RD07
Member
- May 5, 2024
- 52
- 90
Nikikumbukaga huwa nacheka peke angu:
Nina brother angu ni kitombi sana nje ya ndoa, ana michepuko hasa.
Asa bana kuna siku kaenda kuoga kaacha simu ndani, mchepuko siukatuma msg na mkewe akaisoma, akampigia mchepuko na mchepuko nae akapaniki kuwa "wee kama nan unatumia hyo simu?" Wakalumbana simu ikakatwa, bro anatoka kuoga anaonyeshwa msg anatoa macho tuu + kigugumizi maana yaonekana hajawahi kudakwa ktk matukio yake.
Shemeji akampigia simu sister ambae ndo anafuatia akitoka huyo bro kwamba yeye ndo wakwanza kuzaliwa.
Sister ndo kaniambia twende huko kuna kesi tukasuluhishe, tukachukua toyo hadi kwa bro, kufika shem kapaniki balaa, akaanza kumuelezea sister pale mimi nipo kimyaa maana sikutaka kuingilia mambo yasonihusu. Asa sister akawaambia tuingieni ndani tuongee vizuri. Shem akatangulia na sister akafuata. Mimi nikatega niwe wa mwisho japo nlitaka nisiingie ila shem akaniambia njoo naww maana sio mtoto wew uje uone madudu ya kaka ako.
Bwana wee, bro akaitoa ile simu zilikuwa ni zile Nokia za batan nyingi (viji batan vidogodogo vingi kama mnazikumbuka), kulikuwa na ndoo imejaa maji pale nje bro akaitumbukiza kwenye maji baada ya kutoa betri akazitumbukiza zote kwenye maji (simu yenye ushahidi hyo). Anaulizwa mbona huji, anasema nakuja kumbe mwamba anaharibu ushahidi ilinibid nianze kucheka had machoz, bas nikajikausha namm nikaingia ndan. Kikao kikaanza kwa shem kuelezea tukio zima, basi bro kuulizwa kwann unafanya hiv bro anakataa anasema mm sielew chchte. Shem akamwambia sister "Wifi mwambie akupe hyo simu kama naongea uongo"
Sister anamwambia bro tunaomba hyo simu, bro anasema mimi sina simu. Shem anamuuliza umeiacha wapi siulikuwa nayo?, bro anawaambia simu ipo nje kwenye ndoo ya maji. Shem anatoka kwenda kuiangalia sasa ili ambananishe mhalifu wake, anakuta chombo inapiga mbizi kwenye maji. Anarudi anahamaki "Wifi kaka ako kaiweka simu kwenye maji, siunaona?, kaona aiweke kwenye maji maana anajua madudu yake yatafichuka". Asee mimi uvumilivu ulinishinda maana muda wote nlikuwa nimejiinamia chini nimelaza kichwa kwa magoti nacheka chinichini sitaki kumwangalia bro maana nahofia ntacheka kwa sauti mwisho maswali yahamie kwangu. Asa kwa tukio hilo na shem kuiona simu kwa maji asee nlijikuta naangua kicheko non stop, nikaona nitoke nje, nao uvumilivu ukawashinda wakaanza kucheka maana tayari bro alishajifunga kuwa ni kweli kwa makosa anayotuhumiwa ila tuu alichoficha n msg na namba ya mchepuko husika. Anaulizwa asa kwann umeweka simu kwnye maji kama sio kweli, anasema asa kama simu imedondoka kwenye maji mm nifanyeje?, Mimi mbavu sina kwa kucheka. Basi sister akawaeka sawa tuu kwa kumkanyaga sana bro kuwa keshakuwa mtu mzima aachane na mambo ya kando n.k.
Shem temper ilishuka baada ya tukio la kukuta simu kwa maji na mm kuanza kucheka nao wakapokea ikawa sasa kikao chote watu wanacheka had yeye mwenyewe maana bro ni kama alionyesha ukunguru flani hv, na akaona kamkomoa kwamba kaharibu simu kwa mistar kadhaa ya msg.
Badae namuuliza bro asa kwann umeamua kuharibu simu kisa nsg tuu siungeifuta na namba y huyo demu kulko kuiweka kwa maji. Aniambia nilikumbuka basi?, pia ningewapa ile simu ilikuwa ni bomu kuna majanga yakutosha mule.
Baada ya siku 3 akanipgia kuwa ile simu haijafa aliiweka juani na karudishia betry imewaka ila tuu ina ukungu kwenye kioo na ndo hyo anayonpigia nayo.
Asa hili tukio kiukweli nkilikumbukaga huaga nacheka tuu kama chizi.