Je, ulimwengu una mwisho? Bonus question: What is nothing?

Je, ulimwengu una mwisho? Bonus question: What is nothing?

Kwa Hadi Sasa tulipo kiutaalamu majibu hayawezi kukamilika, lazima majibu yatoke kutokana na jinsi tulivyo kiteknolojia Hadi hivi Sasa, Bado sisi ni wageni kabisa wa sayari yetu, hata dunia yetu Bado sana Kuna chungu ya mambo hatujayamaliza hivyo Kwa kuwa Bado tupo kwenye hatua ya kuzidi kutambua swali Hilo halina majibu yaliyokamilika Sasa basi kutokana na swali Hilo nadhani tutazidi kuchambua na kuibua Kwa undani mada nyingine ndogondogo zitakazoweza kuzidi kutupwa mwaga.

Sayari yetu ni kijisayari kidogo sana, hivyo tuna kazi kubwa ya kujua mabilioni ya sayari, kwanza sayari za karibu tu Bado hatujazama ndani kabisa, unajua kinachowatia hofu mabwana wakubwa ni Nini?, pale ambapo binadamu wote watakuja kufahamu kwamba Kuna sayari nyingine nyingi kama vile dunia yetu na wakati huo huo uwezo wa kuzifikia ni rahisi, unahisi Nini kitatokea?, mifumo iliyotengenezwa duniani itakuwaje?, ndio maana Kuna mambo unaweza Dhani yanaenda taratibu lakini kumbe Kuna watu washafika mbali tayari lakini je watu au mataifa yako tayari kuukabili Ukweli mchungu?.
Siku tukiweza kutoka nje ya kifungo fikra cha dini tutakuwa tumefika karibu na kilele cha ufahamu wetu
 
Ili kitu kiwe ukweli lazima uwepo uthibitisho na ushahidi wa kitu hicho.

Ili tukifanya uhakiki, tupate uthibitisho wa kitu hicho.

Sasa wewe Thibitisha uwepo wa Mungu na si imani yako tu.
Narejea maelezo yangu ya awali kuwa ushahidi wa uwepo wa Mungu kwa mujibu wangu ni imani inayokuwa backed na mazingira ya kidunia tuliyomo na yale ambayo wanadamu wameweza kuchunguza na kubaini.

Whereas wewe unataka kum comfine Mungu kwenye scientific methods ili uweze kubaini uwepo wake...utakwama kwani Mungu ni beyond hizo methods.

Imani haiwezi kuthibitishwa kwa kanuni za kisanyansi..ila ni halisi na ipo. Ili uweze kumthibitisha Mungu kiimani ni lazima wewe mwenyewe upitie uzoefu fulani utakaomfunua huyo Mungu kwako.

Otherwise hatutafika mwisho kwenye hii debate. Ni kama wewe usivyokuwa na uthibitisho wa kutokuwepo kwa Mungu.
 
Vyote vyenye mwanzo vinamwisho
Hata maumbile yanaonyesha hili
Maisha ya kila siku ynaonyesha ilo pia
 
Narejea maelezo yangu ya awali kuwa ushahidi wa uwepo wa Mungu kwa mujibu wangu ni imani inayokuwa backed na mazingira ya kidunia tuliyomo na yale ambayo wanadamu wameweza kuchunguza na kubaini.
Imani si ushahidi.

Mimi nikikwambia kwamba nina imani kwamba kuna Dragons 🐉 watemao moto 🔥 midomoni mwao bila kukuthibitishia kwa kukuonyesha hao Dragons wenyewe walivyo,

Je utanikubalia tu hivyo hivyo?
Whereas wewe unataka kum comfine Mungu kwenye scientific methods ili uweze kubaini uwepo wake...utakwama kwani Mungu ni beyond hizo methods.
Ulijuaje Mungu ni beyond hizo methods?

Ulifanya Utafiti gani ukagundua kwamba kuna Mungu, Kisha ukagundua kwamba Mungu huyo yupo beyond scientific methods?
Imani haiwezi kuthibitishwa kwa kanuni za kisanyansi..ila ni halisi na ipo. Ili uweze kumthibitisha Mungu kiimani ni lazima wewe mwenyewe upitie uzoefu fulani utakaomfunua huyo Mungu kwako.
Msingi wa imani ni kutokuwa na uhakika.

Na unaweza kuamini hata uongo, kwa vile ni imani tu.

Ili kitu kiwe ukweli lazima pawepo ushahidi, uhakiki na uthibitisho.

Sasa wewe unathibitisha vipi kwamba huyo Mungu yupo kweli na si imani yako ya kufikirika tu?
Otherwise hatutafika mwisho kwenye hii debate. Ni kama wewe usivyokuwa na uthibitisho wa kutokuwepo kwa Mungu.
Madai ya kuwepo Mungu yametoka kwenu nyie waamini Mungu.

Ninyi ndio mnadai kuna Mungu, Hivyo nyie ndio mnapaswa kuthibitisha madai yenu ya uwepo wa huyo Mungu mnayedai yupo.

Ukishindwa kuthibitisha uwepo wa huyo Mungu unayedai yupo, Ni kwamba madai yako ya uwepo wa Mungu ni madai ya UONGO. Na huyo Mungu unayedai yupo, Hayupo.

Una elewa?
 
Imani si ushahidi.

Mimi nikikwambia kwamba nina imani kwamba kuna Dragons 🐉 watemao moto 🔥 midomoni mwao bila kukuthibitishia kwa kukuonyesha hao Dragons wenyewe walivyo,

Je utanikubalia tu hivyo hivyo?

Ulijuaje Mungu ni beyond hizo methods?

Ulifanya Utafiti gani ukagundua kwamba kuna Mungu, Kisha ukagundua kwamba Mungu huyo yupo beyond scientific methods?

Msingi wa imani ni kutokuwa na uhakika.

Na unaweza kuamini hata uongo, kwa vile ni imani tu.

Ili kitu kiwe ukweli lazima pawepo ushahidi, uhakiki na uthibitisho.

Sasa wewe unathibitisha vipi kwamba huyo Mungu yupo kweli na si imani yako ya kufikirika tu?

Madai ya kuwepo Mungu yametoka kwenu nyie waamini Mungu.

Ninyi ndio mnadai kuna Mungu, Hivyo nyie ndio mnapaswa kuthibitisha madai yenu ya uwepo wa huyo Mungu mnayedai yupo.

Ukishindwa kuthibitisha uwepo wa huyo Mungu unayedai yupo, Ni kwamba madai yako ya uwepo wa Mungu ni madai ya UONGO. Na huyo Mungu unayedai yupo, Hayupo.

Una elewa?
Unaposema kuwa huyo Mungu hayupo ni kwa vile unatumia akili yako kwa kuangalia udhaifu wa sababu za uwepo wake bado unakuwa haujathibitisha kutokuwepo kwake.

Hebu thibitisha kuwa huyo Mungu hayupo with vivid reasons.
 
Unaposema kuwa huyo Mungu hayupo ni kwa vile unatumia akili yako kwa kuangalia udhaifu wa sababu za uwepo wake bado unakuwa haujathibitisha kutokuwepo kwake.

Hebu thibitisha kuwa huyo Mungu hayupo with vivid reasons.
Siwezi kuthibitisha uwepo wa kitu ambacho hakipo.

Kitu kisichokuwepo hakithibitishiki kwa namna yoyote ile.

Kwa sababu hakipo kwa namna yoyote ile ya kuthibitishika kipo. Hivyo hakipo.

Wewe unayedai Mungu yupo ndio uthibitishe yupoje?

Ukishindwa kuthibitisha Mungu yupo ni kwamba Mungu hayupo.

Na madai yako ya kwamba kuna Mungu ni madai ya uongo.
 
Kwa nn usigundue kitu kama una maswali fikirishi kama haya mkuu? Mbaya zaidi hata mradi wa milion 5 tu utakushinda...

Turudi kwenye mada..

Can you define the reality within the term "universe"?. What are the differences between universe and the world?

I think the world universe is beyond the term "world". Universe imebakia kwenye theoretical explanation na sijui kama ina exist. Kilichokuwa exist unachoweza kukiona ni dunia "world".

Universe kuna namna imesimama kama mfumo ambao umesimama solely. Hautegemei kitu kingine kuexist

Hapo kwenye world weka Earth
 
Kwa kwenda juu na kushuka chini ulimwengu una mwisho?

Wazee wa zamani walijua Kijiji wanachoishi ndiyo mwisho was dunia na hakuna maisha nje ya Kijiji. Baadae maendeleo yakafanya watu wajue hakuna maisha nje ya bara lao na wamezungukwa kote na maji tu.

Walipotengeneza meli wakajua kumbe Kuna mabara mengine ila dunia ndiyo mwisho. Walipogundua telescope wakagundua kumbe tupo ndani ya solar system iliyo ndani ya galaxy, galaxy Ina nyota zaidi ya Billioni 400.

Na bado galaxy tulizoziona ni zaidi ya trilioni 2 kwenye observable universe.

Key word ni Observable. Observable haimaanishi kwamba ndiyo mwisho was uwezo was vifaa tulivyo navyo kuona. Sio uwezo wa Bali ndio mwisho wa wigo tunaoweza kuona.

Maana nje ya hapo ulimwengu unatanuka Kwa Kasi kubwa kuliko spidi ya mwanga. Kwahyo mwanga wa hizo nyota kamwr hauwezi kutufikia.

Hence inaitwa unobservable universe. Yani hata tupewe miaka milioni ya teknolojia hatuwezi kupaonaa.

Lakini tuachane na uwezo wa kuona au kutokuona Leo swali langu ni la kifilosofia zaidi, je ulimwengu una mwisho?

Kama mwisho haupo inawezekanaje? Yani ulimwengu uendeleee milele na milele bila kubwa na ukomo?

Ina maana hauna kati pembeni Wala juu? Na kama Kuna mwisho, nje yake Kuna Nini?

Je, kuna utupu TU (space)? Maana hata hicho ni kitu. Kama Hamna kitu, what is Nothing? Is nothing possible?

Kama hakuna kitu na ukasimama kwenye ukingo wa ulimwengu, ukiamua kwenda huko nje itawezekana?

Kitu kwenda kwenye kusiko na kitu?

Kuna baadhi ya wanafizikia wanaamini ulimwengu ni kama mpira, kwamba hii spacetime tunayoishi imecurve Kwa degree ndogo sana na inatengeneza mzunguko kama mpira/yai.

Kwahiyo ukisafiri Kwa kunyooka baada ya mda mrefu karibia milele utajikuta umerudi ulipoanzia. Lakini hiyo siyo solution ya swali langu, maana litabaki palepale; nje ya huo mpira Kuna Nini?

Na labda ukitoka nje ya ulimwengu ukasafiri mbali sana utakutana na ulimwengu mwingine. Lakini Hata kama Kuna limwengu nyingi nje yake Kuna Nini?

Wazee wa multiple universes, Schrodinger's cat mnasemaje? Multiple timelines zinawezekanaje?

Au ulimwengu mzima upon ndani ya bakuli kwenye sebule ya Mungu? Hays huo ulimwengu wa Mungu hauna mwisho? Mungu ana mwisho wa upeo?

How significant are we? Maana ukizoom out ni sawa tunaishi juu ya jiwe linaloelea angani tunaloliita dunia. ila ukizoom out Hilo jiwe linakuwa kama kamchanga kadogo, kama ulimwengu (observable) ni bahari basi sisi tunaishi kwenye kamchanga kamoja kwenye ufukwe wa hiyo bahari. Na vipi tukizoom in? Kuna mwisho?

Mwanzoni wanasayansi kama Kina john Dalton waliamini mwisho ni kwenye atoms.

Baadae wakagundua hizo atoms zimeundwa na electrons protons and neutrons baadae wakagundua quarks, gluons, higgs, bosons, neutrinos nk. Nk.

Na wanazidi kugundua kadri teknolojia inavyokua. Je, Nako Kuna mwisho? Au na penyewe Kuna ukomo wa observation?

Does nothing exist? What is it?
Is it the absence of things?
Space time itself is a thing.
Does time exist when there are no things?

Huko nje ya ulimwengu Kuna muda?

Niishie hapa maana naona maswali ni mengi yasiyo na majibu.
Umetumia neno mujarabu OBSERVABLE, hii inamaanisha mwisho tunaoufahamu ni pale technology iliyopo duniani kwa sasa uwezo wake wa kuona/kukadiria unapoishia.
Ukweli utabaki kuwa UNIVERSE haina mwisho, hakuna NOTHING. Bahati mbaya uliyona(I mean inayokukosesha majibu) ni kuwahi kuzaliwa, kwa watakaozaliwa maybe 20 or rather 100 centuries from now majibu ya maswali yako yatakuwa ni kitu obvious kwao japo nao watakuwa na maswali beyond their knowledge/technology. Maybe colonisation au slavery itarudi kwa viumbe kutoka galaxies tofauti kuvamiana, kupigana na kutekana. Nobody knows. Hata aina ya viumbe(intelligent creatures) wa 'huko kwingine' hatuna hata idea wakoje(I mean maumbile kama idadi ya miguu, mikono, macho nk) na kama wakiingiliana na binadamu watazaa kitu gani lakini hivyo ni vitu ambavyo mbeleni vitatokea na bahati mbaya hatutakuwepo kushuhudia.
 
Kuna siku nilimuuliza padre mmoja kwamba mpaka sasa kitu kinachojulikana duniani kuwa na mwendo kasi kuliko vyote ni mwanga.
Wanasayansi kwa kutumia vifaa wameweza kuona sehemu ya ulimwengu kwa mwisho wa uwezo wa vifaa vyao kutoka hapa tulipo mpaka hapo vifaa vya binadamu uwezo wake ulipo ishia ni miaka ya mwanga bilions kadhaa, ikumbukwe mwanga inasafiri km laki tatu na zaidi kwa sekunde, kwa hio laki 3 kwa sekunde moja mara dakika mara saa mara siku mara kwaka mara miaka elfu mara miaka bilioni ni muda na umbali mrefu mno

Hapo walipo ishia wanasayansi ni kwamba bado ulimwengu unaendela ila hio inayo itwa mbingu au makazi yangu yalio nje ya ulinwengu hayajafikiwa.

Swali langu kwake ni kulingana na masimulizi ya vitabu vya dini au biblia tuna miaka karibu 2000 tokea Yesu alivyo paa kwenda mbingini, kwa makadirio hayo ya muda wa kusafiri kwa mwanga hata kama Yesu alikua ana paa kwa speed ya mara milioni zaidi ya mwanga ina wezekana mpaka leo hajafika huko kunakoitwa mbingini?

Jibu lake alisema hamna mbingu wala jehanam kama sehemu bali mbingu na jehanam ni hali, pia Mungu au kinachoitwa ulimwengu halipo chini ya kifungo cha muda, muda ni dhana , ulimwengu upo kabla ya muda na muda utaisha ila ulimwengu utaendela kuwepo.
Kwahiyo ulimwengu na Mungu ni kitu kilekile?
 
Mwenye tafiti binafsi aweke hapa na sio kuleta habari za watu wengine toka kwenye makabrasha yao.
 
maswal yako ni mazur na ni afya ya akili
sasa ndio ukisikia tunayoyajua katika elimu yake mungu ni sawa na tone au kipande cha ukucha.kwenye bahari. mungu ana elimu bwana
 
Ulimwengu hauna mwanzo wala mwisho.

Ulimwengu ulikuwepo, upo na utaendelea kuwepo milele.
Natamani kukuamini, Lakini hiyo ingemake sense kama ulimwengu ungekuwa static.
ila unabadilika, Tena haubadiliki randomly tu ila Kuna sense ya direction kwenye hayo mabadiliko.
Yani Jana ni tofauti na Leo na Leo ni tofauti na kesho.
Miaka billion 10 iliyopita hata dunia haikuwepo.
Sasa kama Kuna mabadiliko ya kutoka sehemu moja kwenda nyingine hiyo ni kama inaashiria kuwa Kuna sehemu ulimwengu ulipotoka (mwanzo) na Kuna sehemu unaenda (mwisho)
 
Back
Top Bottom