Nishawahi kutongozwa live live yani uso kwa uso kama mara 7 hivi, na zote hizo sikuweza kuchomoa...!
Ila nakumbuka vizuri siku moja nimetongozwa na Mke wa Mtu, sijawahi kuona Mwanamke kauzu kama yule, tulikua tunahughuria kikao flani hivi, sasa kwa jinsi nilivyo sio mtu wa kujichanganya sana, kiasi ambacho Kikao kikiisha tu, mimi huwa wa kwanza kuongoza njia na kuondoka kwenda zangu kwangu...!
Kumbe yule Manzi ananilia timing, tukimaliza kikao mpaka aanze kunitafuta anagundua nimeshafika mbali, kuasi hawezi kunifikia, kesho yake, siku iliyofata baada ya kikao kwisha, kama kawaida yangu naongoza njia kuondoka zangu Home, namwona kwa mbele kasimama, kufika alipo, ananiambia "Nilikua nakusubiri wewe, coz kila siku ni kama unanikimbia mimi" Mdada uso ni Mkavu, ananisemesha akinitizama usoni...
Nikamuuliza ulikua unasemaje!? Usihofu utajua, akaniuliza "Unapita njia ipi!?"
Nikamwambia "Nanyoosha straight" akasema "Basi twende"
Tukiwa njiani yule Dada akanambia "Sikiza, mimi nataka niende kwenye point moja kwa moja, mimi mambo ya kuzunguka huku naumia siwezi"
Nikamwambia "Karibu"
Akasema "mimi nakupenda, kupita kawaida, japo hatuna mazoea ila vikao hivi angalau vimefanya nikuone kwa ukaribu zaidi"
Kwa kweli nilishtuka, haikua mara ya kwanza kutiwa Sound na Binti, ila namna yule Binti alivyokua straight, serious, akinitazama Machoni, uso wake ni kama unasema (Ukikataa utanitesa) alinishangaza.
Nikamwambia "Naomba nipe muda ntakujibu"
Uso ukabadirika, nikauona U serious usoni mwake, (Yani kama ananidai hafu sitaki kumlipa pesa yake)
Akaniuliza "Muda unahitaji wa nini!?"
Nikamjibu "Inabidi nifikilie"
Akaniuliza "Ufikilie nini!?"
Nikamuuliza "Hivi ingekua mm ndo nimekutongoza sasa hivi ungenijibu nini!?"
Akanambia "Kama nimekuelewa nakubari hapa hapa, kama sijakuelewa nakuchana hapa hapa, hayo mambo ya nifikilie subiri, mambo ya kizamani, wewe fikilia hapa hapa nipe jibu langu"
Duh... Yule Dada alinipa wakati mgumu sana siku hiyo.