadi kubwa ya watu ni visingizio tu. Tatizo letu kubwa liko kwenye UONGOZI na policies tunazofuata.
Somehow but with brain,Nchi hii ni ndogo sanaSalaam, Shalom!!
Nimelazimika kupandisha mada hii baada ya kusoma comment ya mdau wa JF aitwaye Voice of Tanzania alipokuwa akichangia mada katika thread isomekayo,
Ni Lini Serikali ya CCM itanunua laptop Kwa Kila mwanafunzi kuanzia shule za kata?
Nilipotoa mfano wa Nchi ndogo ya Rwanda kuweza kuhakikisha wanafunzi wa shule za msingi wanapata laptop za kusaidia kujifunza darasani Ili kuendana na Kasi ya mabadiliko yanayotokea katika mfumo wa Elimu na teknolojia ya mawasiliano, alijibu kuwa, jambo Hilo limewezekana sababu Nchi ya Rwanda ni ndogo!!
Nilipohoji, ikiwa Udogo wa Nchi ya Rwanda ni fursa kupeleka maendeleo na mabadiliko ya kimfumo wa ELIMU nchini mwao, ikiwa nasi tutaigawa Nchi yetu vipande vidogo vidogo vyenye kulingana na ukubwa wa Rwanda, tutaweza kuwafikia na kuwapita kimaendeleo katika sekta mbalimbali, Elimu ikiwamo?
Pia, nimewahi kumsikia kiongozi mmoja mkubwa akijenga HOJA kama ya ndugu Voice of Tanzania kwamba,
Mwalimu Nyerere katika utawala wake, aliweza Kutoa chakula mashuleni na huduma nyingine kirahisi sababu tulikuwa idadi ndogo kulinganisha na sasa tumeongezeka sana.
Maswali ya kujiuliza Watanzania,
1. Je, ni Kweli ukubwa wa Nchi yetu, ni kikwazo Kwa Serikali yetu kushindwa kupeleka maendeleo Kwa haraka?
2. Je, ni Kweli wingi wetu wananchi walipakodi ni kikwazo kikuu ya Serikali yetu kushindwa kutuhudumia wananchi?
Karibuni π.
Somehow nn!!Somehow but with brain,Nchi hii ni ndogo sana
Jamii isiyokuwa na uadilifu haiwezi kuwa na maendeleoSomehow nn!!
Tatizo Hasa Unadhani ni nini?