darasa la pili hilo enzi michezo ya gololi imeenea,
basi baada ya kubunwa gololi zoote nikawa sina jinsi, nikarudi home mpaka chumba cha bro, kuingia nakuta tsh 40 mezani, yaani tsh ishirini ishirini ziko mbili,
basi nikazichukua fasta kisha nikachomekea t-shirt yangu na kile kipensi nikichovaa, then nikazidumbukiza zile hela ndani ya shati(nimechomekea ili nikiweka hela zisidondoke)
na ikitokea hata nimefumwa nikisachiwa mfukoni zisionekane.
sasa mazee ile natoka tu ndani Haaamad bro huyu hapa, uso kwa uso mlangoni, akaanza kuniuliza enhee umefuata nini chumbani kwangu? Kuniuliza vile nikaanza kubabaika cuz kila mtu ana chumba chake,
kisha akaniuliza tena
Hujaniibia hela wewe? Hebu ngoja niziangalie.
Dooh kuzichek hazipo!
Ikabidi aaanze kunisachi huku mimi nikijitetea sijachukua.
Akasema hebu ruka ruka nione, basi ile kuruka ruka mara naskia sarafu yakwanza imeanguka chini, sijakaa sawa na nyengine imeanguka. Dah nilijiskia noma kweli,
ukichek ndo mara yangu ya kwanza kumuibia,
Gololi ziliniponza aisee manake malengo yangu pale nilijua nakwenda kununua gololi zingine ili nizikomboe gololi zangu