Je, ulimwengu una mwisho? Bonus question: What is nothing?

Siku tukiweza kutoka nje ya kifungo fikra cha dini tutakuwa tumefika karibu na kilele cha ufahamu wetu
 
Ili kitu kiwe ukweli lazima uwepo uthibitisho na ushahidi wa kitu hicho.

Ili tukifanya uhakiki, tupate uthibitisho wa kitu hicho.

Sasa wewe Thibitisha uwepo wa Mungu na si imani yako tu.
Narejea maelezo yangu ya awali kuwa ushahidi wa uwepo wa Mungu kwa mujibu wangu ni imani inayokuwa backed na mazingira ya kidunia tuliyomo na yale ambayo wanadamu wameweza kuchunguza na kubaini.

Whereas wewe unataka kum comfine Mungu kwenye scientific methods ili uweze kubaini uwepo wake...utakwama kwani Mungu ni beyond hizo methods.

Imani haiwezi kuthibitishwa kwa kanuni za kisanyansi..ila ni halisi na ipo. Ili uweze kumthibitisha Mungu kiimani ni lazima wewe mwenyewe upitie uzoefu fulani utakaomfunua huyo Mungu kwako.

Otherwise hatutafika mwisho kwenye hii debate. Ni kama wewe usivyokuwa na uthibitisho wa kutokuwepo kwa Mungu.
 
Vyote vyenye mwanzo vinamwisho
Hata maumbile yanaonyesha hili
Maisha ya kila siku ynaonyesha ilo pia
 
Narejea maelezo yangu ya awali kuwa ushahidi wa uwepo wa Mungu kwa mujibu wangu ni imani inayokuwa backed na mazingira ya kidunia tuliyomo na yale ambayo wanadamu wameweza kuchunguza na kubaini.
Imani si ushahidi.

Mimi nikikwambia kwamba nina imani kwamba kuna Dragons 🐉 watemao moto 🔥 midomoni mwao bila kukuthibitishia kwa kukuonyesha hao Dragons wenyewe walivyo,

Je utanikubalia tu hivyo hivyo?
Whereas wewe unataka kum comfine Mungu kwenye scientific methods ili uweze kubaini uwepo wake...utakwama kwani Mungu ni beyond hizo methods.
Ulijuaje Mungu ni beyond hizo methods?

Ulifanya Utafiti gani ukagundua kwamba kuna Mungu, Kisha ukagundua kwamba Mungu huyo yupo beyond scientific methods?
Imani haiwezi kuthibitishwa kwa kanuni za kisanyansi..ila ni halisi na ipo. Ili uweze kumthibitisha Mungu kiimani ni lazima wewe mwenyewe upitie uzoefu fulani utakaomfunua huyo Mungu kwako.
Msingi wa imani ni kutokuwa na uhakika.

Na unaweza kuamini hata uongo, kwa vile ni imani tu.

Ili kitu kiwe ukweli lazima pawepo ushahidi, uhakiki na uthibitisho.

Sasa wewe unathibitisha vipi kwamba huyo Mungu yupo kweli na si imani yako ya kufikirika tu?
Otherwise hatutafika mwisho kwenye hii debate. Ni kama wewe usivyokuwa na uthibitisho wa kutokuwepo kwa Mungu.
Madai ya kuwepo Mungu yametoka kwenu nyie waamini Mungu.

Ninyi ndio mnadai kuna Mungu, Hivyo nyie ndio mnapaswa kuthibitisha madai yenu ya uwepo wa huyo Mungu mnayedai yupo.

Ukishindwa kuthibitisha uwepo wa huyo Mungu unayedai yupo, Ni kwamba madai yako ya uwepo wa Mungu ni madai ya UONGO. Na huyo Mungu unayedai yupo, Hayupo.

Una elewa?
 
Unaposema kuwa huyo Mungu hayupo ni kwa vile unatumia akili yako kwa kuangalia udhaifu wa sababu za uwepo wake bado unakuwa haujathibitisha kutokuwepo kwake.

Hebu thibitisha kuwa huyo Mungu hayupo with vivid reasons.
 
Siwezi kuthibitisha uwepo wa kitu ambacho hakipo.

Kitu kisichokuwepo hakithibitishiki kwa namna yoyote ile.

Kwa sababu hakipo kwa namna yoyote ile ya kuthibitishika kipo. Hivyo hakipo.

Wewe unayedai Mungu yupo ndio uthibitishe yupoje?

Ukishindwa kuthibitisha Mungu yupo ni kwamba Mungu hayupo.

Na madai yako ya kwamba kuna Mungu ni madai ya uongo.
 
Hapo kwenye world weka Earth
 
Umetumia neno mujarabu OBSERVABLE, hii inamaanisha mwisho tunaoufahamu ni pale technology iliyopo duniani kwa sasa uwezo wake wa kuona/kukadiria unapoishia.
Ukweli utabaki kuwa UNIVERSE haina mwisho, hakuna NOTHING. Bahati mbaya uliyona(I mean inayokukosesha majibu) ni kuwahi kuzaliwa, kwa watakaozaliwa maybe 20 or rather 100 centuries from now majibu ya maswali yako yatakuwa ni kitu obvious kwao japo nao watakuwa na maswali beyond their knowledge/technology. Maybe colonisation au slavery itarudi kwa viumbe kutoka galaxies tofauti kuvamiana, kupigana na kutekana. Nobody knows. Hata aina ya viumbe(intelligent creatures) wa 'huko kwingine' hatuna hata idea wakoje(I mean maumbile kama idadi ya miguu, mikono, macho nk) na kama wakiingiliana na binadamu watazaa kitu gani lakini hivyo ni vitu ambavyo mbeleni vitatokea na bahati mbaya hatutakuwepo kushuhudia.
 
Kwahiyo ulimwengu na Mungu ni kitu kilekile?
 
Mwenye tafiti binafsi aweke hapa na sio kuleta habari za watu wengine toka kwenye makabrasha yao.
 
maswal yako ni mazur na ni afya ya akili
sasa ndio ukisikia tunayoyajua katika elimu yake mungu ni sawa na tone au kipande cha ukucha.kwenye bahari. mungu ana elimu bwana
 
Ulimwengu hauna mwanzo wala mwisho.

Ulimwengu ulikuwepo, upo na utaendelea kuwepo milele.
Natamani kukuamini, Lakini hiyo ingemake sense kama ulimwengu ungekuwa static.
ila unabadilika, Tena haubadiliki randomly tu ila Kuna sense ya direction kwenye hayo mabadiliko.
Yani Jana ni tofauti na Leo na Leo ni tofauti na kesho.
Miaka billion 10 iliyopita hata dunia haikuwepo.
Sasa kama Kuna mabadiliko ya kutoka sehemu moja kwenda nyingine hiyo ni kama inaashiria kuwa Kuna sehemu ulimwengu ulipotoka (mwanzo) na Kuna sehemu unaenda (mwisho)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…