Je, ulishawahi kukutana na kitu cha kutisha usiku? Pita hapa tupeane uzoefu

Huko kigoma ni balaa, siku moja tulikuwa huko ikafika mida ya usiku tukatoka kuingia mitaani kuwasaka ma chick. tukiwa ktkt ya road tukamwona demu mmoja mfupi kwa mbali tukampigia mluzi gafla akaingia kwenye kona kuangalia nyuma demu si huyu hapa acha ma raia wajikojolee dah....

Siku nyingine tukiwa shinyanga mida ya saa moja usiku tukakimbizwa na mfuko empty wa sementi du balaa.... Kuna maeneo yanatisha

Siku moja tukiwa moshi town usiku kama saa 3 tunarudi hotelin tukapitia njia flani tukakutana na bonge la nyumba lina uzio halijakamilika tukachungulia ndani kuna nini kulikuwa na mipaka imefika kama ndama ikaruka ukuta ikasepa na sis kujihami tukaingia ndani kwa mtu wote sijui yalikuwa majini ...
 
Binafsi niliwahi oa mke ambaye anasumbululiwa sana na maruhani.
Tuliachana sababu nyingi tu ikiwemo kuchokana haraka kwenye ndoa ila kwa kipindi nilichokuwa nae mandoto ya kutisha yalikuwa mengi sana.
Hivi karibuni alikuja mkoa niliokuwa nakaa ajabu niliota nimedondokewa na kundi kubwa la sisimizi miguuni na nimewakanyaga wanavyotafuta pa kutembea/kutokea na wengine wanataka kunipanda mguuni,ila ajabu ni mguu mmoja tu ndio nnaoangaika nao wasinipande? Sijui ni nini tafsiri yake
 
tuliwahi kimbizwa na kiumbe wa ajabu tulikua tuna toka disco vumbi vijijini , alikua na urefu usio wa kawaida alf miguu yake ina kwato cha ajabu ilikua ukijificha anakutokea kwa mbele na alikua mmoja ila aliweza kumtokea kla mtu tulikua kundi la watu wa 5 alitukimbiza ucku kucha ajabu nyingine kla ukikaribia nyumban kunasogea mbele sita sahau ucku huo wa mateso
 
hahaaa...mpaka leo sijajua kama wale jamaa walinifukuza au nilijikimbiza bure tu.

Wala hawakukufukuza, ulikimbua kwa panic tu, wangekuwa na nia na wewe wala usingepiga hatua mbili. Wangeweza kukufanya ukakimbia mbio kali lakini uko hapo hapo unakimbia mpaka kunakucha lakini nyumbani hufiki.
 
Hao jamaa wakiwa na shughuli zao wala hawana mpngo na mtu
 
Wala hawakukufukuza, ulikimbua kwa panic tu, wangekuwa na nia na wewe wala usingepiga hatua mbili. Wangeweza kukufanya ukakimbia mbio kali lakini uko hapo hapo unakimbia mpaka kunakucha lakini nyumbani hufiki.
Hahahaa
 
vitu vya kutisha havipo usiku tuu ,hata mchana kweupe vinaweza kukutokea,miaka flan tulipata tenda ya kupeleka mzigo kigoma/kakonko na tulipofika ili bidi tukae kama wiki hivi tukingoja mzigo wa kuludi dar es salaam bhas kuna siku tukaingia Bar flan ilikuwa mapema tuu asbuh dah ilipofika mchana tukawa tushakolea vyombo kichwani ikiwa ni mixer ya safari lager na the kick tukaona tukaona madada poa tukapumzike ila kwa mchana ule hawakuwapo so tukabahatika kutongoza akina mama waliokuwa wamekaa pembeni yetu na tukakubaliana bei then tukaanza safar ya kuelekea guest....dah kufika guest kila tulipotaka kuwaingilia vitendea kazi vilisinyaa kabisa,kwakuwa na sisi tulikuwa wahuni kuna mambo tulikuwa nayo yakasaidia viungo kuinuka ila kilichofata jinsia zao zimekuwa za kiume aisee tulitoka guest bila viatu na mashat tulivalia nje.........1998

Hii baba ni chai ya mdalasini kabisa
 
Niaje mipini na majembe wa JF..

Je ulishawahi kutana na kitu cha kutisha usiki kama mchawi, jini, mnyama basi share na sisi tukio lako hapa. Nianze mimi;

Iikua mwaka 2007 nipo na washkaji wawili tumetoka kucheki muvi za usiku saa saba, katika tembea yatu ana kwa ana tunakutana na "JOGOO" nikisema jogoo jogoo kweli kwa ukubwa alikua kimo cha kondoo. Bwanaa wee mbio tulizokimbia kushinda zile za kwenye muvi ya KUNG FU HUSTLE jogoo alituunganishia mpaka karibu na nyumbani kabisa, mpaka leo hua najiuliza sijui atakua yule aliyembeba Pazi shule ya msingi? Toka siku hiyo nilikoma kutembea usiku.[/color=pink]
Hiyo ilikua Kigoma.

Tukio la pii.
2012 tukiwa tumetoka kwenye magroup yetu ya kujisomea usiku tunawasindikiza majamaa gheto kwao wakati tunarudi tukakutana na Ndama wa mguu mmoja aisee tulikimbia mlango wa nyumba tuliufungua kwa Buti la Shaolin soka. Toka siku hiyo kuanzia saa nne usiku hunitoi nyumbani hata kwa dawa.

Please share na wewe.

-Mond-

Sasa mkuu hiyo 2007 unasema ulikoma kutembea usiku halaf ukarudia tena 2012. Kumbe hukukoma
 
1997 Vi-form 1 wenzangu wananitambia kuiona movie ya PREDATOR (Anorld ya jini) kwenye kibanda umiza,nikailaani sana mifugo (mbuzi)waliosababisha niwe malishoni wakati wenzangu wako wanafaidi mikwara ya akina BILLY DUKE...ikapita kama wiki hivi hiyo muvi ikawa inaoneshwa tena ila bahati mbaya inawekwa usiku kuanzia saa 4 mara tu baada ya trela la Alain Kounkou....
Home- ruhusa kama hiyo sahau kupewa (kutembea usiku?!)....nikajiapiza kutoikosa siku ya leo hata iweje,....Ili nifanikiwe lengo mzee nikalihujumu dirisha la chumbani kwangu kwa kung'oa nondo moja ili nipate pa kutokea pale familia nzima ikiwa imelala...
Saa 3 tayari raia wote wanakoroma,starling nikalinyatia dirisha nikajikuta niko nje,...ndani ya dk 5 nikawa nimejumuika na watu wazima holini tunamalizia album ya R.A.S (Alain) ili muvi lianze...muvi likaanza, muvi likaisha,nikaridhika...
Kutoka nje giza totoro....njia ya kwenda home mwendaji ni mimi tu,sina kampan coz tulikuwa tunakaa kwenye kota za shule alafu zimejengwa mbali na kijiji (Kunaitwanga Mahuta-Mtwara)...
Kijiji usiku huu kiko kimyaa,nyayo zangu tu ndo zinatoa sauti...kuna kipande cha msitu kinachotenganisha eneo la shule na hiki kijiji (hilo ndo eneo pekee nililolihofia kabla hata sijalifikia)....sasa wakati nazimalizia hizi nyumba za mwisho-mwisho ili niukabili huu msitu,mita kama 7 hivi kulia kwangu,kati ya nyumba moja na nyingine (zote zimeezekwa kwa nyasi) nikaona kundi la watu wako uchi,wako wima, wametengeneza kamduara hivi,wako kimya...BWANA BWANA wee...
Kuna kitu kama shoti ya umeme hivi iliyonifanya mwili,nywele visisimke kwa pamoja na nikauona mwili kama hauko na mimi vile...huku nikiwa nimesimama,moyo unataka utoke nje kwa mapigo ya KUDU-KUDU,nikiwa sijui la kufanya maana lile kundi nahisi lilikuwa bado halijaniona 'mwana mzurura usiku'... (vyote hivyo ni ndani ya kama sekunde 5 hivi)...
Mara kwa pamoja (utadhani waliambiana) kundi lote lile wakageuza vichwa vyao na kunitazama fwaaa......
Nakumbuka nikasema "Mawee" bila kutoa sauti (nikijua saasaa nyama ya mtoroka kwao inaenda liwa punde) na kufuatia na mbio za kukimbilia vidole/kama sio kucha pasipo kugeuka nyuma...nyumbani nikapitiliza,mbwa wa home akaanza kubweka na yeye akaniungia tela kimyakimya akijua tunacheza,nikajua hapa naenda chaka,nikageuza...mbio hadi dirishani...sikujali nani atasikia ninavyoingia au lah,...narukia dirishani,mbwa naye anavuta suruali kwa chini(huyu dog alikua best angu sana)baada ya zile kukuru-kakara za kuingia ndani...nikajikuta niko kitandani nahema kwelikweli, tena kwa nguvu,koo limekauka, huku mguu mmoja unaning'inia dirishani suruali inaendelea kuvutwa na mbwa nje......
Hahah umenfrahsha mkuu
 
tuliwahi kimbizwa na kiumbe wa ajabu tulikua tuna toka disco vumbi vijijini , alikua na urefu usio wa kawaida alf miguu yake ina kwato cha ajabu ilikua ukijificha anakutokea kwa mbele na alikua mmoja ila aliweza kumtokea kla mtu tulikua kundi la watu wa 5 alitukimbiza ucku kucha ajabu nyingine kla ukikaribia nyumban kunasogea mbele sita sahau ucku huo wa mateso
Usukumani huyo tunamwita Kabhebha

Sent from my TECNO-N8 using JamiiForums mobile app
 
1997 Vi-form 1 wenzangu wananitambia kuiona movie ya PREDATOR (Anorld ya jini) kwenye kibanda umiza,nikailaani sana mifugo (mbuzi)waliosababisha niwe malishoni wakati wenzangu wako wanafaidi mikwara ya akina BILLY DUKE...ikapita kama wiki hivi hiyo muvi ikawa inaoneshwa tena ila bahati mbaya inawekwa usiku kuanzia saa 4 mara tu baada ya trela la Alain Kounkou....
Home- ruhusa kama hiyo sahau kupewa (kutembea usiku?!)....nikajiapiza kutoikosa siku ya leo hata iweje,....Ili nifanikiwe lengo mzee nikalihujumu dirisha la chumbani kwangu kwa kung'oa nondo moja ili nipate pa kutokea pale familia nzima ikiwa imelala...
Saa 3 tayari raia wote wanakoroma,starling nikalinyatia dirisha nikajikuta niko nje,...ndani ya dk 5 nikawa nimejumuika na watu wazima holini tunamalizia album ya R.A.S (Alain) ili muvi lianze...muvi likaanza, muvi likaisha,nikaridhika...
Kutoka nje giza totoro....njia ya kwenda home mwendaji ni mimi tu,sina kampan coz tulikuwa tunakaa kwenye kota za shule alafu zimejengwa mbali na kijiji (Kunaitwanga Mahuta-Mtwara)...
Kijiji usiku huu kiko kimyaa,nyayo zangu tu ndo zinatoa sauti...kuna kipande cha msitu kinachotenganisha eneo la shule na hiki kijiji (hilo ndo eneo pekee nililolihofia kabla hata sijalifikia)....sasa wakati nazimalizia hizi nyumba za mwisho-mwisho ili niukabili huu msitu,mita kama 7 hivi kulia kwangu,kati ya nyumba moja na nyingine (zote zimeezekwa kwa nyasi) nikaona kundi la watu wako uchi,wako wima, wametengeneza kamduara hivi,wako kimya...BWANA BWANA wee...
Kuna kitu kama shoti ya umeme hivi iliyonifanya mwili,nywele visisimke kwa pamoja na nikauona mwili kama hauko na mimi vile...huku nikiwa nimesimama,moyo unataka utoke nje kwa mapigo ya KUDU-KUDU,nikiwa sijui la kufanya maana lile kundi nahisi lilikuwa bado halijaniona 'mwana mzurura usiku'... (vyote hivyo ni ndani ya kama sekunde 5 hivi)...
Mara kwa pamoja (utadhani waliambiana) kundi lote lile wakageuza vichwa vyao na kunitazama fwaaa......
Nakumbuka nikasema "Mawee" bila kutoa sauti (nikijua saasaa nyama ya mtoroka kwao inaenda liwa punde) na kufuatia na mbio za kukimbilia vidole/kama sio kucha pasipo kugeuka nyuma...nyumbani nikapitiliza,mbwa wa home akaanza kubweka na yeye akaniungia tela kimyakimya akijua tunacheza,nikajua hapa naenda chaka,nikageuza...mbio hadi dirishani...sikujali nani atasikia ninavyoingia au lah,...narukia dirishani,mbwa naye anavuta suruali kwa chini(huyu dog alikua best angu sana)baada ya zile kukuru-kakara za kuingia ndani...nikajikuta niko kitandani nahema kwelikweli, tena kwa nguvu,koo limekauka, huku mguu mmoja unaning'inia dirishani suruali inaendelea kuvutwa na mbwa nje......
Nimeipenda hii,ila wachawi noma asee

Sent from my HUAWEI P8max using JamiiForums mobile app
 
Kubwa lao ni rafiki yangu moja alivyonielezea kisa cha yeye kuacha udaktar.

Huyu rafikia yangu akiwa doctor ktk nchi moja ya ng'ambo,siku moja akiwa ktk zamu ya kikazi, wakaletwa majeruhi wengi kutoka ktk ajali ya treni ya umeme, sasa,yeye na wasidizi wake wakaanza kuwapitia wale majeruhi walioumia sana. Akiwa ktk pilikapilka zake pale amewahudumia mpk akachoka na kusikitikia wale majeruhi akaamua kwenda kupumzika kidogo ktk chumba chake akiwa pale,mara ghafla mlango ukafunguliwa hamad tena ghafla anaona MAJERUHI KAINGIA NA KIWILIWILI CHA KICHWA CHAKE KASHIKILIA MKONONI,KILE KIWILIWILI CHA KICHWA AKISEMA "DOCTOR PLEASE NIUMGIE KICHWA CHANGU KWANI NATAKA NIWAHI KWANI KESHO NI SIKU HARUSI YANGU NA MCHUMBA WANGU YEYE AKUUMIA ILA KANIAGIZA NISIPOENDA KUFUNGA NAE NDOA KESHO,NDO MWISHO WA MAHUSIANO YANGU NAE.

LAAAA!!! Yule rafiki yangu dokta alipopata nafasi ya kupenya pale mlango alitimua mbio na kelele za kutosha,yule majeruhi nae mbio nyuma ya doctor.

Laaaa unajua kilichofuata?????...?
Kesho nitamalizia kisa hiki cha kutisha kwani naona4 wino wa kalamu yangu umekwisha na ni usiku sana.
Hahahahahah uuuuwiii hatari saaana hii
 
vitu vya kutisha havipo usiku tuu ,hata mchana kweupe vinaweza kukutokea,miaka flan tulipata tenda ya kupeleka mzigo kigoma/kakonko na tulipofika ili bidi tukae kama wiki hivi tukingoja mzigo wa kuludi dar es salaam bhas kuna siku tukaingia Bar flan ilikuwa mapema tuu asbuh dah ilipofika mchana tukawa tushakolea vyombo kichwani ikiwa ni mixer ya safari lager na the kick tukaona tukaona madada poa tukapumzike ila kwa mchana ule hawakuwapo so tukabahatika kutongoza akina mama waliokuwa wamekaa pembeni yetu na tukakubaliana bei then tukaanza safar ya kuelekea guest....dah kufika guest kila tulipotaka kuwaingilia vitendea kazi vilisinyaa kabisa,kwakuwa na sisi tulikuwa wahuni kuna mambo tulikuwa nayo yakasaidia viungo kuinuka ila kilichofata jinsia zao zimekuwa za kiume aisee tulitoka guest bila viatu na mashat tulivalia nje.........1998
Katika maandishi haya nimeona neno moja tu

THE KICK

TBLMungu atawaaraaaaani
 
Back
Top Bottom