Je, ulishawahi kulazimisha mpenzi au rafiki aendelee kubaki maishani mwako?

Je, ulishawahi kulazimisha mpenzi au rafiki aendelee kubaki maishani mwako?

Sikua na hisia na yeye kabisa sikuona sababu ya kuendelea kumtesa wakati angeweza kupata mwingine na akapendwa tofauti na kwangu. Huwa sipendi kumuweka mtu ili hali najua kabisa napoteza muda wake huwa naamua tu kuwa mkweli.
Kwahiyo hapo haujampotezea muda? 9yrs?
 
Mimi iko tofauti, kwa miaka takribani 9 the guy alikua akinisihi nibaki maishani mwake lakini haikuwahi kuwa vile alivyotamani iwe. Nilikuja kukata mawasiliano kwa makusudi aweze kuendelea na maisha yake. J kokote uliko nakuwish maisha marefu ulikua mwanaume mwema lakini moyo wangu ulikosa hisia za kweli juu yako.
I feel his pain on this. But you are right
 
Habari wakuu.

Kwenye mizunguko yetu ya maisha kuna wakati unakua upo very attached na mtu Fulani either ni rafiki wa kawaida kama Man to man au Man to woman, pengine ni mpenzi wako umpendae sana san. Yaani unakuta una mpenzi roho yako imetokea kumpenda sana husikii wala huoni juu yake, kila muda unatamani uwe nae karibu au kuwasiliana na nae..Au kama ni rafiki yako wa kiume unakua kila ukitaka kufanya kitu Fulani unamstua mshikaji wako, yaani kama kuna ishu unatka kufanya mshikaji wako bila kuwepo unaona unaifanya kimagumashi. Kiuhalisia unakua upo mentally attached to that person, unakua umempa nafasi kubwa sana mpenzi wako au mtu huyo kwenye akili yako na maisha yako kwa ujumla.

Je huo upendo na nafasi kubwa uliyompatia kwenye maisha yako ushachunguza kama naye anakupatia nafasi hiyo? Jibu ni No! na kama ni Yes basi nafasi hiyo amekupa kwa muda, kuna muda utamtext atakujibu kwa wakati wake, utatamani kuongea nae ila yeye ataona unaboa tu, utataka uonane nae yeye atakuona msumbufu.

Ikifika hatua unaona mtu yupo online unamtext pm ana like tu, unamtext wasap ana soma then anakaa kimya sana au unamtext kwa sms halafu yeye kaka kimya wakati unajua hiyo sio kawaida yake jua kwamba huna chako hapo, utakua unalazimisha mawasiliana,mapenzi au urafiki ambao mwenzako hautaki tena.
Kwanini ulazimishe mawasiliano au mapenzi ? Kila kitu chatokea kwa sababu. Unajua unapompenda na kumjali mtu sana kiasi asicho stahili utaishia kupata maumivu usiyo stahili..

Subconscious mind hutenda kazi ikishirikiana sambamba na Nature, kuna hali Fulani unawez kua nayo katika maisha labda ni upweke,huzuni,kukosa faraja kiufupi unakua huna furaha au amani ya maisha. So kinachotokea ni kwamba
Subconcious mind inawasiliana na Nature kua mwanadamu huyu (yaani wewe) una matatizo Fulani maishani inaiamuru nature kutafuta mtu wa kuja maishani mwako ambae ataendana na hali ile uliyonayo.

Baada ya muda mfupi utajikuta umepata rafiki ukawa nae anakuliwaza kweli hadi ile hali ikawa imeisha..Mind ikishaona mentally ya huyu mtu iko stable inamuamuru nature kuruhusu yule mtu kuondoka au akaendelea kubaki. Hapo sasa ndio utaona umepata rafiki labda ni mwanamke au mwanaume akawa anakupa company sana kwa hali uliyonayo kwa muda Fulani (hata mwaka mzima. Unajikuta umekua attached sana na mtu huyo then inafika muda bila sababu yoyote ile ya msingi unaona mawasiliano na urafiki unapungua taratibu then unaisha kabisa. Hapo nature inakua ishafanya yake..

Nachotaka kusema ni kwamba watu ambao mpo kwenye mahusiano jifunzeni kusoa alama za nyakati, so unaona hapa mapenzi au urafiki unaanza kuisha ila wewe ndio bado unazidi kuongeza kupiga simu na kumfuata ili aendelee kubaki…Kijana kila kitu kinakuja kwa muda na sababu Fulani, hutakiwi kutumia nguvu kubwa kumfanya mtu aendelee kubaki kwenye maisha yako. Mtu kama ni muhimu kwenye maisha yako atakuja mwenyewe na kukaa nawe daima, huna haja ya kulazimisha.

Kwanini ulazimishe mahusiano? Watu wote hawa waliojaa duniani au unadhani yeye ndio bora pekee kuliko wote, mwache aende labda alikua sio riziki ya maisha yako! Utapata mwingine. Kikubwa zaidi ambacho hutakiwi kukifanya maishani mwako ni kupuuzia ubaya wa mtu anaokufanyia kwakua unahitaji mtu huyo aendelee kubaki maishani mwako, train your mind to be stronger than your feelings.

Kingine maishani mwako usionyeshe wema au uzuri wako ili uwafanye wavutiwe nawe, waonyeshe ule upande wako ambao ni mbaya uone kama watakuvumilia au wataondoka. Wakiondoka usijali jua ni watu fake. Be real that’s beautiful enogh kijana.
Mwaka mpya,misimamo mipya..Uliumbwa mwenyewe! Huyo mpenzi au rafiki yako umpendae sana ambae unaona huwezi fanya kitu bila yeye ni wa kupita tu.

Hamishia nguvu zote kwa mama yako ndio the best one ambae hatakuja kukusaliti. Jiamini katika uwezowako, unaweza kufanya makubwa bila mpenzi wako huyo ambae unaona huwezi fanya kitu kikafanikiwa bila yeye.If you Doubt your power, you power your doubt.

Binafsi hua sijali wala kujutia chochote maishani mwangu, ukinipenda Ahsante na karibu, ukiondoka hamna shida pia.. you weren't meant to stay in my life, if you were! You will stay in my life forever
A guy has said, It’s up to you To choose me or to loose coz I’m not a second choice
With or Without you, I shine!

Vers
Daah nipo kwenye hili janga na sijui pa kutokea,maana hivi sasa ananijibu kunya balaa lakini bado naamini atabadirika
 
Kilichowaunganisha siku zote ndio hicho kitawatenganisha. Kama mlikutana shule,chuo au kazini, akihama mmoja au mkamaliza,hapo ndio mwanzo wa mwisho wenu.

Alaf pia kumbukeni sheria moja muhimu sana kuhusu mahusiano ambayo inasema "Out Sight, Out of Mind"

Analyse.
 
Daah nipo kwenye hili janga na sijui pa kutokea,maana hivi sasa ananijibu kunya balaa lakini bado naamini atabadirika
Nini kimekukuta mkuu.? Share nasi tukusaidie umpate mrembo wako
 
Binafsi ninahisi nina Phobia ya kuogopa kua attached kwa mtu fulani, Maana najua tu mwanzo atanionyesha wema na upendo ila mwisho ndio atanionyesha upande wake wa shillingi..mmhh
Ila wanasema maisha ni kutake risk, if you can't take you loose a chance
Boss,hii comment huenda niliisoma lakini sikuelewaga,sasa ninaelewa ulichomaanisha hapa.mtu akiisoma kama hajapitia haya maisha hatoelewa
 
Tafadhali sana shea nasi mate yaliyokupata tuone tunatoana vipi huko.
Mm najua udhaifu wangu moyoni mwangu ndio maana naogopa sana
hahaha,mimi pia udhaifu wangu ni huo mkuu,ila to make things short ni kwamba siku hizi nimeacha kuzoeana na watu wapya mfano ile unajenga urafiki na mtu,na nilionao nawakwepa,sitaki kuwa attached kwa sababu unajikuta unamzoea mtu na kumkubali afu mwishowe unagundua hayupo vile ulivodhani au unaona anakupuuza
 
Mimi iko tofauti, kwa miaka takribani 9 the guy alikua akinisihi nibaki maishani mwake lakini haikuwahi kuwa vile alivyotamani iwe. Nilikuja kukata mawasiliano kwa makusudi aweze kuendelea na maisha yake. J kokote uliko nakuwish maisha marefu ulikua mwanaume mwema lakini moyo wangu ulikosa hisia za kweli juu yako.
Dah[emoji26][emoji26][emoji26]
Nimejaribu kuwaza maumivu aliyoyapata.
Nahisi ni maumivu makali Sana.
 
😅kweli kabisa mkuu,alafu mbaya zaidi ni ile mtu kila siku alikuwa anakutafuta ila ghafla anaacha, maisha lazima yaende
Noma sana mkuu. Tafuta girl mmoja atakae kupenda na utakaempenda kwa dhati toka moyoni. Ambae hataweza kuvumilia kukukosa. Unaweza kujikuta umemaliza watu 100 hafu wote wanakuumiza. Tafuta mmoja tu ila mnaependana
 
Mimi iko tofauti, kwa miaka takribani 9 the guy alikua akinisihi nibaki maishani mwake lakini haikuwahi kuwa vile alivyotamani iwe. Nilikuja kukata mawasiliano kwa makusudi aweze kuendelea na maisha yake. J kokote uliko nakuwish maisha marefu ulikua mwanaume mwema lakini moyo wangu ulikosa hisia za kweli juu yako.
Dah.. I understand how J felt nami nilipitia hiyo hisia, kumpenda mtu lakini ndani ya moyo wako unajua kabisa haiwezekani kuwa naye,

Na huyo unayempenda hawezi kulazimisha moyo wake ukupende (na unaona alijaribu lakini akashindwa) accepting defeat and letting go is the hardest part [emoji22] inauma sana
 
Back
Top Bottom