Kuna nyakati around 2006 nikiwa elementary school msimu was visiting day's nilitembelewa na washua, baada ya tukio jioni yake nikawapanga washakaj zangu tuzame bwenini na misosi iliyobaki kinyume na utaratibu. Dah! tukashikwa baadae na Matron tukajua kuwa tutapewa adhabu za kawaida mambo yaishe, aisee kumbe tunatakiwa kula vyakula vyote tulivyobeba as a group na vikiisha tumesamehewa. Sitakaa nisahau wahuni tulivyokula mpaka tukaanza kutia aibu na vilio, tulilia maana tumeshiba, kuvimbiwa na bado midomi havishuki mezani ndio mazaga kama yote bado vinywaji. Nakumbuka ilibidi nilazwe hadi kutapishwa na nurse maana nilianza kukosa hadi pumzi. Kwa kweli tuliabika sana na wana tulipata bahati tukio kuwa lilitokea dormitory ya boys only, mademu walikuja kupewa story tu. Na ndio mara ya kwanza kujishuhudia kuwa mtu anaweza kula mpaka kulia bila hata kupigwa wala kuumizwa popote. Kwa kweli tusiwe na mazoea ya adhabu, unaweza kupewa task ya kawaida ikakupa shida mpaka ukapagawa.