Je, uliwahi kusahau kitu chako cha thamani kwenye usafiri wa umma, yaani Daladala, halafu ukakipata tena?

Je, uliwahi kusahau kitu chako cha thamani kwenye usafiri wa umma, yaani Daladala, halafu ukakipata tena?

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Mimi binafsi nimewahi kushuhudia mtu akilia kwa uchungu baada ya kusahau pochi yenye kila kitu kadi, hela, vitambulisho kwenye siti ya daladala. Hakujua hata jina la gari, wala namba. Hakujua pa kuanzia.

Kwa nini daladala zetu hazina mfumo wowote rasmi wa kutunza vitu vinavyosahaulika?

Wakuu, hivi unadhani kwa nini watu wengi hawarudishi vitu wanavyokuta kwenye daladala? ni umaskini au tabia tu?

1753623446359.png
​
 
Wallet ya pesa hupati
Labda kama vitambulisho
Na mtu akikuta wallet ina pesa na vitu vya thamani kama vitambulisho ndo usahau kabisa
 
Mimi binafsi nimewahi kushuhudia mtu akilia kwa uchungu baada ya kusahau pochi yenye kila kitu kadi, hela, vitambulisho kwenye siti ya daladala. Hakujua hata jina la gari, wala namba. Hakujua pa kuanzia.

Kwa nini daladala zetu hazina mfumo wowote rasmi wa kutunza vitu vinavyosahaulika?
1994, nilisahau vyeti vyangu kwenye chombo cha abiria.
Cheti cha chuo kikuu
Cheti cha chuo cha kati
Cheti cha form6
Cheti cha form4
Kadi zangu kadhaa.
Nilivipata baada ya saa 9 baada ya kuhangaika mnooo.
 
Kuna siku nakula zangu kitimoto roast safiiii,niliondoka nikasahau PC asee nilichukua boda kurudi kumbe yule jamaa pale kwenye kitimoto alinihifadhia akaniambia Sheikh utamu ulinoga sana!
Nilisahau Pua yangu na Meno kwenye Daladala
 
Picha inaanza napigiwa simu na bro.
"Dogo uko wapi(nikamwelekeza)"
Akanambia kimbia stend ya mwisho ya daladala
Namba ya hyo coaster T Blablablah ukiiona tu ,waambie nimekisahau kibegi rangi nyekundu.
Waambie kuna vitenge vya serikal.

Bahati nzuri nikaipata nikamwelekeza konda akasema..kaliona ila nimwambie ndani kuna nini.
Nikamwambia.."Vitenge vya serikal" Kufungua full kombati za jeshi.
Hakunidai ata senti ,na akasema hataki kesi na serkali.
 
Niliwahi angusha wallet ilikuwa na kitambulisho cha kazi,kadi za benk na pesa kwenye basi,baada ya kushuka nkachukua boda inipeleke nyumban,kabla sijafika home wazo likanijia ya kuwa jeans yangu niliyovaa mbon kama imekuwa nyepesi,ile kujisachi wallet haipo nkamuambia boda ageuze turud stend,nilipofika nkaulizia dereva wa lile basi,nkamuambia nimeangusha wallet,akaniuliza wallet ina nini,nikamwambia kilakitu kilichomo,kumbe alikuwa nayo yeye mwenyewe,akanipatia wallet yangu nikampa kama buku tano iv alishukuru sana,
Vitu vyangu vyote kwenye wallet nilivikuta
 
Kwa sisi ambao tumezoea kupambana tangu tukiwa wadogo kipindi cha nyuma kidogo,
Nilisahau nguo kwa ajili ya sikukuu za wadogo zangu kwenye costa niliteremka kwa gude naenda kiwalani gari inaenda tandika.

Mbaya zaidi zimebaki siku mbili au moja tu iwe sikukuu na sina pesa yoyote ambayo naweza fanya replacement ya zile nguo.

Nimefika home naulizwa na mama ulisema unakuja na zawadi, zawadi yenyewe iko wapi?
Oyaa Dah hii hali iliyo nikuta hapa sitasahau kamwe.

Ila Mungu ni mwema sana nilisahau na simu mule kwenye mfuko nilio weka nguo.

Na konda alikua mwema sana jamaa Mungu am-bariki aliko, saa tatu usiku aliipiga simu kwa namba ya mzee akatuelezea wanapo laza gari kwa bahati haikua mbali .
Mpaka saa nne na nusu usiku madogo wakarudisha tumaini jipya.
 
YAMEWAHI NIKUTA⛔️⛔️⛔️⛔️

Nilipokuwa ninaingia kidato cha sita nilipewa hela ya kununulia mahitaji pamoja na ada, nikanunua mahitaji yote ya msingi nikapanda daladala vile nashuka nikasahu dakika chache zilipita baada ya abiria kushuka narudi najaribu kumuuliza kondakta ananambia hawajaviona lakini dalili niliona kama wanajua mzigo huo lakini wakajifanya kama hawajauona.
 
Nilisahau IPAD toilet nilikumbuka baada ya 15 min nilirudi tu kwa kujiridhisha na nikaikuta
Sikuamini
 
Mm mara nne,mara tatu nilipata,mara ya mwisho sikupata!
Ya kwanza ilikuwa simu mwaka 2009 mwezi wa pili,dreva aliniwekea nikaipata kesho yake.. aliniletea mpk kituo nilichoshuka,sikuamini!
Mara ya pili ilikuwa ni vyeti,hapa nilikuwa na tiketi nikaanza kuisaka daladala mpk nilipoikuta parking kesho yake asubuhi na vyeti vyangu vilikuwamo kwenye bahasha A4
Ya tatu ni simu tena,hii ilianguka chini bahati nzuri hakuna abiria aliyeiona,sababu nilimkariri kondakta,nikaivizia stand kuingia ndani nikaikuta kama ilivyo chini ya seat..abiria waliokuwa seat za karibu wakitoa macho tu,bahati nzuri nadhani hakuna mtu aliyepiga.
Mara ya nne ilikuwa ni loss report hizo niliweka nyuma ya cover ya seat hivyo ndo nitolee mpk kesho!
 
Back
Top Bottom