Hakuna aibu mbaya kama kuomba ukajisaidie porini ukiwa kwenye Bus kitendo cha kurudi kwenye Bus abiria 59 wote macho kwako, sijui uwa kuna kosa gani?
Tumepita Shy town alfajir tukielekea Rock city,
Tukiwa DarLux iliyolala Nzega ikitokea Dar,
Viti vya mbele yetu vya tatu kutokea nyuma walikaa Sista duu wawili na Mmoja alikuwa akilia bila msaada,
Nikamuuliza mwenzake vipi Mwenzio?
Akajibu anaumwa tumbo,
Nikamuuliza tena umemjulisha Kondakta?
Akajibu hapana, Mi nikamfuata konda na kumtaka Msaada, ila akajibu Dawa tunazo lakin hatuwezi kumpatia maana hatujui anaumwa nini,
Labda tumpatie Magnesium!!!
Nikachukua na kumpelekea ila mgonjwa akasema haziwezi kumsaidia labda gari isimame akajisaidie!!!!
Kweli bhana akasaidiwa
Aaah amerudi akanishukuru na baada ya dk kadhaa akaanza kuchati amepona