Je, uliwahi kufail/kufanya vibaya mitihani ajili ya mapenzi? karibu utupe mkasa

yuzazifu

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2018
Posts
5,108
Reaction score
9,469
Natumai hamjambo wakuu na weekend inaendelea uzuri.

Tukiwa tunaendelea kuliombea taifa dhidi ya corona, karibuni hapa tubadilishane mikasa ya mapenzi ilosababisha kufail/kufanya vibaya wakati tukiwa shule.

Nikiwa form two wakati mapenzi ya balehe yameshika kasi nilijikuta nafanya vibaya sana mtihan wa mock, nilipata wastan wa 48 kitu ambacho sikuwahi tarajia kupata coz kawaida yangu ilikua kupata wastan wa 80-90...

Matokeo haya yalinipa wakati mgum hadi wazazi wakaitwa shuleni, nilibanwa sana kueleza tatizo ni nni mwisho nilifunguka, niliadhibiwa na kukaripiwa then nikapewa onyo...

Nilipitia wakati mgum inshort but bdae niliweza kuyacontrol mapenzi na masomo hata nikaendelea vzuri

Karibu nawe utupe mkasa wako.
 
Wastani = Jumla /Idadi. Sasa huo wastani wa 80, 90 kwamba hiyo mitihani ulikua unatunga na walimu ama? ulikua vizuri sana

For sure mimi form 2 hata nilikua siwazi mapenzi kabisaa.
mkuu nimesoma na watu walikua wanapata hadi wastani wa 95-98, tz kuna vijana wana akili sana sijui hua tunakwama wapi tu huko mbele ya safari
 
Kuna ***** m'moja nilikuwa nampa attention, akawa analeta usenge, mimi nipo kwenye maandalizi ya mitihani, ananitumia sms usiku ananiambia ana mimba yangu, ***** yule, mimi nimekaa siku tatu nawaza namna imekuwaje nimekuwa baba na wakati plan yangu ni kuwa baba baada ya shule, baadae nimeshakubaliana na hali, na hapo nimeshampigia simu mara kadhaa nikimpa comfort na kumwambia asijali nimefurahi sana kuwa baba mtoto na ninahamu sana ya kuja kumuona mtoto wangu, ila ndani ya nafsi nina kila aina ya wasi wasi jinsi ya kuanza kuyaishi maisha mapya ya uzazi.

Baada ya siku kadhaa anakuja nambia kuwa alikuwa ananipima kuniona kama nina upendo wa kweli kwake na nina malengo nae sababu kama ningekataa huo ujauzito ina maana sina malengo nae....

So ikaishia hivyo nikaamua kukaa kimya sikuongea chochote, alipiga simu sikupokea, nikamtext tu kuwa kwasasa nina mambo mengi kichwani sihitaji mambo ya kitoto.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sawa kamanda
 
Kuwa na mpenzi hakuwezi kukusababisha ufeli, hasa pale unapokua na mpenzi ambae malengo yenu kimasomo na kimaadili yanafanana. Wapo waliopendana shuleni mpaka vyuoni na baadae wakaishi maisha ya mume na mke.

Ukiona umefeli basi ulitaka kulazimisha mambo nje ya muda wake.

HUU UJINGA WADADA WENGI SANA HUTUMIA KUPIMA WENZI WAO
 
Kuwa na mpenzi hakuwezi kukusababisha ufeli, hasa pale unapokua na mpenzi ambae malengo yenu kimasomo na kimaadili yanafanana. Wapo waliopendana shuleni mpaka vyuoni na baadae wakaishi maisha ya mume na mke.

Ukiona umefeli basi ulitaka kulazimisha mambo nje ya muda wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
mkuu ukiwa unayaanza mapenzi ile raha yakunyanduana huchanganya sana, hiki ndo kilinifelisha bt after kuyazoea kila kitu kilienda sawa
 
Nikiwa chuo mapenzi yaliyataka kunipelekesha puta, kilichonistua chuo nilikiwa nalipiwa na wazazi na nilikuwa muoga sana nikifeli itakuwa aibu. Nikawa nasema walau nipate C ila nisishikwe nikarudia mtihani au kurudia mwaka.

Jamaa mmoja nilimpenda sana akaanza kuniletea za kuleta, mwenzie niko kipindi cha mitihani ananiambia tutoke out tena sio pekeyetu tutoke na kundi la washkaji zake kisa washkaji zake wanatoka na mademu zao na yeye anataka awe na mie.... yeye alikuwa mfanyakazi.

Nikamwambia mwenzio nina mitihani, nikifeli ntakuwa mgeni wa nani? Akaanza kunihisi namkwepa ili niwe na vijamaa vya chuoni....

Hasira ikanipanda nikamwambia kama unanipenda kweli utanitafuta tuu hata baada ya mwaka, nikanyanyuka nikarudi chuo kusoma na wenzangu. Sikumtafuta, sikupokea simu zake hadi namaliza mitihani zaidi ya kujibu sms niko library, niko darasani, niko group discussion, nafua, najisomea mwenyewe, nalala kidogo.

Ratiba yangu ya mitihani alikuwa anaijua nilimpa kabla hivyo siku nimemaliza mitihani akaja hadi mlango wa chumba chetu hostel, kufungua ni yeye nikamrukia na kumkumbatia kwanguvuuuu.
 
Wakati nipo chuo kuna siku nililala na demu halafu kesho yake kulikuwa na test.
Asubuhi nimekurupuka nawahi kwenye test kumbe nimesahau Id geto, ikabidi niazime ID ya mwana ninayefanana.
 
Wakati nikiwa Form 3 nilifanya mbaaya kwenye mtihani hadi watu wakaulizana kilichonisibu bila wao kujua! Nilipata alama za chini mno ukilinganisha na uwezo niliokuwa nao kabla.

Nilikuwa muhuni sana! Sasa wakati huo wa kukaribia mitihani Mademu 2 nikawagonganisha, ikawa shida. Wakatishiana hadi kufanyiana mbaya!Ugomvi wao haukuishia mtaani, ukafika hadi shuleni! Na wakati huo kuna mmoja ni mdogo wa madame hapo school!!!!!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom