Je, ulishawahi kukutana na kitu cha kutisha usiku? Pita hapa tupeane uzoefu

Je, ulishawahi kukutana na kitu cha kutisha usiku? Pita hapa tupeane uzoefu

Huyo ndama wa mguu mmoja alikuwa amesimamaje!?

Sent from my HTC Desire 816 dual sim using JamiiForums mobile app
 
Nimeelewa mwl...
Naona nilicheka sana mpaka nikawa sikuiona hii maana umeielezea hata kwenye story maana imebidi niirudie (wakanitizama fwaa)
Mi nilidhani walikuwa katikati ya barabara

Nazan kwa huu mwaka huu uzi wa tatu kunichechekesha sana...

Sent from my TECNO-C8 using JamiiForums mobile app
Hahaha...basi poa mkuu!
 
Mie bhana nliendaga kwa ndugu zangu uko kijijini sasa tulikua ndugu wengi kidogo, hapakua na option zaidi ya wao ndugu zangu kunipa chumba cha ajabu kidogo, yaan nje ya nyumba yao kulikua na chumba ambacho kilikua hakitumiwi na watu, kilijengwaga kwa ajili ya wafanyakazi wa ng'ombe nk. Sasa hao wafanyakazi walikua ni wakabila flani iv tata kidogo kwa maswala ya ushirikina, walivyoondoka na kurudi kwao watu wakawa wanalalamika kila wakilala icho chumba, sasa mie sikuwai kujua habari hizi na kwa siku ile hapakua na option yoyote zaidi ya mie kupewa icho chumba, sasa sijui ndugu zangu waliniona mie kijana wa mjini mauza uza yatakwama au vp, ila ni vile ndugu wengine walikua watu wazima.

Kimbembe kikaanza usiku wa siku hio, sasa nimelala nahisi mmmmhh humu mbona kama kuna watu wengine tena waziada,basi napuuza mawazo haya tu ila sense zinaniambia kabisa we are more than 3 humu, aargggh nkafungulia RFA sikujali, sasa kimbembe kikaja usiku sanaa nikaanza kuskia watu wanatembea humo ndani, wengine wanapanda hdi juu ya kitanda nlicholala yaan nimelala naskia kabisa kuna mtu imesimama hapa kitandani, asee nliatuka vibaya sanaa, moyo unadunda, presha juu najiuliza naota au live, kumbe live, mara nikaskia mtu anavuta shuka, asee nliongea kwa nguvu "k**mamaaaaaeeeee" nani uyo, nkaskia sauti ya kicheko, nkajiuliza ndan au nje, asee nlisali sala zote, hali ikatulia kidogo, nikalala ila usingizi hauji, yaani nimetetemeka mpaka nimechoka, nimesali sanaa, sasa ukaja kama usingizi iv nikaanza kuota mambo ya ajabu et mule kuna watu watatu wananihoji wew umetoka wap, mbona mkorofi? Nani kakutuma uje chumbani kwetu khaaa nkastuka sasa nimestuka ila ile ndoto naiona kabisa inaendelea nikiwa macho, asee usiku ule ulikua vita vikali sanaa, nikawa macho tu nimefungulia radio kwa saut kubwa tu ila natetemeka haswa,,, kilichofuata kesho yake nikawaeleza ndugu zangu yote ndo wakanipa huu mkanda wa icho chumba na wengine hawakuamin kwamba nimewezaje kulala humo? Nikawamind kimoyo moyo wale ndugu kesho yake mchana tena uyoo nkarudi kwetu mjini,na nikasema niko radhi niue mchawi ila sio mwizi.
Ha ha ha kwa tusi ulilotoa lazma waseme we mkorofi
 
Anko wangu aliwah kunihadithia kwamba wakat anasoma huko Tunduru kuna siku waliwasindikiza wenzao stendi wakapande mabasi ya alfajir (miaka hiyo safar huanza saa 10 alfajiri)Basi baada ya kuhakikisha wenzao wamepanda basi wao wakaona haina haja ya kubaki pale wakaona warud shule.Ni mwendo kidogo na ni porini.Walipokuwa katikati ya safar Porini wakakutana na msafara.
Msafara ulikuwa unaongozwa na vikongwe wawili (Babu mbele na bibi nyuma)katikati wapo watu kama kumi wamebebeshwa mizigo ya kuni.
Anko alipowaona wale jamaa na mwenzie wao wakawapisha wale watu (Babu na bibi walijifunga nguo nyeus like kaniki)hawakusemeshana,so hawa wazee wa feva za usiku kama hawana na shida na wewe wanakuacha ila wale vibwengo watakua wanakuchezeachezea tu kwa bitimbwi

May Allah bless Me and You
Usiombe kukutana na kibwengo ni msumbufu
 
Nakumbuka ilikuwa amri kila jpili nyumba nzima hasa watoto kwenda kanisani hasa ya kwanza. Siku hyo Mimi na wadogo zangu tulidamka saa10 pasipo kujua na kuanza kujiandaa kama dk20 tukawa tayari tunajiandaa kuondoka, pembeni ya nyumba yetu alikuwepo mama muuza samaki alisemekana anatumia nguvu za Giza( mchawi) ile tunapita kwenye kona inayotenganisha kwake na kwetu mara paap!! Nikamuona kazungukwa na moto mkubwa sana na yupo uchi kama anaoga. Nilimkazia macho sana akapayuka piteni haraka.. Sijui kama wadogo zangu waliliona hilo, Sikuuliza Kitu wala kusema mpaka nilipokuja kusema badae sana
 
Ilikuwa Ifakara, maeneo ya Viwanja 60, nikiwa Form 2, siku 1 nikawa nasafiri kwenda DSM. Ili kupanda treni TAZARA, ilikuwa kuna basi tunapanda (mf wa daladala) kutoka Viwanja 60 mpk Kibaoni ilipo station ya TAZARA.

ili kubana matumizi kwa akili za kitoto, classmate wangu akanambia atanfata home kwa baiskeli yake na kunipeleka station.

Treni ilikuwa inapita alfajir kutokea Mbeya, so ili kuiwahi mshkaji alikuja home kama Saa 7 (enzi hizo IFAKARA ni kijiji) na kwa wastani baiskeli ingetuchukua masaa 2-3!

Safari ilianza powa. Humo njiani vijiji VYOTE kimyaaaaa, miti, misitu na mashamba ya mpunga!

Tulikuwa tunapokezana kuendesha kila Mmoja anapochoka! Ikafika zamu yangu kuendesha! Nikaendesha kama dk 20 hv - kukawa na observation flani tunaziona!

1. Mimi nikawa nafeel Kitu flani mf wa vile mtu analiskia tumbo wkt ndege inashuka ama kupaa!

2. Mshkaji akanambia anahisi kama vile tunaendesha baiskeli ktk barabara ya lami, alikuwa haisi kami yale makorongo ya mashimo (IFAKARA lami bado)

3. Ajabu ya Mungu, kila mtu alipatwa na woga lakini hakuna aliemuambia mwenzake! Binafsi nikaanza kuona MWENDOKASI wa baiskeli umekuwa juu sana, zaidi ya Mara 3 ya mwendo wa kawaida!

4. Mshkaji ghafla akanambia anahisi tairi za baiskeli hazigusi ardhi! Kweli kuangalia chini.... Tukaona Kitu mf wa pumba za mpunga!

5. Kilichofuata, ile baiskeli ilikuwa inafanya kama vampire! Ni sawa niseme ikiruka Morocco inatua Victoria! Ikiruka tena inatua Science! Ikiruka science inatua Makongo! Ikiruka Makongo inatua GOIG! Ikiruka GOIG inatua Mbuyuni! Cha kushangaza ile baiskeli ilikuwa ikitua haitoi wala hatuhisi kishindo km vile ikianguka Nazi ama embe!

6. Tulipiga kimya. Nikaacha kunyonga pedal na mshkaji nae akawa kimyaaaa! Nikahisi amelala lkn nikawa naogopa kumuita!

Tulifika station ndani ya kama dk 45 tu! Tulifika pasi na uchovu! Baiskeli ilikuwa Ok tu! Mshkaji nlikaa nae station mpk treni ilipokuja! Alirudi town baada ya jua kuchomoza!

Tangu Hapo tuliacha rasmi kuendesha baiskeli usiku!
 
Bibi yako alikurahisishia safari uwahi kufika..
 
Nakumbukaga wale walikua wanaitwa vigozo walikua wanatabia ya kupoteza watu walikua wanaishi milimani sasa utakuta kuna ukungu mwingi mliman harafu ukiwa unatembea unamona MTU mbele yako kisha unatembea haraka haraka ili safar yenu iwe moja babu unaenda kunyofolewa macho
 
Naskia umemnunulia diamond kikuku cha kuvaa mguuni
 
Sijawahi kutana na mizoga ya aina hiyo maishani mwangu japo kuna wakati fulani tukiwa vijana tulikuwa tukiamka usiku na kwenda maporini kusaka wachawi na mara zote hizo sikufanikiwa kuwapata.
 
Nilisha wai kukutana na mzuka weeee sitak hata kukumbuka
 
Back
Top Bottom